Hivi ni sahihi kuanzisha kanisa unapohisi una upako?

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,793
2,000
Jaman, Asalaam aleikhum wale waislam na Tumsifu yesu kristo kwa wale wakristo mimi swali langu ni je?

Kama ni sahihi kuanzisha kanisa lako pale unapojihisi una upako wa roho mtakatifu?

Kama ni Yes je siku ya hukumu tutahukumiwa kwa imani zetu au kwa imani zetu na madhehebu yetu piaa kumekua na wimbi kubwa la watumishi ambao wanajiita watumishi wa Mungu mimi siwezi kusema ama ndio ama sio lakini maandiko yanasema

JIHADHARINI NA MANABII WA UONGO
Maana siku za mwishi watakuja wengi wakijiita manabii,

Naona sasa kuna watu wanachukua advantage ya ujinga wa watu fulani kama Fursa pia.
Huwezi kuhisi kuwa una upako isipokuwa unaweza kujua kuwa una upako. Kwa mfano, Mzee wa Upako Mch. Anthony Lusekelo, anajua kuwa ana upako, huwa hahisi kuwa ana upako.
Ukiona unahisi, huyo siyo Roho Mtakatifu (RM). RM huwa hawezi kuongea na muumini halafu akamuacha kwenye mashaka. Ukiona uko kwenye mashaka na unauliza lakini bado unaendelea kuwa kwenye mashaka, hapo unakuwa hujajibiwa. Kwa hiyo, hali hiyo uliyonayo wewe sasa hivi, nakushauri usifanye hilo jambo, bado hujaitwa! Usije ukalazimisha halafu ukawa uanasimama madhabahuni unaanza kurusha mapepo kwa waumini. Haya nayo pia yapo hasa kwa wale ambao hawakuitwa bali walilazimisha, wakiwa wanatafuta ajira Kanisani, tumeshayaona yapo!
 
Aqua

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
1,625

Mkuu wewe binafsi una amini Lusekelo ana upako wa Mungu Mwenyezi?
 
christmas

JF-Expert Member
Jul 21, 2011
2,662
2,000
Mungu anagawa karama mbalimbali kwa watu wake na ukipewa say karama ya uchungaji hiyo utasikia sauti ndani mwako mapema kabisa sio suala la kukurupuka wala Mungu wetu huwa hakurupuki.

Roho Mtakatifu atakupatia maelekezo yote kuanzia ni sehemu gani huduma yako itakuepo pamoja na kila kitu.

Ukiwa mtiifu na ukidumu kwenye maombi hakika hakuna kitu utafanya bila maelekezo na usaidizi wake yeye!!
 
Aqua

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
1,625
2,000
Siyo kwamba naamini, najua
Umekuwepo hapa Tanzania walau miaka kumi iliyopita?Au nikupunguzie kazi,Ile video yake amelewa anatukana majirani,gari lake limeziba njia uliiona?Baada ya lile tukio alihojiwa akaulizwa kama ni sahihi kunywa pombe,akajibu inategemea na kanisa.Unywaji wa pombe biblia haisemi unategemea na kanisa.Niishia hapo,lakini nataka ujue ya kwamba kuna kuwa mtumishi wa Mungu na kunakuitwa mtumishi wa Mungu wakati siyo.Kufanya miujiza siyo kigezo pekee cha mtu kuwa mtumishi wa Mungu,kufundisha Neno la Mungu hata kwa kutumia biblia haimfanyi mtu kuwa mtumishi wa kweli wa Mungu.
Kukemea watumishi wengine say mitume na manabii feki haimfanyi mtu kuwa mtumishi wa kweli wa Mungu.
Tunampima mtumishi wa kweli wa Mungu kwa kutumia Neno la Mungu na ushuhuda wa maisha yake.
Au nikupunguzie kazi; Yesu aliwauliza wanafunzi wake 'watu wanasema mimi ni nani?"
Sasa hapa wewe waulize watu "Lusekelo ni nani?" uwe tayari kwa majibu yao.Hili swali watumishi wengi hawako tayari kujua majibu yake.
Juzi juzi nimemuangalia anakemea wanaotabiri alikuwa sahihi mpaka nikadhan kabadilika,baadaye watu wanaitwa kuchukua vitu vya upako.
Hiki ni kipindi cha Mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo,wengi watapotea yamkini hata wateule.Kwa hiyo sishangai hawa kuwa na kundikubwa.
Simhukumu bali mimi namwangalia mtu kwa wakati huo,lakini kipimo sahihi nikuangalia Neno la Mungu linasemaje.
Neno la Mungu linasisitiza kabla ya kuwafundisha watu kitu,wewe kwanza ukiishi hicho kitu,unfortunately this is not the case now days.
Mtu kuwa mtumishi wa kweli wa mungu ni zaidi ya kutumia biblia,kufanya miujiza na kutabiri.Katika Agano jipya kwenye matendio ya mitume kulikuwa na jamaa Mchawi lakini alikuwa anaitwa mtumishi wa Mungu,haya mambo hayajaanza leo.That is why biblia inaposema hakuna jambo jipya chini ya jua,sisi tunaelewa hofu na mshaka ni kwenu.
Wandamu wanaweza wakakuita mtumishi wa Mungu wakati Mungu hakutambui au hujui kuna watu walitoa pepo na kuponya wagonjwa na wakomkuzimu?Kasome Biblia
 
Mtu kuwa na upako, haimaanishi kuwa amekuwa Malaika. Unaupima upako wa mtu katika muda ule ambao anakuwa amejiunganisha na Mungu halafu mambo mengine yote ameweka pembeni, na si vinginevyo; kwamba katika mazingira hayo, huyu mtu huwa anakuwa wa namna gani?.
Wewe ukiongea hayo huwezi ukawakubali watumishi walio wengi; ukwemo wewe mwenyewe pia, assuming na wewe ni mmoja wao
 
Biblia haijatuambia tumkubali kila mtu,imetuagiza tuzichunguze roho ili kujua kama zinatoka kwa Mungu,huwa sipendi kutaja majina lakini huyu amekija bahati mbaya.Sijakataa the so called upako kuja na kuondoka lakini Roho wa Mungu anaishi ndani,sasa mbona huongei kitu kuhusu zile video za kulewa ?Siwezi kuuasema mengi kwani si busara nimefunguka kwako just a portion ili kukusaidia,na anayeweza kukuokoa ni Mungu pekee na si ushawishi wa wanadamu.Soma biblia yako kwa makini,kisha mpime yeyote kwa kutumia Neno la Mungu na siyo miujiza,kwani miujiza hata shetani anafanya,si unajua Farao aliita wachawi na wenye akili nao wakageuza fimbo kuwa nyoka?
Kwa kukusaidia tu sasa hivi hapa Tz mbwa mwitu ni wengi,huwezi kuwatambua kama Neno la Mungu hulijua
Mtu kuwa na upako, haimaanishi kuwa amekuwa Malaika. Unaupima upako wa mtu katika muda ule ambao anakuwa amejiunganisha na Mungu halafu mambo mengine yote ameweka pembeni, na si vinginevyo; kwamba katika mazingira hayo, huyu mtu huwa anakuwa wa namna gani?.
Wewe ukiongea hayo huwezi ukawakubali watumishi walio wengi; ukwemo wewe mwenyewe pia, assuming na wewe ni mmoja wao
Mungu ni Mtakatifu na ili amtumie mtu ni lazima mtiu huyo ajitenge na yote ambayo Mungu anataka ajitenge nayo,nimekueleza yeyote anayejiita mtumishi wa Mungu maisha yake,tabia zake ni lazima ziwe mfano mzuri wa kuigwa katika jamii.kaome biblia yako kuna Kipindi Samweli aliwaambia wana wa Israel kama kuna mtu ana neno juu yake aseme alimanisha kama kuna ubaya wowote ameufanya.Watumishi wengi wasanii wewe usiyelijua Neno la Mungu vizuri unakamatwa na wala sishangai they are very deceptive lakini mimi kwa elimu na jinsi ninavyoyafuatilia haya mambo,ni ngumu.Mbona hujasema kitu kuhusu huyu mwenye upako kulewa chakali?
Mengine kuhusu huyu siwezi weka hazarania but in a nutshell anakazi kubwa ya kumtafuta Mungu na kurekebisha njia zake,trust me.
Nikusaidie tu wafuastilie hao jamaa au tafuta video zao,kisha sikiliza kama huwa wananena kawa lugha,na wakijifanya kunena kwa lugha kwa anayefahamu kunena kwa lugha atagundua kuna kitu kina miss katika kunena kwao kwa lugha.
Ndugu hizi ni nyakati za hatari,be watchfull,soma sana biblia na kuitafakari Mungu atakusaidia otherwise you are not safe.
Regards
aqua
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,793
2,000
Mungu ni Mtakatifu na ili amtumie mtu ni lazima mtiu huyo ajitenge na yote ambayo Mungu anataka ajitenge nayo,nimekueleza
Mungu alishawahi kuwatumia hadi makahaba kama akina Rahabu, na kuna nabii fulani, (nadhani ni yule aliyewahi kuongezewa umri wa kuishi miaka 15) aliambiwa aende akaoe kahaba.
Sikatai kuwa Mungu ni mtakatifu, na anahitaji utakatifu ila kumbuka pia amesema kuwa "njia zangi si njia zenu.........". Mungu anajua kila kitu, Anaweza kila kitu, Yuko kila mahali. Hata hapo ulipo wewe sasa hivi yupo pia
Kila alichokiumba Mungu ni kitakatifu kwake na anaweza kukitumia kama apendavyo yeye.
Nachelea kusema kuwa wewe ni mmojawapo kati ya watu wale ambao wamenyimwa kabisa roho ya kichungaji, huna hekima hiyo. Waache wale ambao wamepewa karama hiyo wamtumikie Mungu usiwabigudhi, usije mwishowe ukamsababisha akakugeukia na kukutandika
 
Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
1,102
2,000
Hakuna upako wala nini sanaa tupu, kila mtu anajiita mchungaji sijui nabii sijui malaika stupid na mama zetu hata hawashituki wanajazaaaaaana wakati mwingine hadi wanadhalilishwa na kuliwa uroda hovyo
 
Emmanuel180

Senior Member
Dec 17, 2019
187
250
The Bible

the Bible comands all of us to preach the Gospel to all creation. unatakiwa kuhubiri injili kwa kila kiumbe. lakini kuhusu kufungua kanisa, hakikisha Mungu amekuagiza ufanye hivyo, la sivyo utaenda peke yako. kila mtu, ukiachilia wito mkuu wa Mathayo 28 na 29, amekuja hapa duniani kwa mission fulani, Mungu ndiye atakuelekeza kwenye mission hiyo kwa utukufu wa Jina lake na kwa manufaa ya ufalme wa Mungu. ukijituma kuwa mchungaji au mwinjilist, huwezi kustahimili utakayokutana nayo kwasababu utaenda peke yako. ukiona una upako, hiyo ni opportunity ya wewe kuwa upo karibu na Mungu, ongea naye basi si upo karibu naye, akuelekeza yakupasayo kufanya hapa duniani.that's your very opportunity.
Utajuaje Mungu kaguagiza?

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom