Hivi ni sahihi kisarufi kusema nimekuja hapa tangu jana?

Hivi ni sahihi kisarufi kusema nimekuja hapa tangu jana?

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
Tangu ni neno ambalo hutumika kuonesha uendelevu wa jambo.

Mfano "magufuli ni raisi tangu mwaka 2015,hivyo kitendo cha magufuli kuwa raisi ni endelevu"

Hivyo ukisema "nimekuja tangu jana" sio sahihi kwa sababu wewe jana ndo ulikuja sio kwamba unaendelea kuja tuuu mpaka sasa,kitendo cha kuja kwako hapa kilisha isha tokea jana,kitendo kilichokuwepo ni kuwa wewe upo hapa.

Sahihi ni kusema "nipo hapa tangu jana" kwa hiyo tangu hapo inaonesha kuwa kitendo cha wewe kuwepo hapo ni endelevu hadi sasa.

Na kuhusu kuja ulikuwa useheme "nimekuja hapa jana"

Neno tangu usahihi hasa liambatane na "NA" ya wakati endelevu au "me ki" kuonesha jambo la mazoea.

Mfano wa "NA" endelevu.

1.Tangu mchana namtafuta yeye.(endelevu)
2.nimekuwa nikipiga chabo tangu nilipobaleghe.(endelevu)
 
Tangu ni neno ambalo hutumika kuonesha uendelevu wa jambo.

Mfano "magufuli ni raisi tangu mwaka 2015,hivyo kitendo cha magufuli kuwa raisi ni endelevu"..
Dah asante sana, tunaongea kiswahili ila kina ugumu sanaaa, nimefaidika na kupata elimu na mchango wako, ubarikiwe sana.
 
Nilikuja hapa jana na sio nimekuja hapa jana, nime---, hutumika kwa muda mfupi wa dakika
Ni sahihi mkuu lakini ukitumia li kwa vitendo hivi vya kawaida visivyokuwa vile vitendo ambacho havijirejei kama kifo n.k basi hiyo li huwa kana kwamba humaanisha kilifanyika kikapita.

Mfano ukisema "nilienda sokoni"
.hii sentensi bia shaka ina maana ya kuwa ulienda kisha ukarudi,huweza kusema "nilienda sokoni" alafu ukawa bado upo huko sokoni itakuwa haileti maana

Ama ukisema "nilikula" huwezi kusema nilikula huku ukawa unaendelea kula itakuwa haileti maana.maanake ulikula kitendo kikapita vikafanyika vitendo vingine kinyume na umekula pengine umemaliza muda mfupi tu hapo.

Na hivyo hivyo kusema "nilikuja hapa jana" kana kwamba amesharudi vile na AKAJA TENA, wakati yupo hapo hapo ambapo amekuja.

Ila ukisema "nimekuja hapa toka jana" maana yake baada ya kuja hiyo jana alibaki hapo hapo wala hakurudi.
 
Back
Top Bottom