Ndugu wana JF tumekuwa tukilaumu saana serikali yetu kwa mambo mbalimbali nakujiaminisha kabisa kuwa sasa ni wakati muafaka wa kukitoa Chama Tawala Madarakani. Nimekuwa nikijiuliza na hatimaye nikaona ipo haja ya kuileta hoja hii jamvini. Tukiitoa CCM madarakani, nani anafaa kuchukua madaraka kama Rais wa Tz. Anatoka Chama gani? Ameifanyia nini nchi yake? Je ni msafi? Hana kashfa au ufisadi wa aina yoyote? Si mbaguzi? Au nani anamfano wa watu wachache wazalendo wanaoweza kuongoza nchi yetu. Kwa maoni yangu naona hakuna mbadala katika kizazi cha sasa. Labda tuwaandae watoto wetu. Tukae kimya tujipange kwa miaka ijayo. Kwa sasa tukemee ufisadi. Nawakilisha!