Hivi ni kweli kwamba huwezi kuwa tajiri kama umeajiriwa au unamfanyia kazi mtu?

daxy Jr

Member
Apr 15, 2020
88
304
Kwema wakuu?

Mimi ni kijana wa miaka 20 na ndo kwanza nimeanza maisha ya kujitegemea na ndoto yangu ni kuwa tajiri siku moja.

Nimekua nikisikia baadhi ya watu hasa hawa motivational speakers wakisema kuwa huwezi kutajirika kama utafanya kazi za kuajiriwa tu na hii imenifanya kuona kama sipo kwenye njia sahihi ya kutimiza ndoto yangu.

Imekaaje hii wadau, kuna ukweli ndani yake?
 
Kabla hujatuuliza hilo swali tuoneshe tajiri mmoja tu ambaye unamfahamu ameajiliwa.

Halafu hakuna tajiri wa umri wako labda wa kurithi au land of opportunity kama Marekani.

Kwa nchi za dunia ya tatu una miaka mingine 20 ya kuukaribia utajiri kama utafanikiwa kujiajiri Kwa mafanikio.
 
Unaweza ukawa Tajiri kwa kuajiriwa kwa njia mbili kubwa :-

1. Uwe unalipwa mshahara mkubwa sana.
2. Uwe una matumizi madogo sana, kutoka kwenye huo mshahara.
Kisha ufanye kazi kwa muda wa maisha yako yote. Otherwise, sahau kuwa tajiri kwa kutegemea ordinary paycheck.
 
Kama umeajiriwa, convert your Salary into Passive income or Portfolio income. Kisha tumia hizo passive or portfolio kununua assets generating income hapo ndio unaweza kutimiza hizo ndoto zako kama ni kuwa tajiri otherwise zitakuwa wild dreams tu.
 
Kwema wakuu? Mimi ni kijana wa miaka 20 na ndo kwanza nimeanza maisha ya kujitegemea na ndoto yangu ni kuwa tajiri siku moja.

Nimekua nikisikia baadhi ya watu hasa hawa motivational speakers wakisema kuwa huwezi kutajirika kama utafanya kazi za kuajiriwa tu na hii imenifanya kuona kama sipo kwenye njia sahihi ya kutimiza ndoto yangu.

Imekaaje hii wadau, kuna ukweli ndani yake?
Dogo wenzie tunakimbiza 40+ na ndoto hiyo yako bado tunayo, fanya kazi na matajiri jifunze kutoka kwao wanafanye kazi zao, wanakusanya vipi mali, wanalipaje wafanyakazi na suppliers wao, ubunifu wao katika kazi zao ukoje na mwisho zaidi ni ile shuleni tulikuwa tunaita managers are getting things done by others.
Unawezaje kutumia akili za watu wengine kupiga noti na mwisho jifunze kutoamini hao speakers wanatia moyo na kufanya maisha mepesi wakati ni ngouma ngumu.
 
Kwema wakuu?

Mimi ni kijana wa miaka 20 na ndo kwanza nimeanza maisha ya kujitegemea na ndoto yangu ni kuwa tajiri siku moja.

Nimekua nikisikia baadhi ya watu hasa hawa motivational speakers wakisema kuwa huwezi kutajirika kama utafanya kazi za kuajiriwa tu na hii imenifanya kuona kama sipo kwenye njia sahihi ya kutimiza ndoto yangu.

Imekaaje hii wadau, kuna ukweli ndani yake?
labda uwe mwezi kama mawaziri wakurugenzi maris hapa sawa kwa mshahara ndoto
 
Kwema wakuu?

Mimi ni kijana wa miaka 20 na ndo kwanza nimeanza maisha ya kujitegemea na ndoto yangu ni kuwa tajiri siku moja.

Nimekua nikisikia baadhi ya watu hasa hawa motivational speakers wakisema kuwa huwezi kutajirika kama utafanya kazi za kuajiriwa tu na hii imenifanya kuona kama sipo kwenye njia sahihi ya kutimiza ndoto yangu.

Imekaaje hii wadau, kuna ukweli ndani yake?
Utajiri ni mtu kumiliki asset kuanzia kiasi gani?
 
Nautamani huo Umri wako aisee, yaani na huu ufahamu nilonao sasa kutajirika hata kama ingeshindikana ila ningekuwa napigania Kombe Moja tu .... 🤗
Kuna mda unatamani miaka irudi nyuma, dogo anayo nafasi kubwa sana ya kutengeneza utajiri kama atajitambua na kujipanga vzuri. Ila huo umri vijana huwa wanawaza na kufanya yasiyo ya msingi wanakuja kushtuka 27yrs
 
Back
Top Bottom