Hivi ni kweli kuna dawa ya mapenzi?

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
9,943
13,403
kwamba eti kuna mganga wa kienyeji mahali Fulani, anaweza kumrudisha mpenzi wako alie potea au kukutoroka au kukufanya upendwe sana na boss wako ofisini au akupe dawa ya kupandishwa cheo kazini?

Au akupe dawa ya mvuto wa kimapenzi?šŸ’

vipi ndugu, uliwahi kujaribu kupitia njia hii na vipi matokeo yalionekana? nini kilikuchochea šŸ’
 
Dawa za mapenzi zipo ila huko usukumani mjini wapo wanao ziagiza unaweza kumvuta ukafanikiwa ila shida dawa ikiisha shida inarudi tena na riba juu.

Kuhusu mvuto kazini mapenzi zipo ni kupata mtu sahihi au zikubali mfano mie dawa ya miti shamba hazinisaidiii hazifanyi kazi ila dua nikisali usiku nakuwa vizuri.

Unaweza kuona mganga tapeli hujafanikiwa lumber kwenu ni watu wa maombi sio miti.
 
dawa ya kupandishwa cheo ipo nimewahi shuhudia kwa ndugu yangu mmoja

aliomba apandishwe cheo, wiki tatu nyingi kapandishwa cha ajabu akaanza laumu si haki hii maana aliye tolewa alikuwa mchapakazi sana

yule bwana miezi kama sita aliamua kuokoka akisema dawa ni dhulma kwa wenye haki
 
Kama alikuacha muache tu aende zake, utajisikiaje na wewe mwanamke alokupenda kisha ukamuacha halafu usikie ameenda kwa mganga ili wewe umpende tena muwe wapenzi?

Acha hayo mawazo mkuu, kila jambo mshukuru Mungu, hujui ni yupi sahihi amekupangia ktk safari yako ya mahusiano.
 
Dawa za mapenzi zipo ila huko usukumani mjini wapo wanao ziagiza unaweza kumvuta ukafanikiwa ila shida dawa ikiisha shida inarudi tena na riba juu.

Kuhusu mvuto kazini mapenzi zipo ni kupata mtu sahihi au zikubali mfano mie dawa ya miti shamba hazinisaidiii hazifanyi kazi ila dua nikisali usiku nakuwa vizuri.

Unaweza kuona mganga tapeli hujafanikiwa lumber kwenu ni watu wa maombi sio miti.
una swali swala za usiku unapokuwa na tatizo au ni kawaida yako?
 
Achana na hayo mambo
Fanya kazi kwa bidii cheo kitapanda.

Ukiwa mwaminifu kwa mwenza wako na yeye atakupenda na kukuamini.

Ukitaka kuwa Boss fungua kampuni yako na wewe uajiri wafanyakazi uitwe Boss.

Kikubwa ni Kufanya kazi kwa bidii na Maarifa, Uaminifu, Subira na kujishusha
shida usipo jiweka fiti, cheo utashushushwa kwa wengine kukuendea kwa waganga

watu washa onesha sana bidii, sema nyota zao zimefifishwa na wahuni
 
Dawa za mapenzi zipo ila huko usukumani mjini wapo wanao ziagiza unaweza kumvuta ukafanikiwa ila shida dawa ikiisha shida inarudi tena na riba juu.

Kuhusu mvuto kazini mapenzi zipo ni kupata mtu sahihi au zikubali mfano mie dawa ya miti shamba hazinisaidiii hazifanyi kazi ila dua nikisali usiku nakuwa vizuri.

Unaweza kuona mganga tapeli hujafanikiwa lumber kwenu ni watu wa maombi sio miti.
Aise kumbe kuna kaukweli kwenye hili..
ila shida ni kwamba zina expirešŸ’

hapo kwenye dua patamu sana,

bilashaka mafanikio ni ya uhakika zaidi na yanadumu bila kuexpire...

thanks a lot madame
 
shida usipo jiweka fiti, cheo utashushushwa kwa wengine kukuendea kwa waganga

watu washa onesha sana bidii, sema nyota zao zimefifishwa na wahuni
aise kumbe sote tunapaswa kua wakakamavu na wenye bidii zaidi šŸ’

ukilegea kumuomba na kumshirikisha Mungu kazini katika kazi zako, unazidiwa nguvu na anaetegemea tunguli kazini dah šŸ’

kuna vitu hupaswi kutegea ee...
 
shida usipo jiweka fiti, cheo utashushushwa kwa wengine kukuendea kwa waganga

watu washa onesha sana bidii, sema nyota zao zimefifishwa na wahuni
Na ndiyo kitu ambayo changamoto kubwa sana maeneo ya utafutaji riziki hasa makazini kuna watu hawana huruma kabisa.

Yani utakuwa mtiifu, unapambana sana, hujihusishi na makundi mabaya na mazuri mengi tu ila kuna wahuni wana kutafuta kwa kila angle.

Noma sana
 
Hizo dawa zipo mkuu, kuna watu tulikuwa nao Mwanza ni watu wa kuamini madawa na uganga wa kienyeji sana katika maisha wanafuata sana maelekezo ya mganga wao,hao watu walitoka kigoma vijijini wakaja mwanza tufanya kazi pamoja,bosi alikuwa ndugu yao lakini alikuwa ananiamini mimi kuliko wao kwa kila kitu kazi zote zilikuwa zikifanyika kwa kunisikiliza mimi na sikuwahi kutumia dawa au kwenda kwa mganga niaminiwe,jamaa walifanya ushirikina nikafikwa na mitihani na kesi za ajabu julisha kuchukiwa na bosi hadi nikaondoka sasa hivi wamebaki wao wanatawala,ila hiyo ilikuja kutokea baada ya mimi kuacha kujibidisha katika dua na kusoma qur an kila siku ndipo mabalaa yao yakanipata.
 
Na ndiyo kitu ambayo changamoto kubwa sana maeneo ya utafutaji riziki hasa makazini kuna watu hawana huruma kabisa.

Yani utakuwa mtiifu, unapambana sana, hujihusishi na makundi mabaya na mazuri mengi tu ila kuna wahuni wana kutafuta kwa kila angle.

Noma sana
ukweli.
 
Hao Waganga wenyewe wanakuchukulia kidogo tulicho nacho na wanakutengenezea chuki na watu na wanakuondolea kujiamini. Muamini Muumba wako tu.
hao n waganga waongo
mganga wa kweli fedha hachukui sana
mganga wa kweli anakutibu bila kusema nan kakuroga

sema wengi tunakutana na waganga wapiga ramli chonganishi
 
Hapo ni hela ndo hufanya kazi, hao waganga wanakuwa kama wasindikizaji tu hamna uhalisia kwenye hilo. Bila pesa na kitu cha thamani hauna mvuto
Mkuu hao wote unao waona wanavuma kwenye tasnia nyingi wanatumia waganga na hizo dawa za mvuto,hata wanawake wa mjini wanaohongwa magari,nyumba,biashara kubwa wanatumia madawa kuwavutia watu.

kuna madalali waliwahi kumwambia jamaa mmoja alikuwa kaenda kununua nyumba maeneo flani dar,sasa akajifanya ni dalali wa maeneo mengine tofauti na hapo basi dalali mmoja wapo akawa anajisifu yaani yeye hata nyumba iwe mbovu vipi yeye akimuonesha mteja hachomoi kabla ya kuongea na mteja anajipaka hiyo dawa akiongea kitu wewe mteja hupindui utakuja kushtuka mlishafanya biashara.

Hizo dalala mnazopanda uliza madereva wtakuwambia mengi sana kuhusu madawa.
 
Kama ilivyo Good and Evil, Mwanga na giza, panapo nguvu za Mungu basi na za giza zipo......kikubwa ni kutoa sacrifice, kama kwa Mungu utatoa sadaka, kufunga, maombi n.k basi vice versa is true hata na upande wa pili utafanikiwa pale utapotimiza masharti, shida ni pale utapoacha kutekeleza masharti na kurecharge hizo nguvu za giza na maagano, kiufupi nguvu za giza huwa hazidumu. Mganga wa kweli ni Mungu na uchawi wetu ni sala/maombi.
 
Back
Top Bottom