Hivi ni kweli Asali ya Tabora sio nzuri kiafya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli Asali ya Tabora sio nzuri kiafya?

Discussion in 'JF Doctor' started by Brooklyn, Oct 24, 2012.

 1. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Wana JF habari za ujenzi wa Taifa?

  Mimi ni mtumiaji mzuri sana wa asali ya kutoka mkoa wa Tabora. Jana nilienda kuchukua mzigo wangu (asali) katika ofisi moja inayojihusisha na kusafirisha mizigo. Nilipokuwa nikitoka kuelekea parking kwa bahati mbaya au nzuri nikawa nimeongozana na jamaa mmoja ambaye naye alitokea kwenye hiyo hiyo ofisi nilitokea mimi.


  Akaniomba samahani kuna neno anataka kuniambia, nikamwambia bila shaka anaweza kunieleza. Akasema alinisikia nikitamka pale ofisini kuwa nimeenda kuchukukua asali na angependa kwa roho safi kunitahadhalisha juu ya matumizi ya asali kutoka mkoa wa Tabora. Akaniambia asali ya kutoka mkoa wa Tabora sio nzuri kiafya kwa sababu ina kiwango kikubwa sana cha nicotine kinachosababishwa na mazingira ya uzarishaji wa asali yenyewe. Nyuki wanapotengeneza asali huwa wanakuwa tayari wamefyonza chemicali za nicotine kwenye mimea ya tumbaku.

  Mwishoni akamalizia kwa kusema kuwa ndio maana nyuki kutoka mkoa wa Tabora wamepigwa marufuku kuuzwa/kusafirishwa nje ya nchi.

  Sasa nauliza kwa wadau werevu kwenye hili eneo je ni KWELI asali ya Tabora haifai kwa matumizi ya binadamu?

  Kama hivyo ndivyo, serikali na mamlaka zinazohusika mbona zimekaa kimya bila kuwaelimisha wananchi jii ya hatari hii.

  Angalau wangefanya kwenye pakiti za sigara, wawalazimishe wafanyabiashara waweke angalizo (disclaimer).
   
 2. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Weledi katika eneo hili mpo??
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Kabisa, Asali ya Tabora imepigwa marufuku kwenye masoko ya Jumuia ya Ulaya na Marekani na hii ni baada ya kugundulika kwamba ina kiwango kikubwa cha nicotine,

  Na hii imesababishwa na uharibifu mkubwa sana wa Mazingira, miti imekatwa imeisha na Nyuki wanakosa maua ya asili kwa ajili ya kutengeneza Nyuki, hivyo inapelekea kuchukua na maua ya Tumbaku ili kuongezea katika utengenezaji wa asali
   
 4. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Hili suala liligundulika mwaka juzi nchini Japani na kubainika kuwa hiyonasali ya Tabora ina kiwango kikubwa sana cha Nicotine.
  Hii inasababishwa na kilimo cha tumbaku Tabora, moshi wa kuni wakati wa kukausha tumbaku unabeba nicotine ambayo inaingia kwenye nta ya maua ya mimea ambayo nyuki wanakuja kuchukua na kwenda kutengenezea asali, matokeo yake asali nzima nayo inakuwa na Nicotine.

  Nicotine ina madhara kwenye mwili wa binaadamu.
   
 5. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Asante wakuu.

  Ngoja nimalize hii stock niliyonayo, sitaagiza tena.

  Je ni asali ya wapi nitumie kwa hapa Tanzania? Mi ni mpenzi sana wa asali, ningependa nijue ili nianze kuagiza mapema kabla mzigo nilionao haujaisha.
   
 6. Ansah Miles

  Ansah Miles JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 395
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Tafuta asali ya Mpanda-mkoa mpya wa Katavi,asali ambayo ni mbaya zaidi ni kutoka wilaya za Uyui na Urambo ambako ndio kuna mashamba makubwa ya tumbaku chanzo cha hiyo Nicotine,lakini ukibahatisha asali ya kutoka maeneo (wilaya) ya Nzega iko vzr,tatizo ukiwa dar ni vigumu sana kutofautisha imetoka wapi,sikonge sifahami,nawasilisha viongozi
   
 7. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Mi nilinunua hii ya katavi katika yale maonesha ya asaLi pale sabasaba Dar, Kumbe nili lamba Jike. Hureee!
   
 8. Bosco Ntaganda

  Bosco Ntaganda JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 551
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Maskini wakulima wa asali wa Urambo, Tabora
   
 9. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Ni kuchafuliana biashara huko, kwani Mpanda hawalimi tumbaku?

  Wala kwenye asali nicotine haijawahi onekana; tatizo ni madawa ya kuulia wadudu (pesticides na insecticedes) ndizo zilizoonekana kwenye asali hiyo, of course na moshi. Na swala la madawa sio kwenye tumbaku tu, hata kahawa na mazao mengine.

  Shida ya wafanya biashara wengi wa asali hata wa Mpanda ni uchakachuaji wa kuchemsha na kuongeza maji na sukari ili asali iwe nyingi.
   
 10. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,186
  Likes Received: 680
  Trophy Points: 280
  Kaunga, nicotine ni tatizo kwenye asali hasa inayotoka Tabora ambako kuna mashamba ya tumbaku. Rejea wavuti hii torita.or.tz/index.php?option=com_ars&view...format..., kuna utafiti uliofanywa kuangalia nicotine content kwenye maeneo yanayolima na yasiyolimwa tumbaku na matokeo yanaonyesha kuwa nicotine content ni kubwa kwenye maeneo yanayolima tumbaku (0.0033 - 0.0051 mg/kg). Pesticides residue na adultaration (uchakachuaji) ni tatizo pia.

  Kwenye masoko ya Ulaya na Marekani wana strict regulations kwenye quality za vyakula vinavyoingia nchini kwao ili kulinda afya za customers hivyo kama nicotine au pesticides residue levels ziko juu ya viwango vyao (EFSA for European Union; rejea www.efsa.europa.eu/en/efsajournal/doc/2770; kiwango cha nicotine kinachokubalika ni 0.01 mg/kg ) basi wata-reject asali yetu.. Na hii imeshatokea maana EU countries especially Beligium, UK, The Netherlands na German wanategemea asali yetu kwa kiwango kikubwa sana.

  Note:
  Kiwango cha nicotine kinachokubalika kwa soko la Ulaya ni 0.01 mg/kg na kiwango kilichoonekana kwenye asali ya Tabora ni kati ya 0.003 - 0.005 mg/kg..., Je Kaunga, sali yenye kiwango cha 0.005 mg/kg unadhani itakubalika kwenye soko la Ulaya..? Jibu ni HAPANA!

  Nasisitiza kuwa, traces za nicotine au pesticides residues ni ngumu kuziepuka kwa 100% ndio maanamashirik mbali mbali ya viwango vya chakula yameweka Maximum Residue Limits (MRL's) ambazo zinakubalika kwenye vyakula vingi tu na sio asali peke yake. Hivyo kazi kwako mlaji kuhakikisha kuwa unapata chakula ambacho hakina viwango vikubwa vya nicotine n.k.

  Ushauri: Kwa wapenzi wa asali kama mleta uzi hapo juu tumia asali ya Singida ndio the purest honey in Tanzania.

  Nawasilisha kama mtaalamu/nguli wa bioteknolojia ya chakula.
   
 11. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Safi kabisa mtaaalamu. Hivi na africa tuna AFSA Africa Food Safety Authority...coz tunakula mauzaua mengi tu kutoka china
   
 12. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,292
  Likes Received: 2,958
  Trophy Points: 280
  vip ya kigoma ni nzuri kama singida? ndiyo ninayotumia.
   
 13. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,890
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Na hiyo ya Singida sio yote ....achana na ya Manyoni nako kuna kilimo cha Tumbaku pia ....pata asli safi toka kwenye kilimo ambacho hakijachakakachuliwa na utumiaji wa madawa ya mazao!
   
 14. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,628
  Likes Received: 2,049
  Trophy Points: 280
  Mbona mnatutisha labda mngetuambia, kiwango gani cha hicho kilimo cha tumbaku maana unawezakuta maeneo mengine yana msitu ya kutosha na kilimo cha tumbaku ukilinganisha na ukubwa wa mistu iliyopo unakuta kilimo cha tumbaku kipo katika negligible percentage
   
 15. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,628
  Likes Received: 2,049
  Trophy Points: 280
  Ila soko limeharibiwa vibaya kweli maana zamani asali ya Tabora ndio ilikuwa ina jina hasa kibiashara na nakumbuka zamani kulikuwa kuna kiwanda kabisa kinasindika asali ya kopo, pole kwa kuharibiwa biashara ila usihofu endeleeni kuzalisha ila mnabadilisha lugha ya biashara na kuweka lebo kwa kuandika asali nzuri toka Kigoma maana zamani ukisema asali toka Tabora unapata soko
   
 16. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  mimi ndo maana natumia hile ya zanzibar tamu kweli!
   
 17. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kweli bwana, tatizo sie tunaonunua asali mbichi isiyo na lebo hatujui hata imetoka tabora au singida.
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Naona sasa hapa mmegeuza bango la matangazo, mimi navuta sigara na ina nicotine ya kutosha tu, kwahiyo asali yenye nicotine kwangu siyo issue.

  Mnajifanya mnaogopa nicotine wakati mafuta mnayopikia chakula colorestal kibao. Pambafu.
   
 19. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2013
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,856
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Mh.... kila kitu sumu!!!
   
 20. wende

  wende JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2013
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Agiza asali fresh toka mkoa wa njombe!
   
Loading...