Hivi Ni kweli alipokuja Mandela Tz alipata mapokezi makubwa kuliko Pope John Paul 2 au Obama?

Paima

Member
Oct 13, 2012
71
125
JK alipokuwa akihutubia kwenye mazishi ya Mandela alisema hakuna kiongozi yoyote aliyewahi kupokelewa na watu wengi kama Mandela alipokuja Tz, ukumbi mzima wakaanza kunong'ona kuashiria sii kweli. Wenye kumbukumbu nzuri tusaidie.
 

Ndakilawe

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
4,817
2,000
haiwezi kuwa kweli, coz wakati ule anakuja hata publicity ilikuwa chini sana! Technology kwa media ilikuwa low...Pope alipata watu, Obama kawaida...

Tanzania matukio ambayo yamekusanya umati mkubwa wa watu Ujio POPE JOHN II, MAPOKEZI YA MWILI WA NYERERE, wakati Mrema Lyatonga anahama kutoka NCCR-Mageuzi kwenda TLP?
 

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,263
2,000
Pope alikuwa na watu waliotembea kilomoeter kadhaa kufika kk sehemu ya hotuba kwa ile magari yalihitaji vibali maalumu kwa kazi maalumu ktk maeneo ya hotuba.Bado ni historia na record ya kuvunjwa.Kipindi kile cha Pope dini zote walikwenda watu kwa vile ilikuwa nadra sana kwa watanzania kupata ujio wa watu maarufu kwa staili ya kupita na kufanya mikutano ya wazi.
 

Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,504
2,000
Si unamjua JK! Alisema vile ili apigiwe makofi; aliyapata kweli. Mtu mmja hapa kasema hata media wakati haikuwa active kivile m; watu walikuwa wachache Dar. Isingewezekana Mandela, miaka ile ya tisini kupata umati mkubwa kumlaki kama ilivyokuwa Obama. Nafikiri mkuu alidanganya bila kudhamiria!
 

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,419
2,000
Alivyokuja Mandela mwaka 1990 alipkewa na watu wengi barabarani na baadae siku iliyofuata alikwenda Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) kuhutubia watanzania...Ikumbukwe kwamba kipindi hicho uwanja wa Uhuru uliokuwa na uwezo wa kubeba watu elfu 18 ulifurika....

Hata alivyokwenda Zanzibar alipokewa na umati mkubwa sana wa watu..

Hii ndio tofauti ya ziara ya Obama na Papa Yohane Paulo wa Pili....
 

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,419
2,000
Si unamjua JK! Alisema vile ili apigiwe makofi; aliyapata kweli. Mtu mmja hapa kasema hata media wakati haikuwa active kivile m; watu walikuwa wachache Dar. Isingewezekana Mandela, miaka ile ya tisini kupata umati mkubwa kumlaki kama ilivyokuwa Obama. Nafikiri mkuu alidanganya bila kudhamiria!

Kwani wingi wa watu unabainishwa na Media?....

Obama hafikii hata mapokezi aliyoyapata Papa Yohane Paulo wa Pili alipokuja Tanzania mwaka 1990
 

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
16,872
2,000
Si unamjua JK! Alisema vile ili apigiwe makofi; aliyapata kweli. Mtu mmja hapa kasema hata media wakati haikuwa active kivile m; watu walikuwa wachache Dar. Isingewezekana Mandela, miaka ile ya tisini kupata umati mkubwa kumlaki kama ilivyokuwa Obama. Nafikiri mkuu alidanganya bila kudhamiria!

Alifikiri yupo Nyarugusu kwenye kampeni za uchaguzi
 

CYBERTEQ

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
7,349
0
Hivi kukosoa kauli wa Rais wa nchi yako juu ya jambo hili la kitaifa na la kisiasa inatusaidia nini?

Kwani yeye anapoidanganya dunia msibani inatusaidia nini sisi kama watanzania?...Amini nakwambia, kila mtu huwa anabugi na anakuwa embarrased mara kadhaa katika maisha, hakuwa yeye pekee kituko katika msiba ule, hata Obama aliaibika pale alipoonekana wakijipiga picha na Cameron, tena wakitabasamu..huku Michelle akionekana kununua kwa pembeni! Ni heri hata hao wa kupiga selfie, sasa huyu wetu kudanganya uma kwa jambo ambalo liko wazi inatia shaka zaidi!..SHAME!
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
37,025
2,000
Hivi kukosoa kauli wa Rais wa nchi yako juu ya jambo hili la kitaifa na la kisiasa inatusaidia nini?

Ni kummzuia asipendelee kusema uongo katika mambo yaliyo dhahiri kwani ni aibu. Kwani akisema siku Mandela anakuja Tanzania hata jua liligoma kuzama magharibi bado wewe utaendelea kumwamini hutamkosoa?
 

Box 2

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
508
250
Kwani unaposema mapokezi makubwa unaangalia nini?,idadi ya raia wa kawaida waliojitokeza barabarani,idadi ya viongozi wa serikali waliohusika,idadi ya magari ama gharama zilizotumika?
 

TaboraONE

Member
Jun 30, 2013
8
0
Watz mnatakiwa msiwe wepes wa kukarir neno mojamoja na kubadilisha maana halis ya kilichosemwa. uvunjaj wa record aliomaanisha Rais c tu wa wing wa watu bali ni umat wa watu uliojitokeza ilihali kulikua na mvua inanyesha kipind hcho, hii ilimaanisha kuwa wakat Mandela anawasili Tz watu weng walijtokeza na mvua ikanyesha bt bla ya watz kujali waliendlea na mapokez. sasa jiulize na cku papa anapokelewa mvua ilikua inanyesha?...jiulize tena Madiba alikuja mwaka gani na papa alkuja mwaka gani hapa utaelelewa nguvu iliyokuwepo na alichomaanisha Rais.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom