Hivi Ni kweli alipokuja Mandela Tz alipata mapokezi makubwa kuliko Pope John Paul 2 au Obama?

Mtoa mada kapotosha JK alichokisema ni rekodi yake haijawahi kuvunjwa na sio kwamba haijawahi kutokea..! Swali; Pope Paul na Mandela nani alitangulia kuja? Obama anashikilia rekod ya Usafi, Ulinzi labda na kuchezea mpira
 
JK alipokuwa akihutubia kwenye mazishi ya Mandela alisema hakuna kiongozi yoyote aliyewahi kupokelewa na watu wengi kama Mandela alipokuja Tz, ukumbi mzima wakaanza kunong'ona kuashiria sii kweli. Wenye kumbukumbu nzuri tusaidie.

Kuna ugonjwa unaitwa " habitual lairs" huu ugonjwa umeingia kwa viongozi wetu na unaambukiza kam hysteria vile
 
POPE si kiongozi wa nje; he is beyond that.
Rais amesema kiongozi wa nje, na amesema kweli, Obama alipata watu gani? kwanza watu walizuiwa sasa utakompareje ujio wa Obama na Mandela?

Tuwe watu makini; tusidakie dakie maneno kama watu wasiolelewa vema. Umati wa watu waiompokea, na kumzika Nyerere ni sawa na ujio wa kiongozi toka Nje?????? TAFAKARI, TUMIA AKILI.

Rais ameongelea mapokezi ya wageni
 
Kumbukeni henzi hizo tunajipanga barabarani kutoka airport mpaka ikulu. Mie nakubali mapokezi ya mandela ni makubwa mno na ushuhuda siku hiyo wanafunzi wote wa shule ya uhuru tulishinda tukiimba mpaka jioni alipopita.
Siku hizi viongozi wanapita mbio na enzi za nyerere na mwinyi ni hado hado na wanapunga mikono.
 
Naomba tutoe facts and figures, mtujuze Madiba alipokelewa na watu wangapi, Pope na Obama walipokelewa na wangapi respectively!
!
 
Si unamjua JK! Alisema vile ili apigiwe makofi; aliyapata kweli. Mtu mmja hapa kasema hata media wakati haikuwa active kivile m; watu walikuwa wachache Dar. Isingewezekana Mandela, miaka ile ya tisini kupata umati mkubwa kumlaki kama ilivyokuwa Obama. Nafikiri mkuu alidanganya bila kudhamiria!

Hata alipokuja Obama nakumbuka alisema idadi ya waliokuja kumlaki haijawahi kutokea!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Naona unakurupuka ndugu....

Heading ya thread inasemaje?..Ama ndio mambo ya kuongeza posts?

Naona haujanielewa!Heading inasomeka:
Hivi Ni kweli alipokuja Mandela Tz alipata mapokezi makubwa kuliko Pope John Paul 2 au Obama?

Ulinganifu ni kati ya Ziara ya Madiba na Obama, au Madiba na John Paul II, na si kati ya Obama na John Paul II!!!!!:bored:

Nadhani una busara ya kutosha kuona nani anakurupuka.
Kazi njema.
 
Hivi kukosoa kauli wa Rais wa nchi yako juu ya jambo hili la kitaifa na la kisiasa inatusaidia nini?

mkuu, mtu yeyote anapotamka kitu kinacholeta taswira ya uongo huonesha jinsi alivo, lkn la muhim zaid ni kujitambua vnginevyo acha watu wakusahihishe ili ujifunze kusema ukiwa na conscious mind
 
Naona unakurupuka ndugu....

Heading ya thread inasemaje?..Ama ndio mambo ya kuongeza posts?

Balantanda
Habari yako mkuu .Long time sana kaka .JK pale alichapia nina uhakika .Pope aliokuja Tanzania Watanzania walitoka Mikaoni na Tanzania karibia yote hata wakenya waliuja kuanzia uwanjani hadi Ikuku na Jangwani ilikuwa issue nyingine ile .JK leo kafanya vyema sana mimi si mpenzi wa CCM but Mtanania I am happy kwa aliyo yasea kasoro la Pope Mandela hakuweza fikia .
 
Si unamjua JK! Alisema vile ili apigiwe makofi; aliyapata kweli. Mtu mmja hapa kasema hata media wakati haikuwa active kivile m; watu walikuwa wachache Dar. Isingewezekana Mandela, miaka ile ya tisini kupata umati mkubwa kumlaki kama ilivyokuwa Obama. Nafikiri mkuu alidanganya bila kudhamiria!

Ni uongo kwa wasiojua history. Ziara ya Mandela na Pope John Paul II zilipishana kwa miezi sita tu. Mandela alikuja March 1990 na Pope alikuja September 1990.

Wote Mandela na Pope walikuwa na popularity. Kama utakumbuka kuna mwaka 1982 bendi ya DDC Mlimani Park ilizawadiwa kuwa bendi bora nchini kwa kupiga wimbo wimbo uliovuma sana uliosisitiza Nelson Mandela afunguliwe, tena wakati huo tukidhani bado yuko Robben Island.

Vilevile, bendi iliyokuwa ikiitwa Watu Njatanjata ya akina Eddy Sheggy nayo iliimba wimbo MANDELA NI MWANA WA AFRIKA AFUNGULIWE MANDELA.

Kuhusu ziara Pope alitembelea miji mitano yaani Dar, Songea, Arusha, Mwanza na Tabora. Na kote huko vilijengwa vibanda rasmi kumpokea maana viwanja kama Uwanja wa Taifa alikofikia Mandela havikutosha.

Kuna magazeti ya kizushi duniani yalitabiri kwamba Pope Francis angehudhruria mazishi ya Mandela lakini kwa tunaojua tulisema isingewezekana. Ziara ya Pope lazima iwe organised si chini ya miezi nane kabla ya kutoka pale Vatican.
 
JK alipokuwa akihutubia kwenye mazishi ya Mandela alisema hakuna kiongozi yoyote aliyewahi kupokelewa na watu wengi kama Mandela alipokuja Tz, ukumbi mzima wakaanza kunong'ona kuashiria sii kweli. Wenye kumbukumbu nzuri tusaidie.

Kaka mjini umekuja lini yawezekana ukabisha kumbe umechelewa kuja mjini
 
Watz mnatakiwa msiwe wepes wa kukarir neno mojamoja na kubadilisha maana halis ya kilichosemwa. uvunjaj wa record aliomaanisha Rais c tu wa wing wa watu bali ni umat wa watu uliojitokeza ilihali kulikua na mvua inanyesha kipind hcho, hii ilimaanisha kuwa wakat Mandela anawasili Tz watu weng walijtokeza na mvua ikanyesha bt bla ya watz kujali waliendlea na mapokez. sasa jiulize na cku papa anapokelewa mvua ilikua inanyesha?...jiulize tena Madiba alikuja mwaka gani na papa alkuja mwaka gani hapa utaelelewa nguvu iliyokuwepo na alichomaanisha Rais.

Hii ndiyo tabu ya kuchanganyika na kindergaten mitandaoni. Mandela alimtangulia miezi zita tu Pope John Paul II.
 
Mtoa mada kapotosha JK alichokisema ni rekodi yake haijawahi kuvunjwa na sio kwamba haijawahi kutokea..! Swali; Pope Paul na Mandela nani alitangulia kuja? Obama anashikilia rekod ya Usafi, Ulinzi labda na kuchezea mpira

Hii ndiyo taabu y akuvamia mitandao maadam tu unajua ku-press keyboard. Hivi ina maana hujui kwamba Mandela alimtanguli Pope kwa miezi sita tu yaani Manela alitua Dar March 1990 na Popo John Paul akaja September 1990.

Acha kuparamia. Acha uvivu wa kusoma hasa history.
 
Watu waliompokea Mandela walikuwa wengi zaidi ya waliompokea papa paulo. Watu waliompokea Obama sina la kusema kwa sababu wakati Obama yupo Tanzania mimi sikuwa nchini.
 
Ni uongo kwa wasiojua history. Ziara ya Mandela na Pope John Paul II zilipishana kwa miezi sita tu. Mandela alikuja March 1990 na Pope alikuja September 1990.

Wote Mandela na Pope walikuwa na popularity. Kama utakumbuka kuna mwaka 1982 bendi ya DDC Mlimani Park ilizawadiwa kuwa bendi bora nchini kwa kupiga wimbo wimbo uliovuma sana uliosisitiza Nelson Mandela afunguliwe, tena wakati huo tukidhani bado yuko Robben Island.

Vilevile, bendi iliyokuwa ikiitwa Watu Njatanjata ya akina Eddy Sheggy nayo iliimba wimbo MANDELA NI MWANA WA AFRIKA AFUNGULIWE MANDELA.

Kuhusu ziara Pope alitembelea miji mitano yaani Dar, Songea, Arusha, Mwanza na Tabora. Na kote huko vilijengwa vibanda rasmi kumpokea maana viwanja kama Uwanja wa Taifa alikofikia Mandela havikutosha.

Kuna magazeti ya kizushi duniani yalitabiri kwamba Pope Francis angehudhruria mazishi ya Mandela lakini kwa tunaojua tulisema isingewezekana. Ziara ya Pope lazima iwe organised si chini ya miezi nane kabla ya kutoka pale Vatican.

Nimevutika hapo mlipodhani alikuwa Robben Island....kumbe alikuwa wapi kwa wakati huo??
 
To be honest Pope John Paul II had won the crowd than any guest whom has come to Tanzania. This is a fact. ..:thumbup:
 
Back
Top Bottom