Hivi ni kwanini kuna watu kila jambo la maendeleo linalofanywa na Serikali wanachukia?

Utakuwa unatoka ktk familia ya ki-ccm.
Mkuu Mimi nikupe siri moja ni kijana tu ambaye baada ya kusoma shahada yangu na kujifunza vingo toka nikiwa chuo kikuu nimekuja kugundua wapinzani wengi wanafanya siasa za kijinga sanaaa,isitoshe nimemaliza shahada yangu mwaka 2018 mpaka sasa sina Ajira lakini.Maana usije ukani judge kwambaa nakula mema ya nchi la hasha.Uzalendo tu wa JKT na kukaaa mtaani kuona mambo makubwa ambayo serikali inafanya nikikaa na kuona naumia sana yani natamani niingie kwenye vichwa vya hao wanasiasa wa kipinzani wanaotafuta kiki kila kukicha.Maendeleo hayana vyama mkuu,hii ni nchi yetu sote tuijenge.Nadhani umenielewa Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umechambua vizuri hoja kiuchumi mwisho ukahitimisha kinazi.

Ngoja nikurejeshe kwa ulichokiandika, :

...maendeleo ndo yanajenga nyumba. Ni sahihi kabisa kama utasfsiri maendeleo kwa maana ya kuwekeza ulichonacho kuongeza pato la kukuwezesha kumudu mahitaji yako ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba. Na umesema kwa kudai kwamba mchaga akipata pesa hajengi nyumba wala kununua gari bali ataitumia kutufuta maendeleo kwanza kwa maana ya kuongeza productivity yake.

Unahitimisha kwa kukanusha hoja yako hiyo, unaposema ...kwangu Mimi kukopa tirions of money kujenga reli wakati nguvu kazi ya taifa lako hawana elimu bora,watoto wanakaa chini huku darasa moja likiwa na watoto zaidi ya mia ishirini na mwalimu mmoja ni uzuzu. Je, hayo utayamudu kwa jinsi ipi kama hukuwekeza kwenye njia kuu za kuongeza pato?
Mkuu serikali haifanyi biashara na hakuna nchi iliyoendelea kwa serikali yake kufanya biashara,reli bila kubeba mzigo haiwezi kuzalisha pesa,sasa swali ni je reli hiyo itabeba mizigo ya nani wakati productivity ya watu wako ikiwa sifuri? Wekeza kwenye productivity then productivity ndo itajenga reli
 
Boss! Hiyo ndo haki ya watu wanaojifanya ni wa maana kuliko wengine. Mimi ni mkulima na kazi yangu haina taabu na Magufuli na polisi. Wewe unayeamini umeajiliwa na siasa, usituingize kwenye tabia yako kwa kujidai eti unatupigania. Hatukukutuma, ulijipeleka mwenyewe. Kama unaona kupigwa na kuvunjwa mkono ni mtaji, pigwa tu!
Aisee.... ya wakulima wa korosho umesahau..? Ya wakulima wa mbaazi umesahau..?? Kiongozi, zami tu yako haijafika.. na mara zote mtu hujiona yuko salama kwa kudanganywa na zamu..
 
Aisee.... ya wakulima wa korosho umesahau..? Ya wakulima wa mbaazi umesahau..?? Kiongozi, zami tu yako haijafika.. na mara zote mtu hujiona yuko salama kwa kudanganywa na zamu..
Korosho zipi? zile za shamba la Zitto? Nalima mahindi na mpunga. Nilijaribu Korosho nikaona inaleta taabu, nikajaribu Pamba kule simiyu, nayo ikaleta shida pamoja na ukame nikaacha. Hawa wanaopigwa kwa nini hawaachi wajaribu kazi nyingine? Au ni nono sana! Wakomae tu! Wapigwe tu, lakini wasituhusishe ni akili na uzembe wao. nasema tena sihitaji mtu ajifanye yuko ktk siasa kwa niaba yangu.
 
Aisee... Zito ndo analima korosho Kusini mwa Tanzania..!!?? Wale wanajeshi walienda kusini kukusanya korosho za Zito..?? Kumbe huna hoja
 
..sisi ndugu zenu wapenda mabadiliko, mashabiki na wanachama wa vyama vya upinzani.
Tafuta kazi ya kutumia akili boss! Hayo mambo ya kushinda majukwaani haina maana. Kwani kuwezi kutumia akilia yako kupambana na maisha, au huna?
 
Tafuta kazi ya kutumia akili boss! Hayo mambo ya kushinda majukwaani haina maana. Kwani kuwezi kutumia akilia yako kupambana na maisha, au huna?

..napambana na maisha.

..pia napambana na ccm, polisi,na dola, ili kuleta mabadiliko ya kweli nchini kwetu.
 
Back
Top Bottom