Hivi ni kwanini kuna watu kila jambo la maendeleo linalofanywa na Serikali wanachukia?

mazaga one

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
558
500
Wakuu nashindwa kujua shida ni nini.Maana Mh Rais alisema maendeleo hayana vyama sasa kulikoni kila jambo la maendeleo ambalo Serikali inafanya kuna baadhi ya watu wanakasirika na kuombea kabisa hayo mambo yasifanikiwe.

Inajengwa reli ya kisasa ya SGR kuna kuna watu wanaomba mradi usiishe mapema,mradi wa kisasa wa umeme na mengine mengi tu.

Hivi juzi juzi pia serikali imetoa Ajira 1000 za madaktari na pia wameahidi kuajiri walimu lakini ukifatitilia kiundani kuna watu kama hawapendi au wanaumia kuona haya mambo mazuri yakifanyika.Shida ni nini Wakuu?

Ahadi ni Vitendo!

Awamu ya tano,Hapa kazi tu!
JPM kazini!
Nawasilisha!!!
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,402
2,000
Hostel mbovu, bomba limekwama, SGR inaangamia, Mikopo vyuo vikuu kapunguza, Elimu bure watoto wanakaa chini tena secondary.

Angalia alivyotesa wakulima wa korosho na mbaazi

Pesa yote kawekeza kwenye kuua, kuteka, kununua wapinzani, kuhujumu vyombo vya habari na kuwapa kesi za uhujumu uchumi watu wasiokubaliana naye

Utapendaje mambo yake mtu kama uyo labda uwe punguani.
 
Mr Big

JF-Expert Member
Sep 16, 2019
478
1,000
Let me give out my opinion like this....

1.siasa nyingi za kipinzani kwa africa zimekaa kupinga chama tawala,au mtawala aliyepo,hata bila sababu ya msingi.
Hutasikia mpinzani anampongeza mtawala juu ya jambo fulan jema.
2.iman potofu kwamba upinzani ndio chama bora cha kuleta mabadriko yaliyokosekana.
Kitu ambacho si kwel.

3.watawala wenyewe,chama tawala kuwafanya wapinzan kama mbwa koko,kuwapinga kila jambo na kuwasurubisha.hatimaye wapinzani kuamua kupinga kila jambo maana wana banwa mno,kama jera wao,mikutano kukatazwa wao!

So bora wapinge kila kitu..yaan watoto wa mjin wanasema kama mbwai na iwe mbwai!!
 
google helper

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
8,113
2,000
Wakuu nashindwa kujua shida ni nini.Maana Mh Rais alisema maendeleo hayana vyama sasa kulikoni kila jambo la maendeleo ambalo Serikali inafanya kuna baadhi ya watu wanakasirika na kuombea kabisa hayo mambo yasifanikiwe.

Inajengwa reli ya kisasa ya SGR kuna kuna watu wanaomba mradi usiishe mapema,mradi wa kisasa wa umeme na mengine mengi tu.

Hivi juzi juzi pia serikali imetoa Ajira 1000 za madaktari na pia wameahidi kuajiri walimu lakini ukifatitilia kiundani kuna watu kama hawapendi au wanaumia kuona haya mambo mazuri yakifanyika.Shida ni nini Wakuu?

Ahadi ni Vitendo!

Awamu ya tano,Hapa kazi tu!
JPM kazini!
Nawasilisha!!!
ni ngumu sana kumfurahisha mtu mwenye njaa, unajua kucheka ukiwa na njaa hata mbavu zinauma so ni vzuri kwanza tupewe chakula alafu utaona vile tunatoa cheko kwa kila utakachofanya ww na wenzio wa awamu ya tano.
 
Top Bottom