Hivi ni kuna uweli kwamba wanaume nao husengenya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kuna uweli kwamba wanaume nao husengenya?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by vukani, Jun 27, 2012.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hebu chukulia umechelewa kufika kazini , unapofika ofisini unasikia sauti za wafanyakazi wenzako wakizungumza kwa ndani, unapofungua mlango na kuingia, ghafla wananyamaza na kukuangalia kwa mshangao!

  Jiulize walikuwa wanazungumzia nini?

  Kwa kuangalia mfano huo kwa haraka utagundua kwamba walikuwa wanazungumzia jambo linalokuhusu au walikuwa wanakusengenya. Kwa mujibu wa watafiti mbalimbali, imethibitishwa kuwa wanawake na wanaume wote wanasengenya, labda kinachowatofautisha ni uwiano kwamba wanawake ndio wasengenyaji wazuri zaidi ya wanaume.

  Hebu jaribu kutembelea kwenye saluni za kike na za kiume, utakuta hakuna kinachozungumzwa huko zaidi ya kusengenya, tena kibaya zaidi ni usengenyaji wa kubomoa na kuharibu umaarufu wa watu wengine.

  Kwa mfano kama wamemtembelea mwenzao au kuhudhuria mazishi ya msiba unaomhusu mwenzao, shuhudia mazungumzo yatakayotawala wakati wanarudi.

  Njia nzima mjadala utakuwa unahusu maisha ya mwenzao, kwamba hana hiki , hana kile, au mazishi hayakuwa mazuri kama ya fulani, pia hata kulinganisha thamani ya jeneza la maiti na umaarufu wa mhusika. Utawasikia wakisema “kuringa kote kule kumbe si lolote wala si chochote, ndani kwake kubaya, hana hata kitu cha thamani ukilinganisha na mavazi yake na umaarufu wake”.

  Litazungumzwa hili na lile ilimradi tu kumbomoa mhusika.
  Hivi karibuni niliamua kufanya kautafiti kadogo kwa kuwauliza baadhi ya watu nilio nao karibu na wapita njia wengine. Nilizungumza na baadhi ya wanawake pamoja na wanaume kadhaa kuhusu hili suala la kusengenya. Dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sharifa, alithibitisha kuwa ni kweli sisi wanawake tunaongoza kwa kusengenya, lakini alitetea kuwa kuna tofauti ya kusengenya na kumzungumzia mtu au watu kwa mazuri na mafanikio yao.

  Sharifa alibainisha kuwa sio vibaya kumzungumzia mtu kutokana na mafanikio yake, kwani hiyo kuwapa fursa ya kujifunza kulingana na mafanikio ya mwenzao, pia hata wanapozungumzia mapungufu ya mtu, hiyo ni kwa ajili ya kujifunza kutokana na mapungufu ya mwenzao. Dada mwingine aitwae Bupe, alisema kuwa hata wanaume nao husengenya, yeye alishawahi kumfuma mvulana ambaye punde tu alitoka kufanya naye mapenzi akiwasimulia wenzake jinsi yeye (Bupe) alivyo awapo kitandani, kuanzia mwili wake hadi namna anavyofanya mapenzi.

  Ukweli ni kwamba hakuamini tukio lile kwa sababu mvulana aliyemwamini na kukubali kuwa mpenzi wake baada ya kumtongoza kwa muda mrefu, angeweza kusimulia yale yote aliyoyasikia. Kibaya zaidi hata wale waliokuwa wakisikiliza ule utumbo walionekana kwa nje, kuwa ni watu wenye busara.
  “Usiwaone wamekaa kwenye makundi wakizungumza ni wasengenyaji wazuri sana, tena usidhani wanajadili jambo la maana, sanasana wanazungumzia wanawake wale waliotembea nao” alisisitiza Bupe.

  Kijana mmoja aitwae Dikupila ambaye anamiliki saluni ya kunyoa nywele jirani na ofisi ninayofanya kazi, kwa upande wake aliwatetea wanaume kuwa siyo wasengenyaji, alidai kwamba hayo ni mambo ya wanawake.
  “Sisi wanaume kusengenya! Haiwezekani, hayo ni mambo ya wanawake, sana sana ukikuta mwanaume anajadili udhaifu wa mpenzi wake hadharani basi ujue huyo jamaa anamatatizo makubwa ya kiakili” alisema Dikupila.

  Watu wengi wa jinsia tofauti niliobahatika kuzungumza nao walikuwa wanakiri kusengenya lakini walikuwa wanajaribu kutengeneza fasili ya neno kusengenya kwa namna ya kukidhi haja zao. Kwao kusengenya walisema ni mtu kutafuta namna ya kujifunza kuwa bora kupitia makosa ya wengine. Je tabia hii inaweza kuachwa? Wengi walikiri kwamba siyo rahisi tabia hiyo kuachwa kwani imekuwa ndiyo sehemu ya maisha, kwamba haiwezekani watu kukaa pamoja na kuacha kuzungumza matukio na yanapozungumzwa matukio, ni lazima yatawahusu watu hivyo kujikuta watu wanasengenya.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  nikiingia mahali watu wakanyamaza sifikiri kama walikuwa wananisengenya.

  Ila wanamme wanaosengenya wapo, tena mwanamme anayesengenya huwa haachi anawazidi hata wanawake.
   
 3. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Wanaume kusengenya si kwa saana kivilee, huweza kusengenya inapobidi (na hasa hawa hua wanaume makini) Btw wanaume wao hua sana WANATETA.
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  wanaume wanaosengenya wapo, tena hakuna watu wambea kama wanaume....
   
 5. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,994
  Trophy Points: 280
  Tena ktk dunia hii hakuna viumbe wambea-sengenyaji kama wanaume.
  Tena wakikutana Chemba utawasikia,
  ...umeona Pm ya Madame B aliyonitumia?
  Then mnaonyeshana.
  ...nyie nikiwakamata...
  NAWAMEZA BILA MAJI.
   
 6. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  We mtoto taratibu basi, huna dogo!
  Una source ?
   
 7. Mwanyasi

  Mwanyasi JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 5,761
  Likes Received: 1,895
  Trophy Points: 280
  Mwongooooooooooo, labda wawe ndugu zake Cameroon
   
 8. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ukiingia watu wakanyamaza,yawezakana anasimulia:-
  1. mfano wanasimulia jinsi alivyomchukua changudoa na kufaidi usiku uliopita, sio vyema mtu wa jinsia nyingine(mdada) asikie uliofanya utakuwa unamdhalilisha na kupoteza heshima kwake, so akiingia mnapiga kimya.

  2. Ninakuzimikia ww ulie ingia na kila nikitupa ndoano, unanipiga chin najaribu kutafuta msaada kwa washkaji wanipe maujanja so ukiingia lazima tupige kimya usijesikia mikakati ya kukutokea.

  3.mkiwa ofis moja lazima mchunguzane nyie wanaume ni nani anamchukua nani ili msije mkagongana kwa dem( samahan msichana) mmoja alaf mkaleta tiff, au msije mkachukua kifaa cha boss alaf kibarua kikaota nyas, so wakati wa kutafuta hizo taarifa ukiingia tunapiga kimya, coz hata ww unahuksika.
   
 9. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Aalaaaaaaa ndo yale ya boss asipojibu barua yuko bize karani asipojibu ni mzembe......kupuu apuu kuku akipuu bata.....
   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Hata humu chit chat wapo wengi tu
  sijui niwataje.

   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  hiyo ndo hali halisi, si mashuleni si maofisini, halafu watunzi wazuri wa majungu
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  hahahahahahaha
  sosi jei efu!
   
 13. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,675
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Wee binti mbona unatukandamiza hivo wanamume? Kusengenya ni ktk matendo ya kike bana kama kuvaa hereni na vipuri, so ukiliona dume linavaa hereni, vipuri au kusengenya jua ana homoni za kike huyo hivyo sio mwanaume kamili (analo jina lake)

   
 14. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,016
  Likes Received: 23,738
  Trophy Points: 280
  Unataka kuniambia hizi njemba zinaweza kuwa zinasengenya? Siamini asee!!

  [​IMG]
   
 15. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  punguza jazba! wamasai wanavaa hereni na kusuka nywele. does that mean wao sio 'wanaume kamili'?
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  Sana tu,
  halafu my hazbendi huyo kaka kakalia kisu?   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  Hawavai hereni wala vipuri.... Ila ukiwakuta wanaoiga majungu, au utabaki mdomi wazi.... Tehetehteh   
 18. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Tena hawa ndo proffesional,hadi wana bunduki
   
 19. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,016
  Likes Received: 23,738
  Trophy Points: 280
  Hahahaha wife bana, hebu angalia vizuri afu unambie kwa PM. Nna mahaba na PM zako ujue. Weekend hii twende wapi?
   
 20. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,675
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  noooo!!! Sikumaanisha hivo mkuu, wamasai huvaa kama desturi ya mila zao, nadhani hapa twazungumzia mambo ya kawaida kabisa na si mila ama tamaduni fulani!
   
Loading...