Hivi ni kilimo kwanza au kilo kwanza

Najijua

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,039
180
Wadau najaribu kutafakari hii slogan ya mzee Pinda ya kilimo Kwanza, kila siku gharama za chakula zinapanda kila siku zinapanda mfn:- Sukari imetoka 1600 - 2500/=Tshs, ,mchele toka 1000 - 1700/=Tshs maharage toka 800 - 1400/=Tshs, na bado wanatuambia Kilimo Kwanza nadhani mambo yalikuwa afadhali sana kabla ya hii falsafa

Tuamke tufanye jambo ilin serikali ijue kuwa maisha yanapanda kila siku na wanachi hatuwezi kuyamudu, sisi hatuna allowances kama wanazojilipa wao ambao zinafidia mishahara na mifumuko ya bei
 
Ni baba gani ambae mwanae akiomba samaki atampa nyoka, au akiomba mkate atampa nge? kama yupo hafai kuwa baba.
 
Kilimo kwanza 98% imetekelezwa jijini Dar es salaam.

Kijijini tunaita KILIO KWANZA
 
Mungi umenena, fikiria benki iliyopewa dirisha la fedha za kilimo ni TIB na ipo pale mlimani City, je wakulima wangapi wanaweza kufika pale?nenda kapate majina ya watu waliokopa fedha za kilimo ambazo nyingi hazijarudishwa wengi wao ni vigogo au washirika wa karibu wa vigogo au vigogo wastaafu wanaotumia ushawishi wao
 
Back
Top Bottom