Serikali itangaze rasmi balaa la njaa - ACTWazalendo

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
620
1,543
Serikali Itangaze Rasmi Balaa la Njaa kwa Mujibu wa Sheria

[Sehemu ya hotuba ya ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto, akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Nkome, Geita, Januari 6, 2017]

Wananchi wa Geita, juzi nilipokuwa kwenye ziara mkoani Morogoro nilizungumzia hali ya njaa nchini. Ninanukuu sehemu ya maelezo yangu kwa wananchi wa kata ya Kiwanja cha Ndege ambao nao wana uchaguzi mdogo Kama ninyi wa kata ya Nkome. Nilisema yafuatayo

"Hali ya chakula nchini sio nzuri. Wananchi mmeshuhudia namna bei za vyakula zinapanda kila siku. Bei ya sembe sasa kilo moja imefikia tshs 1600 hapa morogoro. Mchele kilo tshs 1500, maana yake Leo ugali na wali imekuwa bei inafanana. Gharama za maisha zitaendelea kupanda kutokana na uhaba wa chakula kuwa mkubwa.

Kwanini Hali ya chakula inazidi kuwa mbaya? Ni kwa sababu ya maamuzi mabovu ya Serikali kuhusu hifadhi ya chakula. Serikali zote zilizopita huko nyuma zilikuwa zinanunua chakula cha akiba ili wakati wa ukame kama sasa chakula hicho kiingie sokoni na hivyo kushusha bei na kuwezesha wananchi kumudu gharama za chakula. Rais wetu kawaambia wananchi wa Kagera kwamba Serikali haina shamba hivyo hakuna chakula cha njaa. Hii kauli sio ya uongozi. Ni kauli ya kuficha maamuzi ya serikali yaliyotupelekea kukosa akiba ya chakula.

Wananchi, Leo tunavyoongea ghala la chakula la Taifa lina tani 90,000 tu za chakula. Kipindi kama hiki mwaka 2015 ghala la chakula lilikuwa na tani 450,000. Chakula kilichopo kwenye ghala kinatosha kwa wiki moja tu. Takwimu hizi zote zipo kwenye Taarifa ya Benki Kuu ya Mapitio ya uchumi ya mwezi Novemba". Mwisho wa kunukuu.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba alijibu hoja hizi kwa wepesi kabisa na kusema kwamba Tanzania ina chakula cha kutosha. Alipoulizwa ataje kiasi kipo kwenye ghala la Taifa (NFRA), alijibu kwamba "kwa sababu za kiusalama hawezi kutaja". Hata hivyo takwimu za kiasi cha chakula zipo kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania na hivyo ni taarifa za wazi. Ni dhahiri Waziri wa Kilimo Alikuwa anajaribu kuficha kwa kuogopa kutumbuliwa kwa kusema Hali halisi ya chakula nchini.

Ninampongeza Sana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu Kassim Majaliwa kwa kuamua yeye Mwenyewe kutembelea NFRA na kujionea hali halisi. Huu Ndio uongozi badala ya kukanusha habari ambazo ni za kweli kabisa na kuthibitishwa na taasisi za Serikali Kama Benki Kuu ya Tanzania. Waziri Mkuu anapaswa kuchukua hatua dhidi ya viongozi wa Serikali wanaoficha ukweli kuhusu baa la njaa nchini.

Waziri wa Kilimo anasema kama wananchi wanaona ugali ni ghali wale wali. Anasema kuna mchele mwingi nchini lakini umeshikwa na watu binafsi. Waziri anataka kuwaambia watanzania kuwa hivi sasa Serikali inategemea chakula cha watu binafsi ambao haijui idadi ya tani zilizopo kushughulika na suala la njaa. Hii ni ajabu kubwa Sana.

Nchini Ufaransa alitokea mke wa mfalme mmoja. Wananchi walikuwa wanalalamika kuwa hakuna mikate. Malkia yule akiitwa Marie Antonnoite alimwambia mumewe, hawa watu wako Kama hawana mikate si wale keki? Hii ndio hali ya sasa nchini. Waziri anasema kama sembe imekuwa ghali, wananchi wale wali. Anasahau kuwa hata mchele umepanda bei. Maharage yamepanda bei na mafuta ya kupigia yamepanda bei.

Leo nimeona katika Mbunge wa jimbo la Mchinga, Ndugu Bobali akiitahadharisha Serikali kuhusu bei za chakula jimboni kwake. Nimepita kwenye maduka ya Singida leo na kuuliza bei za sembe na mchele nimeambiwa zimepanda Sana ndani ya miezi miwili iliyopita. Sembe sasa imefikia kilo tshs 1700 kwenye baadhi ya maeneo nchini. Hapa Geita naambiwa gunia la mahindi sasa ni shilingi 98,000 na Muhogo umepanda mpaka tshs 95,000 kwa gunia kutoka shilingi 70,000 mwaka Jana mwezi Kama huu.

Tunataka tumwone Waziri wa Kilimo akihangaika na suala hili linalowagusa wananchi wote hapa nchini. Hali ya chakula ni mbaya, ni mbaya, ni mbaya. Tunataka tumuone akishughulika kutatua hali hii.

Lakini Hali Hii imetokana na nini? Kwanza nilieleza kuwa Serikali ya awamu ya tano ilipunguza Bajeti ya pembejeo kutoka shilingi 78 bilioni katika bajeti ya mwaka 2015/16 mpaka shilingi 10 bilioni mwaka 2016/17. Serikali ilifanya Hivi ikijua kuwa mwaka huu kutakuwa na hali mbaya ya chakula kwani tayari dalili zilionekana mwaka uliopita ambapo uzalishaji wa mahindi ulipungua kwa 12%.

Pili Serikali haikutenga fedha za kununua chakula kuweka kwenye hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA). Hii imethibitishwa na ziara ya Waziri Mkuu kwenye maghala ya Taifa ambapo ghala Kuu la Songea lina tani 10,000 tu za chakula. Hii ilimfanya Waziri Mkuu kuagiza kuwa chakula hicho kisitolewe kwani kutokana na Uhaba wa mvua nchi itatapata balaa la njaa.

Tatu, mipango mibovu ya Serikali kwenye sekta ya kilimo. Mwezi Juni mwaka 2016, Serikali ilitoa Taarifa ya Hali ya Uchumi ambayo ilionyesha kuwa kiwango cha ukuaji wa sekta ya Kilimo nchini kimeporomoka mpaka 2.3%. Sababu zilizoelezwa na Taarifa hiyo ya Serikali ni pamoja na;
- kutokuwa na mvua za kutosha na za wakati
- Kuendelea kutegemea mvua ambayo haitabiriki.
- Ukosefu wa masoko ya uhakika
- Uhaba wa Viwanda vya kusindika mazao ya Kilimo

Wananchi, sababu hizi zilizoelezwa na Serikali zilipaswa kujibiwa kwenye Bajeti ya Serikali. Kilimo cha umwagiliaji ambacho tungetegemea kuwa tiba hakikujaliwa na kilitengewa fedha kiduchu sana kwenye Bajeti ya Serikali. Angalau tungeona juhudi hizi tungesema Serikali ipo makini kushughulika na suala la Kilimo nchini. Serikali ambayo iliingia kwa matumaini makubwa kwamba itafanya mambo tofauti imefanya vibaya zaidi kuliko Serikali iliyotangulia.

Hapa Geita ninyi ni mashahidi wa namna sekta ya Kilimo inavyoanguka kupitia zao la pamba. Pamba ni zao nyeti sana kwa sekta ya Viwanda kwa nchi yeyote ile duniani. Sekta ndogo ya nguo ni moja ya shughuli za uchumi ambazo dunia nzima inatambua Kama kichocheo cha maendeleo ya Viwanda na kuondoa umasikini. Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikiimba kuwa itajenga viwanda na tumeambiwa anakuja Waziri wa Mambo ya Nje wa China kwa ajili ya kuleta Viwanda 200 nchini Kati ya sasa na mwaka 2020.

Maswali muhimu ni viwanda gani hivyo? Kama ni Viwanda vya nguo mbona sekta ndogo ya Pamba inakufa? Mwaka 2014 uzalishaji wa Pamba ulishuka kwa 47% na mwaka 2015 ukashuka tena kwa 18%. Ninyi Geita mlikuwa walimaji wakubwa wa Pamba lakini leo hata Ginnery ya Pamba iliyokuwa pale Kasamwa imegeuka kuwa kituo cha polisi. Hakuna juhudi zozote za kuhamasisha Kilimo cha Pamba licha ya bei kuanza kuwa nzuri katika msimu uliopita. Nasikia mmeacha kulima pamba na mnalima zenu matikiti maji.

Baada ya ziara ya Waziri Mkuu kwenye maghala ya Taifa na kujionea Mwenyewe Hali ya chakula nchini ninapendekeza Serikali ichukue hatua muhimu ya kisheria ya kutangaza baa la njaa nchini. Tamko la baa la njaa litaisaidia Serikali kuweza kupata bajeti ya dharura ya kununua chakula na kutoa uhuru kwa Wakuu wa Wilaya kutangaza bila woga kuwa maeneo yao yana njaa. Bila kufanya hivi Serikali italeta maafa makubwa kwa sababu wakuu wengi wa wilaya na mikoa wataendelea kuficha hali halisi ya njaa nchini.

Watu wa Nkome mnayo nafasi ya kuishtua Serikali kutoka kwenye dimbwi la usingizi huu kwa kuinyima kura CCM. Mwenyezi mungu amewapa fursa ya kuiambia Serikali kwa sanduku la kura mnamo tarehe 22 January 2017. Kama mwananchi wa Nkome unachukizwa na njaa usiipigie kura CCM. Kama unachukizwa na maneno bila vitendo kwa Serikali ya CCM ya awamu ya Tano kwenye sekta ya Kilimo na Viwanda usiichague CCM.

WanaNkome nawaletea kwenu Mgombea wa Chama cha ACT Wazalendo mumchague kuwa diwani wa kata ya Nkome katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita. Tunawaahidi kushirikiana nanyi kutatua changamoto zetu za maji na afya. Nimeelezwa shida kubwa ya maji hapa katani kwenu licha ya kuwa jirani Kabisa na ziwa viktoria. Sisi Kama Chama na diwani wenu tutakuwa sauti yenu kutafuta majawabu ya changamoto zenu.

Ahsanteni kwa kunisikiliza

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Nkome - Geita
Januari 6, 2017
 
Na hiki chama nacho eti kinataka kushika dola. CCM naona itazeekea ikulu kwa mtindo huu. Kama kuna njaaa yeye hiyo nguvu ya kuongea kaitoa wapi.Ebu badala ya kuwambia wafuasi wake walime, sasa anatangaza njaaa. Inamaana kero ya watanzania kwa sasa ni njaa?? Naomba nijiwe na vyama vya upinzani
 
Acha kuongea mikojo wewe. Watu walime wakati wazao yamekauka shambani.
c50a4d6caee9fc9821494adc8e12eb05.jpg

Wanachama wa ccm wakati mwingine mnakuwa kama vichaa. Hata jambo muhimu mnapinga bila fikira.
 
Dying declaration pia kisheria iko admissible,nakuunga mkono zitto,japo act wazalendo inakufa,lakini maneno yako yanaweza kutumika mahakamani kuelezea the pending situation
 
Back
Top Bottom