Hivi ni alikuwa dikteta? Au sijui sifa za dikteta!! Mbona alitoa ushauri juu ya Tanzania ya baadae kuepuka dikteta?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Hakuna Rais aliyekuws anaogopwa Tanzania kama Mwl Nyerere.
Kama sifa ya udikteta ni kuogopwa basi Mwl. Nyerere alikuwa ni dikteta.

Kikubwa zaidi yeye aliamua hata kuondoa kwenye katiba kifungu kinachohusu haki za binadamu.

Yeye aliingia madarakani kwa njia ya vyama vingi lakini alipoapishwa akaamua kufuta vyama vingi lakini cha kushangaza zaidi, alipong'atuka kutokana na nchi kuelekea kufirisika, akaamua kuwalazimisha wengine waanzishe mfumo wa vyama vingi.

Ninakuhakikishia kama utawala wa Mwl. Nyerere ungekuwa ndio kwa sasa, hata hawa wanaosema Rais Mgufuli ni dikteta wasige thubutu hata kutamka maneno wanayotamka.

Huwa ninawashangaa sana watu wanajaribu kujenga hoja kuhusu haki za binadamu kwa kutumia kioo cha utawala,wa Mwl. Nyerete.

Kwa hiyo kama ni udikteta, basi tumwangalie Rais Magufuli kwa kutumia kioo cha matendo ya Mwl. Nyerere wakati akiwa Rais wa Tanzania.

Kwangu mimi sioni tofauti ya kuvunja katiba au kuibadilisha katiba na kuwa katika msingi wa udikteta.

Mwl. Nyerere alikuwa anaibadilisha katiba ili kuimarisha udikteta wake huku akidai ni kosa kuvunja katiba. Mwl. Nyerere hakuhitaji kuvunja katiba kwa sababu alikuwa na uwezo wa kuibadilishaapendavyo.

Kwa waliomuona mwalimu Nyerere, mwalimu Magufuli haijafika hata robo ya matendo ya madikteta, lakin mwalimu Nyerere alikuwa na sifa nyingi za madikteta wazuri
 
madikteta huwa waanaamini wanafanya mambo kwa manufaa ya nchi na huamini wanayafanya vizuri hivyo huwa hawataki kuingiliwa ndiyo sababu Nyerere kwa usomi wake alijua kuwa vyama vingi, demokrasia, na uhuru wa kujieeleza ni mambo mazuri kwa ustawi wa nchi. lakini power ili mcorrupt hakurusu hayo na kuja kuyaona hayo baada ya kutoka. akaishia kutuachia katiba inayoruhusu udikteta.
 
madikteta huwa waanaamini wanafanya mambo kwa manufaa ya nchi na huamini wanayafanya vizuri hivyo huwa hawataki kuingiliwa ndiyo sababu Nyerere kwa usomi wake alijua kuwa vyama vingi, demokrasia, na uhuru wa kujieeleza ni mambo mazuri kwa ustawi wa nchi. lakini power ili mcorrupt na kuja kuyaona hayo baada ya kutoka. akaishia kutuachia katiba inayoruhusu udikteta.
Mh
 
kila kitabu na zama zake kwa mazingira ya wakati ule ilikuwa sahihi kufuta vyama vingi ila kwa mazingira ya sasa ni vigumu huyo Nyerere unayemkashifu ndio ameweka misingi ambayo unaweza kukaa kwenye keyboard na kumkashifu
 
nchi nying za kiafrika baada ya kupata uhuru zilibadili mfumo kutoka kwenye vyama ving vya siasa hadi kimoja sababu ni:-
1.mfumo wa wakoloni ulikuwa wa chama kimoja hivyo haukufuata demokrasia na sisi tukaiga
2.uchochezi na shinikizo kutoka kwa mataifa ya ulaya na mashariki ya mbali
3.falsafa ya plato juu ya demokrasia
hivyo ndo vilipelekea hivyo, Mwl Nyerere hana kosa ila mwenye makosa ni huyo unaemfananisha na nyerere
 
Inawezekana ote wakawa madikteta ila mmoja kamzidi mwenzie
 
Maadam umekiri Mwalimu Nyerere alikuwa na sifa za madikiteta wazuri, hivyo hakuivunja katiba bali aliibadili, vivyo hivyo tumemshauri rais Magufuli, kama vipi afute katiba atawale kwa decrees

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria, ongoza kwa 'presidential decrees'!

Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

P
Kwahiyo ye Hana uwezo wa kubadilisha katiba Ila anaivunja??
 
..vyama pinzani kwa Tanu vilishindwa vibaya ktk uchaguzi.

..kwa maneno mengine kilikufa vyenyewe, wazungu wanaita " natural death. "

..mazingira hayo ndiyo yaliyopelekea Nyerere kuanzisha mfumo wa chama kimoja.

..kinachotokea sasa hivi ni "mtu fulani" kutumia MABAVU, UKATILI, HUJUMA, na DHULUMA, ili vyama mbadala na CCM vipotee au vife.
 
Hakuna Rais aliyekuws anaogopwa Tanzania kama Mwl Nyerere.
Kama sifa ya udikteta ni kuogopwa basi Mwl. Nyerere alikuwa ni dikteta.

Kikubwa zaidi yeye aliamua hata kuondoa kwenye katiba kifungu kinachohusu haki za binadamu.

Yeye aliingia madarakani kwa njia ya vyama vingi lakini alipoapishwa akaamua kufuta vyama vingi lakini cha kushangaza zaidi, alipong'atuka kutokana na nchi kuelekea kufirisika, akaamua kuwalazimisha wengine waanzishe mfumo wa vyama vingi.

Ninakuhakikishia kama utawala wa Mwl. Nyerere ungekuwa ndio kwa sasa, hata hawa wanaosema Rais Mgufuli ni dikteta wasige thubutu hata kutamka maneno wanayotamka.

Huwa ninawashangaa sana watu wanajaribu kujenga hoja kuhusu haki za binadamu kwa kutumia kioo cha utawala,wa Mwl. Nyerete.

Kwa hiyo kama ni udikteta, basi tumwangalie Rais Magufuli kwa kutumia kioo cha matendo ya Mwl. Nyerere wakati akiwa Rais wa Tanzania.

Kwangu mimi sioni tofauti ya kuvunja katiba au kuibadilisha katiba na kuwa katika msingi wa udikteta.

Mwl. Nyerere alikuwa anaibadilisha katiba ili kuimarisha udikteta wake huku akidai ni kosa kuvunja katiba. Mwl. Nyerere hakuhitaji kuvunja katiba kwa sababu alikuwa na uwezo wa kuibadilishaapendavyo.

Kwa waliomuona mwalimu Nyerere, mwalimu Magufuli haijafika hata robo ya matendo ya madikteta, lakin mwalimu Nyerere alikuwa na sifa nyingi za madikteta wazuri
wakati huo kwenye akili walikuwa wachache labda wale watani zake tu waliomtikisa, Sikh hi wrnye akili tuko wengi, huyu mchunga ngombe wa chato hawezi kutushawishi
 
Back
Top Bottom