Hivi ndoa ni kero kiasi hiki?

mbalisana

Member
Dec 15, 2011
46
42
Hivi inakuwaje binti ndo kwanza kamaliza chuo 26yrs,anaomba aolewe na mwanaume mwenye mke na watoto 2, kila siku anaahangaika kupiga simu mara nakupenda sana, nakumis sana,ukinioa namimi nitakuzalia watoto 2,huyo mkeo labda anatumia dawa lakini naamini unanipenda mimi zaidi kwakua tunatoka kijiji kimoja na ulikuwa na mimi kabla hujao.mimi ni mke wa huyo mwanaume, yawezekana bado wanaendelea wanapokutana, lakini najiuliza huyu binti hata kama ni upendo kweli yupo radhi kuharibu ndoa ya mtu mwingine hata kama kweli mume ndo anamfuatilia bado. Na huyu mwanaume kama bado alikuwa anampenda x-girlfriend kwa nini hakumuoa. nawashangaa sijui nianze nao vipi, maana nilimwambia mwanaume mawasiliano yao siyapendi naona ndo kwanza yanazidi.
 
Pole mwaya, Mungu akupe busara za kudeal na hiyo issue. Ongea na mumeo vizuri maana kama angekuwa anajitambua asingekuwa anainkareji hayo mawasiliano. Kuna mtu amesema adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie.......naanza kuamini taratibu.
 
pole sana dada ,umeshawahi kusikia kitu inaitwa obssession?....basi huyo binti atakuwa na kaugonjwa hako ,mwambie mumeo ajihadhari naye huyo anamatatizo ya akili.
hlf huyo mumeo naye inaonekana anamuentertain huyo binti ndo maana mazoea hayaishi.
 
Mbalisana ndio ujue kua a good man to marry are hard to find... Huyo binti kisha msoma mumeo kua ni good parent na hubby na atatumia njia yoyote ile ampate. Mwanamke mwenye guts za kutamka kwa mwanaume kua yule mwanamke hakufani muache na unioe mimi yupo desperate! (siwezi shangaa hata akienda kwa bibi kama ni mshirikina); Inabidi ugangamale na uhakikishe mumeo asije kua chambo (if you still love him) for ukileta ulege lege na kuishi kulalama then aweza fanikiwa azima yake...

Uzuri ni kwamba wajua (I am taking it for granted mumeo mwenyewe ndio kakwambia) for kama kweli angekua na nia ya kuendelea nae sidhani kama angesema kwako. Bali mambo yangefanywa kimya kimya... Na usishangae saana baana, wanaume walooa hua mara nyingi responsible saana katika mahusiano kuliko single guys, hivo hubby is bound kusumbuliwa once in a while na desperate wadadas... Ni aibu but ndio ukweli....
 
Ndoa ndoano mama...ukiona mwanamke mwenzio anatumia manjonjo kumpata mume ujue taratibu utampoteza huyo mume..uwe mbunifu na wewe kumfanya asizinguke na wenzio hacha kuamini tu kwa kuwa una ndoa basi nyote yamefungwa katika ndoa..Kila mwanaume upo wakati fulani lazima awaze kuwa na mwanamke mwingine na hii inatokana na:
(i) Mkewe kubweteka kwa mengi ikwemo kushindwa kutimiza wajibu wake kama mke;
(ii) Kushawishiwa na marafiki hasa akiwa nje ya nyumbani (ofisin, sehemu za starehe au safarini)
(iii) kuvutika na wale anaokutana nao kila wakati
(iv) kuboreka na vitendo vya Mkewe
(v) kukosa busara tu ya kuheshimu ndoa yake.
nk nk ...

Junior Member

Join Date : 15th December 2011


Posts : 1


 
Junior Member

Join Date : 15th December 2011


Posts : 1




Ngoshwe this was not neccessary jamani.... Kuna wengine hapa ni guests siku zooote na akipata tatizo ndio anjiunga. Wengine kweli ni member lakini anaona aibu. Sasa ukifanya hivi mkuu wamfanya akose raha (kwa wengine ambao ni sensitive)
 
hana upendo wowote kwa huyo mwanaume anamindi tu atm? hv unadhani sms zote wasichana wanaandika kwa wanaume especialy waume za watu ni kweli? kawekwa mjini lazima atumie njia zote ili apate huduma,kumbuka waume za watu wengi wana uwezo visharobaro navyo havilipi
chunga ndoa yako. mama.
 
umenikumbusha movie moja ya kighana inaitwa suicide mission itafute utajifunza kitu mle
zingatia maombi zaidi na mshirikishe mumeo ktk maombi
pia jinagalie ni kitu ghani humfanyii mumeo au mambo gani unafanya yanamuudhi
jiangalie usawa wa 6 kwa 6 kwani mkishaolewa mnajisahau kabisa na kumpa kifo cha mende
wkt nje huko anapewa kila mkao autakao.ulimi wako je una asali kwa mumeo? pole yataisha sema nae kuhusu ukimwi pia na future ya wanenu-
 
pole sana dada ,umeshawahi kusikia kitu inaitwa obssession?....basi huyo binti atakuwa na kaugonjwa hako ,mwambie mumeo ajihadhari naye huyo anamatatizo ya akili.
hlf huyo mumeo naye inaonekana anamuentertain huyo binti ndo maana mazoea hayaishi.

Kuna movie ame-act Beyonce inaitwa OBSESSION...ina kitu kinacho relate hiyo stori hapo juu moja kwa moja...#Ni nzuri sana..

Otherwise,huyo wa kijiji kimoja hakuwa chaguo lake kama mke au wife material ndo maana hakumuoa...wewe ndio mwenye mali,ila usiposimama kidete kumkatisha kuwasiliana na yule wa kijiji moja unaweza kunyang'anywa tonge mdomoni huku unaona endapo mwanaume atajiachia pande hizo...OKOA NDOA MAMAA.
 
haya ndo matatizo ya kutafuna vitumbua ovyo bila kuvichunguza mental stastus.hako kademu ni chizi na vinakuwaga visumbufu balaa...pole sana mama.kuna mtu kakuambia hapo juu a good man is hard to find.......fight for what is urs,ukizubaa unapoteza
 
Ngoshwe this was not neccessary jamani.... Kuna wengine hapa ni guests siku zooote na akipata tatizo ndio anjiunga. Wengine kweli ni member lakini anaona aibu. Sasa ukifanya hivi mkuu wamfanya akose raha (kwa wengine ambao ni sensitive)
[/LEFT]


kumbe siku moja moja zina charge eeh?? safiii
 
Jipange sawasawa,hapo unapigwa bao sasa hvi na nyumba ndogo. Anza kukemea mapema
 
Huyo mume anayaendekeza hayo! Sometimes nafikiri ni vema mke ukajitia uchizi wa muda kwa huyo mume, pengine utaeleweka!

Upole sana nao saa ingine si mzuri
 
Back
Top Bottom