Hivi ndiyo Visa vyangu vidogo vidogo vya mapenzi nilipoanza kupenda totoz shule ya msingi

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,733
Kitambo kidogo mwamba nikiwa darasa la saba najiita LY (last year ). Nilitokea kumzimia mtoto mmoja wa kipemba lakini mwamba kumwambia kuwa nampenda ndiyo ulikua mtihani mkubwa sana.

Kwa kuwa mwamba nilikua kipanga kwenye somo la hisabati, hii ndiyo ilikawa njia ya mtoto kuwa karibu na Mimi, Yule mtoto wa kipemba nilikua nae karibu lakini kumtongoza ikawa shida nikaishia kula kwa macho tu.

Nilipata wazo nikamfata broo mmoja wa kitaa nikampa story juu ya huyo mtoto, broo alinishauri niandike Barua nikampe, mwamba nikaona yess!! Huu ndiyo ushauri, nilitimba homu nikadraft mistari mizuri kwenye Barua niliyokua nimepewa na huyo bro wa kitaa.

Ile Barua niliweka mfuko wa kaptula, lakini kila nikikutana na huyo mchumba/mtoto wa kike nafsi inasita kumpa, mwamba nilizunguka na ile Barua wiki mbili bila kumpa aisee.

Siku moja tukiwa class, mwamba nilipata ujasiri wa hali ya juu, nilimfuata Yule mtoto wa kike nikamwambia njoo nje nikuambie maana kulikua hakuna mwalimu.
Basi alitoka nje kusikiliza wito, mwamba nikampa ile Barua halafu sikutaka mengi Wala nini, nilizama class nikamuacha nje anaisoma kimoyo moyo nikifurahi huyu mtoto wangu.

Baada ya nusu saa, nashangaa mwalimu mwalimu kaingia na kiboko huku kamshika mkono Yule mchumba, mwamba niliitwa mbele ya darasa kumbe ile Barua alipomaliza kuisoma Yule mtoto wa kipemba aliipeleka kwenye ofisi ya walimu.

Nilichezea stick za kutosha mbele ya darasa Kisha nilipewa Barua yangu niisome kwa sauti huku darasa zima likinisikiliza mzee baba.

Hiyo sitoisahau abadani.

...….…...….....…….......….…..........….......…......…...

Kisa kingine hiki ndiyo huwa najiona mjinga sana baada yakuulizwa swali na mtoto wakike na nilishindwa kujibu mpaka hivi Sasa nikikutana nae huwa ananizingua sana.

Ilikua hivi nikiwa form two, mwamba Kuna toto moja la kitanga nilikua nalikubali sana na yeye alikua anasoma kidato Cha pili.

Sikumoja nilijichanganya kwa mabroo wa kidato Cha nne wakaanza kunipa nondo namna gani jinsi yakumtongoza Yule mtoto.

Yule mtoto tulikua tunaishi jirani jirani alikua ameniziea lakini mwamba nilikua Domo zege nilikua Nina maneno mengi lakini kutongoza siwezi.

Wale mabroo waliponipa nondo za kutosha basi nikajipiga kifua nakuseama NALIA NGWENA naweza lazima huyu mtoto anikubalie.

Nilimvizia kwenye Kona moja alipokatiza tu nilimuita akaitikia wito bila hiyana

Mimi: Mambo vipi

Yeye: poa niambie

Mimi: Unajua Mimi nakupenda sana

Yeye: Unanipenda kivipi??

Alipouliza Hilo swali nilikosa majibu maananiliona nikisema nakupenda kimapenzi basi angeniona muhuni na ningesema ninampenda kiurafiki nilihisi ningekosa mbususu.

Mwamba nilijichekesha Kisha nilimjibu tutaongea kesho, mpaka hivi Sasa sikuwahi kumjibu kuwa nampenda kivipi kaolewa na anafamilia yake.

Na huwa tukikutana huwa anacheka sana na ananitania "unanipenda kivipi??

Huwa nacheka tu, maana mwamba sikutegemea swali Kama Hilo kutokana na mabroo walivyonipa nondo hicho kipengele hawajakiweka.

Juhudi zangu ziligonga mwamba nikaamua kuachana nae sikufuatilia Tena, na huwa nikikumbuka huwa nacheka sana.
 
.
20230412_210639.jpg
 
Duh Maisha ya primary ni ya kichoko Sana bora angalau secondary

Nilimtongoza dogo akalia na kuondoka kwenda kwao !!!

Wakati mimi mtoto wa mwalimu mather angejua siku iyo sijui hata ingekuwaje.

Sikulala siku iyo kwa mawazo
Toka hapo nikaacha mapenzi mpaka nilipomaliza f4!!!

All in all mapenzi na shule hasa primary na olevel haviendani ni kulazimisha tu!!
 
Duh Maisha ya primary ni ya kichoko Sana bora angalau secondary

Nilimtongoza dogo akalia na kuondoka kwenda kwao !!!

Wakati mimi mtoto wa mwalimu mather angejua siku iyo sijui hata ingekuwaje.

Sikulala siku iyo kwa mawazo
Toka hapo nikaacha mapenzi mpaka nilipomaliza f4!!!

All in all mapenzi na shule hasa primary na olevel haviendani ni kulazimisha tu!!
 
Duh Maisha ya primary ni ya kichoko Sana bora angalau secondary

Nilimtongoza dogo akalia na kuondoka kwenda kwao !!!

Wakati mimi mtoto wa mwalimu mather angejua siku iyo sijui hata ingekuwaje.

Sikulala siku iyo kwa mawazo
Toka hapo nikaacha mapenzi mpaka nilipomaliza f4!!!

All in all mapenzi na shule hasa primary na olevel haviendani ni kulazimisha tu!!
Kwamba mtoto alilia nakukuona wew muhuni
 
Back
Top Bottom