Hivi ndivyo wafugaji wengi wa kuku wanavyotapeliwa kwa kuuziwa vifaranga vya uzao wa pili au tatu

nadhani uko sahihi. Sema wengi wetu tumekariri. Kuku wa kienyeji pure anafaida sana ukimaanisha biashara kweli.
Pia kunanjia nyingi za kuminimise cost kwa kuku kienyeji kuliko hao kuroiler.
Zaid ya hapo nyama kuroiler hata kwa dawa haiwez fikia kwa kuku toka musoma.
Watu wanaangalia sana muda bila kujifunza ni kwa namna gani ya kuweza kuzalisha kwa wingi na kupunguza gharama ili upate faida zaidi.
Mfano mimi naweza nikanunua labda matetea 100 na majogoo 10. Nikitarget kwa muda miezi sita na kumaanisha biashara kweli na naweza jikuta nafikisha mtaji hata wa kuku 3000 wakafi wewe utakuwa baado unahangaika na chotara wako ila mim naweza kuwa nishauza vifaranga hata 2000kwa kuku hata1000 na nikaangiza milion mbili wakat weye umejibana ukanunua vifaranga 1000 kwa miezi yote pata faida ya kiwango changu
Unawajaza watu ujinga kiongozi
Kuku wa kienyeji wanakuwa taratibu sana
Hadi kufikisha hao kuku 3000 kwa kutumua hao kuku 100 utatumia muda mrefu sana
Wakati anayefuga kisasa keshauza kuku hata mara 10 zaidi ya hao ndani ya muda huo
Kuku wa kienyeji labda uwafugw nyumbani kwa ajili ya kula tu sio biashara, utasubiri sana
 
Safi sana
Leo ningependa kuzungumzia hii biashara ya kuku inayofanywa na baadhi ya wafugaji ambao mwisho wa siku wanazalisha vifaranga na kuwauzia wajasiliamali wengine.

Somo hili ni mahususi kwa wale wajasiriamali ambao wanakimbilia kununua vifaranga kwa watu hapa na walenga wale wanaofuga Kuroiler ama Sasso.

Kwa ufupi ni kwamba mmachezewa mchezo mchafu na baadhi ya wafugaji kwa kuwauzia vifaranga ambao ni kizazi cha pili ama tatu ambapo kuku hao perforamance yao iko chini mno tofouti na mnavyoaminishwa na hao wafugaji. Mbaya zaidi, wameenda mbali sana kuwauzia kwa gharama ya juu zaidi ambapo kihalali inakuwa si sawa.

Labda nigusie kidogo hapa, hawa kuku wazazi wa either Layers, Broiler ama Kuroiler/Sasso ni gharama sana kuwaingiza hapa nchini na pia uleaji wake unahitaji umakini mkubwa sana tofouti na hawa kuku wetu wa kawaida. Kwa makadrio tu kifaranga kimoja cha parent stock mpaka kuingia nchini kitakugharimu kati ya USD 15~20 hivyo ni ngumu kwa mtu wa kawaida kumudu gharama yake, hivyo kupelekea makampuni makubwa kama Silverlands, Interchicks na Mkuza Chicks kuwa na kuku hao.

Baada ya kulelewa vyema kuku hao wazazi hutaga mayai na kupelekwa hatchery ambapo mayai ya broiler yatoa vifaranga vya kuku wa nyama ambavyo mtauziwa kwa lengo la kutoa nyama tu, mayai ya kuku wa mayai yatatoa kuku wa mayai kwa ajili ya mayai tu na mayai ya kuroiler/sasso vifaranga ambao watatumika kama kuku wa nyama au kwa ajili ya mayai pekee.

Sasa baadhi ya wafugaji hutumia mwanya huu kuwakuza hao kuku chotara na kupata mayai yao ambapo huyapeleka hatchery kutotoleshwa na kupata kizazi cha pili (2nd generation) na wao pia kuwauzia wafugaji wengine. Labda niwaambie tu hapa ndiyo huwa munaibiwa maana performance ya kuku hao itakuwa chini sana kwa maana kwamba kuanzia utagaji, ukuaji utakuwa chini na pia kuku hawa hawatokaukiwa na magonjwa maana kinga yao ya mwili iko chini mno.

Mwisho, kwa wafugaji ambao wangependa kuingia katika industry hii ningependa kuwataadharisha muache mara moja kununua vifaranga kwa wafugaji wa nyumbani maana mnatapeliwa mchana kweupe kwa kununua kuku ambao hawatokupa matokeo mazuri.

Kwa maana hiyo ningependa mnunue kuku hao katika makampuni makubwa ambayo yana kuku wazazi (parent stock) mtapata matokeo mazuri tofouti na hao wa mtaani.

Maelezo yote nimefupisha katika mchoro hapo chini.

Kama kuna sehemu hujaelewa na utahitaji maelezo zaidi weka swali lako hapo nami nitakujibu.

b9b6d0f75338469ab0a593aa7e10b621.jpg
 
ok kuna hoja Mh
1. kuna wakala anae sambaza vifaranga kutoka compun ya Silverlands wa saso miongoni mwao nimeona wamelemaa katika 100 unaweza kuona 20 hawakui kama maelezo uliyo eleza na wakala anasema nikawaida.
2. hayo makampuni kama kweli yana hitaji kulinda soko kwanin hawaja fanya mpango kazi kwaajili ya hii changamoto?
3.ufugaji wa kuku wakisasa unagarama kubwa saana kwa vijijini hilo ukipinga utakosea maana A hao vifaranga sisi huku tunapata kwa awamu 2-4 kwa mwaka
B. bei ya vyakula maalum ni changamoto + dawa na madini mbalimbali ,kwa hoja hii naomba ushauri
 
Ahsante kwa swali zuri. Iko hivi hayo makumpuni makubwa wao huwa ndio wenye parent stock na hawawezi kukuuzia na ilitokea wanakuuzia basi huwa ni kwa kukuuzia kama nyama na si vinginevyo wanafanya hivyo kwa sababu ya kwamba ukipata huyo jogoo wa parent stock na ukienda kuwachanganya na kuku wako basi kuku wako watakuwa na uwezo mkubwa wa uzalishaji hivyo wanaliepuka hilo kwa sana maana wataua biashara yao.

Hivyo hao parent stock wakizeeka majogoo yote huchinjwa na hapo hufuatiwa na matetea ya parent stock baada ya siku 7~10 maana kwa siku hizo mayai yote ambayo ni fertilized yanakuwa hayapo tena.

Swali la pili, Makampuni tajwa hapo juu hayana second generarion bali wana 1st generation ambao ndio wanawauzia nyie ili nyie mkapate nyama au mayai pakee na sio kupata mayai na kuyapeleka hatchery kwa ajili ya utotoleshaji hivyo kuishia kupata second generation ambayo kwa performance inakuwa iko chini mno...

Kwa mfano. vifaranga wa 1st generation wa kuroiler na sasso wanaweza kukupa mayai 250 kwa mwaka lakni hao wa second generation wataishia kukupa mayai kati ya 80 mpaka 100 ambapo iko chini mno...

Na kwa upande wa nyama 1st generation anaweza kukupa kilo 1.8~ 2.2 za nyama kwa siku 56 tu wakati 2nd generation wanuwezo wa kukupa kilo 0.5~0.7 za nyama kwa siku tajwa hapo juu...

Siri kubwa ya kuku hawa ni kuwa kadli kizazi kinavyoshuka zaidi ndivyo performance iko chini mno...

Mkuu asante kwa shule hii.Ubarikiwe sana
 
YANI HAPA NAPIGA TIKI YOTE ULIYOANDIKA NDO NILIAMBIWA!!

KUKU WA KIENYEJI MPK AFIKE MAHALI PA KUUZWA KWA 25,000 SI CHINI YA MIAKA MIWILI!
NA HATAZIDI KILO 2

KUKUNWA KIENYEJI ANALALIA KWA ASILI!
HATA UKIMTOTOLESHEA MAYAI, MWILI WAKE UNACHUKUA MUDA TENA KUANZA KUTAGA TENA!!
Mmmh, haya mambo bana. Kila mtu na uzoefu wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa somo zuri sana. Nina swali moja. Nikichukua hao chotara F1 kutoka kwa makampuni uliyotaja, alafu nikawakuza. Wakiwa wakubwa nikatenga jogoo mzuri kuliko wote nikamweka kwa kuku wangu wa kienyeji pure. Then hao chotara nikawauza wote. Abaki huyo jogoo awashughulikie tetea wangu wa kienyeji, si nitakuwa nimefanikiwa kuboresha kuku wangu wa kienyeji? Maana lengo langu nataka kuku wa kienyeji ila ambao watakuwa na miili mizuri
Cross breeding kama hiyo mara nyingi hupelekea kupatikana kuku fulani wa ajabu sana. Yaani hafikii ubora wa kuku chotara na hana pia vigezo vya kienyeji. Kuwauza hawa ni shughuli. Pia hukua kwa taabu sana. Uzoefu wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unawajaza watu ujinga kiongozi
Kuku wa kienyeji wanakuwa taratibu sana
Hadi kufikisha hao kuku 3000 kwa kutumua hao kuku 100 utatumia muda mrefu sana
Wakati anayefuga kisasa keshauza kuku hata mara 10 zaidi ya hao ndani ya muda huo
Kuku wa kienyeji labda uwafugw nyumbani kwa ajili ya kula tu sio biashara, utasubiri sana
Muda mrefu kiasi gani? Dadavua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasso ni "both purpose " yaani ni kwaajili ya nyama na mayai.

Iko hivi : Sasso wa old day hadi 28th day wanakula starter. Baada ya hapo mfugaji ndo anaamua amfanye awe wa nyama pekee au wa mayai.

Akitaka kumfanya awe wa nyama,atatakiwa kumpa chakula cha broiler (si lazima cha dukani,unaweza kuchanganya ).Baada ya mwezi na nusu (yaani kutoka alipofikisha 28days ). Jumla ni miezi miwili na nusu unawezakumuuza.Anakua ameshafikisha 1.8 -2.5 kg.

Na ukitaka kumfanya atage mayai huna budi kumpa chakula cha layers,baada ya miezi minne ataanza kutaga.

Nb: maelezo haya nimepatiwa na ma -officer wa SILVERLAND nilipohudhuria 2019 POULTRY SHOW iliyofanyika sabasaba Dar
Duh! Hao hao Silverland hutoa elimu kuwa sasso asitumike kwa ajili ya mayai kwani ni hasara. Ni special breed kwa ajili ya nyama. Silverlands wanao kuku special wa mayai, siyo sasso.

Kuhusu chakula iko hivi. Kifaranga wa mayai apaswa kula Layer's starter na yule wa nyama apewe broiler starter. Ila kwa kuwa broiler starter "huwakimbiza" vifaranga, wabunifu huwapa vifaranga wa mayai broiler starter kwa wiki 2 au 3 tu na kisha kuendelea na layer feeds.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nawezaje kupata jogoo la kisasa( first generation) ambalo linaweza kumate na kuku tetea wa kawaida nitotoleshe katika incubator na mimi nile vichwa huku kijijini kwangu.

Sent from my Nokia 6.1 Plus using Tapatalk
 
YANI HAPA NAPIGA TIKI YOTE ULIYOANDIKA NDO NILIAMBIWA!!

KUKU WA KIENYEJI MPK AFIKE MAHALI PA KUUZWA KWA 25,000 SI CHINI YA MIAKA MIWILI!
NA HATAZIDI KILO 2

KUKUNWA KIENYEJI ANALALIA KWA ASILI!
HATA UKIMTOTOLESHEA MAYAI, MWILI WAKE UNACHUKUA MUDA TENA KUANZA KUTAGA TENA!!
Hapana Mm nina Kuroiler wana Wiki 17 na wana kilo zaidi ya 2...
Hii kitu ya kufuga inahitaji umakini,na ufuatiliaji wa hali ya juuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo ningependa kuzungumzia hii biashara ya kuku inayofanywa na baadhi ya wafugaji ambao mwisho wa siku wanazalisha vifaranga na kuwauzia wajasiliamali wengine.

Somo hili ni mahususi kwa wale wajasiriamali ambao wanakimbilia kununua vifaranga kwa watu hapa na walenga wale wanaofuga Kuroiler ama Sasso.

Kwa ufupi ni kwamba mmachezewa mchezo mchafu na baadhi ya wafugaji kwa kuwauzia vifaranga ambao ni kizazi cha pili ama tatu ambapo kuku hao perforamance yao iko chini mno tofouti na mnavyoaminishwa na hao wafugaji. Mbaya zaidi, wameenda mbali sana kuwauzia kwa gharama ya juu zaidi ambapo kihalali inakuwa si sawa.

Labda nigusie kidogo hapa, hawa kuku wazazi wa either Layers, Broiler ama Kuroiler/Sasso ni gharama sana kuwaingiza hapa nchini na pia uleaji wake unahitaji umakini mkubwa sana tofouti na hawa kuku wetu wa kawaida. Kwa makadrio tu kifaranga kimoja cha parent stock mpaka kuingia nchini kitakugharimu kati ya USD 15~20 hivyo ni ngumu kwa mtu wa kawaida kumudu gharama yake, hivyo kupelekea makampuni makubwa kama Silverlands, Interchicks na Mkuza Chicks kuwa na kuku hao.

Baada ya kulelewa vyema kuku hao wazazi hutaga mayai na kupelekwa hatchery ambapo mayai ya broiler yatoa vifaranga vya kuku wa nyama ambavyo mtauziwa kwa lengo la kutoa nyama tu, mayai ya kuku wa mayai yatatoa kuku wa mayai kwa ajili ya mayai tu na mayai ya kuroiler/sasso vifaranga ambao watatumika kama kuku wa nyama au kwa ajili ya mayai pekee.

Sasa baadhi ya wafugaji hutumia mwanya huu kuwakuza hao kuku chotara na kupata mayai yao ambapo huyapeleka hatchery kutotoleshwa na kupata kizazi cha pili (2nd generation) na wao pia kuwauzia wafugaji wengine. Labda niwaambie tu hapa ndiyo huwa munaibiwa maana performance ya kuku hao itakuwa chini sana kwa maana kwamba kuanzia utagaji, ukuaji utakuwa chini na pia kuku hawa hawatokaukiwa na magonjwa maana kinga yao ya mwili iko chini mno.

Mwisho, kwa wafugaji ambao wangependa kuingia katika industry hii ningependa kuwataadharisha muache mara moja kununua vifaranga kwa wafugaji wa nyumbani maana mnatapeliwa mchana kweupe kwa kununua kuku ambao hawatokupa matokeo mazuri.

Kwa maana hiyo ningependa mnunue kuku hao katika makampuni makubwa ambayo yana kuku wazazi (parent stock) mtapata matokeo mazuri tofouti na hao wa mtaani.

Maelezo yote nimefupisha katika mchoro hapo chini.

Kama kuna sehemu hujaelewa na utahitaji maelezo zaidi weka swali lako hapo nami nitakujibu.

b9b6d0f75338469ab0a593aa7e10b621.jpg
kaka ushwah kuwaskia mr. kudu farmers? ndo hao
 
Ahsante kwa swali zuri. Iko hivi hayo makumpuni makubwa wao huwa ndio wenye parent stock na hawawezi kukuuzia na ilitokea wanakuuzia basi huwa ni kwa kukuuzia kama nyama na si vinginevyo wanafanya hivyo kwa sababu ya kwamba ukipata huyo jogoo wa parent stock na ukienda kuwachanganya na kuku wako basi kuku wako watakuwa na uwezo mkubwa wa uzalishaji hivyo wanaliepuka hilo kwa sana maana wataua biashara yao.

Hivyo hao parent stock wakizeeka majogoo yote huchinjwa na hapo hufuatiwa na matetea ya parent stock baada ya siku 7~10 maana kwa siku hizo mayai yote ambayo ni fertilized yanakuwa hayapo tena.

Swali la pili, Makampuni tajwa hapo juu hayana second generarion bali wana 1st generation ambao ndio wanawauzia nyie ili nyie mkapate nyama au mayai pakee na sio kupata mayai na kuyapeleka hatchery kwa ajili ya utotoleshaji hivyo kuishia kupata second generation ambayo kwa performance inakuwa iko chini mno.

Kwa mfano. vifaranga wa 1st generation wa kuroiler na sasso wanaweza kukupa mayai 250 kwa mwaka lakni hao wa second generation wataishia kukupa mayai kati ya 80 mpaka 100 ambapo iko chini mno.

Na kwa upande wa nyama 1st generation anaweza kukupa kilo 1.8~ 2.2 za nyama kwa siku 56 tu wakati 2nd generation wanuwezo wa kukupa kilo 0.5~0.7 za nyama kwa siku tajwa hapo juu.

Siri kubwa ya kuku hawa ni kuwa kadli kizazi kinavyoshuka zaidi ndivyo performance iko chini mno.
asante mkuu
 
Back
Top Bottom