Hivi ndivyo wafugaji wengi wa kuku wanavyotapeliwa kwa kuuziwa vifaranga vya uzao wa pili au tatu

Umesema ukweli na asante sana kwa somo zuri.
Jambo la muhimu sana si kuweka ukomo wa mawazo kwamba lazima mfugaji anunue Kuroiler kutoka kwa AKM Glitters.

Msisitizo unatakiwa uwe kama unataka kufuga kuku wa Kuroiler unatakiwa ujiridhishe kama msambazaji/mfugaji anayekuuzia vifaranga wa Kuroiler ana cheti cha ithibati kutoka Kegg Farm India ambao ndio wazalishaji na wasambazaji wa Kuroiler wazazi duniani.

Pia wafugaji wanaotaka kuuza vifaranga wa Kuroiler inatakiwa wapate mafunzo kutoka Kegg Farm, wafanyiwe majaribio ya ubora kisha wapate cheti cha ithibati ya kusambaza vifaranga ambao ni F1.

Tuache kuibia watu na kiwadhulumu kwa kuwauzia vifaranga ambao sio uzao wa kwanza.

Ukihitaji kujua zaidi nicheki 0768678122.
 
Halafu guys Hivi TANBRO na KUROILER wakikuwa wakubwa wanafanana uzito au Kuna ambaye Huwa anakuawaida ya kuwa na uzitio mkubwa kuliko mwengine ? (Assuming wote wamelishwa vizuri)
 
Ukiongelea silverland unaongelea ipi? Waliopo mikoa yote? Au wa dar pekeake?

Kimfano wapo silverland pale nzuguni dodoma nao wanazalisha vifaranga ila unakuta kuku wengine ni wazuri wazito na wanapendeza, wengine kama wakienyeji wepessii na wengine vishingo na wengine ni vifupi vinene, kwa ufupi ktk kuku 100 unakuta ndani yake kuna makundi 3-4 tofauti.

Au ndo kawaida tu kupata mchanganyiko?
 
OS Cordis
silverland wanauza broiler?na kama sio silverland naweza nunua wapi ili kupata matokeo bora zaidi?
kati ya broiler na kuloirer(kwa mayai) kama mtaalam unamshauri mtu afanye option ipi?

unawaongeleaje sasso?mkuu pm....
Nasikia sasso wanakula sanackwa kuku 1000 wanaweza kula kg 130 kwa mwez kuroiler anakula kg 75 kwa mwez na mayai kuroiler wanataga vizur kuliko sasso ila sasso wako vizur kweny nyama sasso anaweza kufikia kg 1.5 ndan ya miez 3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo ningependa kuzungumzia hii biashara ya kuku inayofanywa na baadhi ya wafugaji ambao mwisho wa siku wanazalisha vifaranga na kuwauzia wajasiliamali wengine.

Somo hili ni mahususi kwa wale wajasiriamali ambao wanakimbilia kununua vifaranga kwa watu hapa na walenga wale wanaofuga Kuroiler ama Sasso.

Kwa ufupi ni kwamba mmachezewa mchezo mchafu na baadhi ya wafugaji kwa kuwauzia vifaranga ambao ni kizazi cha pili ama tatu ambapo kuku hao perforamance yao iko chini mno tofouti na mnavyoaminishwa na hao wafugaji. Mbaya zaidi, wameenda mbali sana kuwauzia kwa gharama ya juu zaidi ambapo kihalali inakuwa si sawa.

Labda nigusie kidogo hapa, hawa kuku wazazi wa either Layers, Broiler ama Kuroiler/Sasso ni gharama sana kuwaingiza hapa nchini na pia uleaji wake unahitaji umakini mkubwa sana tofouti na hawa kuku wetu wa kawaida. Kwa makadrio tu kifaranga kimoja cha parent stock mpaka kuingia nchini kitakugharimu kati ya USD 15~20 hivyo ni ngumu kwa mtu wa kawaida kumudu gharama yake, hivyo kupelekea makampuni makubwa kama Silverlands, Interchicks na Mkuza Chicks kuwa na kuku hao.

Baada ya kulelewa vyema kuku hao wazazi hutaga mayai na kupelekwa hatchery ambapo mayai ya broiler yatoa vifaranga vya kuku wa nyama ambavyo mtauziwa kwa lengo la kutoa nyama tu, mayai ya kuku wa mayai yatatoa kuku wa mayai kwa ajili ya mayai tu na mayai ya kuroiler/sasso vifaranga ambao watatumika kama kuku wa nyama au kwa ajili ya mayai pekee.

Sasa baadhi ya wafugaji hutumia mwanya huu kuwakuza hao kuku chotara na kupata mayai yao ambapo huyapeleka hatchery kutotoleshwa na kupata kizazi cha pili (2nd generation) na wao pia kuwauzia wafugaji wengine. Labda niwaambie tu hapa ndiyo huwa munaibiwa maana performance ya kuku hao itakuwa chini sana kwa maana kwamba kuanzia utagaji, ukuaji utakuwa chini na pia kuku hawa hawatokaukiwa na magonjwa maana kinga yao ya mwili iko chini mno.

Mwisho, kwa wafugaji ambao wangependa kuingia katika industry hii ningependa kuwataadharisha muache mara moja kununua vifaranga kwa wafugaji wa nyumbani maana mnatapeliwa mchana kweupe kwa kununua kuku ambao hawatokupa matokeo mazuri.

Kwa maana hiyo ningependa mnunue kuku hao katika makampuni makubwa ambayo yana kuku wazazi (parent stock) mtapata matokeo mazuri tofouti na hao wa mtaani.

Maelezo yote nimefupisha katika mchoro hapo chini.

Kama kuna sehemu hujaelewa na utahitaji maelezo zaidi weka swali lako hapo nami nitakujibu.

b9b6d0f75338469ab0a593aa7e10b621.jpg
Wewe umetumwa kwa niaba ya makampuni makubwa ili kuwahujumu wazalishaji wadogo. Mfugaji usiyumbishwe.
 
aksante kwa kutusambazia maarifa-tronics
 
Ahsante kwa swali zuri. Iko hivi hayo makumpuni makubwa wao huwa ndio wenye parent stock na hawawezi kukuuzia na ilitokea wanakuuzia basi huwa ni kwa kukuuzia kama nyama na si vinginevyo wanafanya hivyo kwa sababu ya kwamba ukipata huyo jogoo wa parent stock na ukienda kuwachanganya na kuku wako basi kuku wako watakuwa na uwezo mkubwa wa uzalishaji hivyo wanaliepuka hilo kwa sana maana wataua biashara yao.

Hivyo hao parent stock wakizeeka majogoo yote huchinjwa na hapo hufuatiwa na matetea ya parent stock baada ya siku 7~10 maana kwa siku hizo mayai yote ambayo ni fertilized yanakuwa hayapo tena.

Swali la pili, Makampuni tajwa hapo juu hayana second generarion bali wana 1st generation ambao ndio wanawauzia nyie ili nyie mkapate nyama au mayai pakee na sio kupata mayai na kuyapeleka hatchery kwa ajili ya utotoleshaji hivyo kuishia kupata second generation ambayo kwa performance inakuwa iko chini mno.

Kwa mfano. vifaranga wa 1st generation wa kuroiler na sasso wanaweza kukupa mayai 250 kwa mwaka lakni hao wa second generation wataishia kukupa mayai kati ya 80 mpaka 100 ambapo iko chini mno.

Na kwa upande wa nyama 1st generation anaweza kukupa kilo 1.8~ 2.2 za nyama kwa siku 56 tu wakati 2nd generation wanuwezo wa kukupa kilo 0.5~0.7 za nyama kwa siku tajwa hapo juu.

Siri kubwa ya kuku hawa ni kuwa kadli kizazi kinavyoshuka zaidi ndivyo performance iko chini mno.
 
YANI HAPA NAPIGA TIKI YOTE ULIYOANDIKA NDO NILIAMBIWA!!

KUKU WA KIENYEJI MPK AFIKE MAHALI PA KUUZWA KWA 25,000 SI CHINI YA MIAKA MIWILI!
NA HATAZIDI KILO 2

KUKUNWA KIENYEJI ANALALIA KWA ASILI
HATA UKIMTOTOLESHEA MAYAI, MWILI WAKE UNACHUKUA MUDA TENA KUANZA KUTAGA TENA!!
kuna Kuku wapo Tunduma sogea karbu na shule ni wakienjeji pure kbs wanafika had 5Kg ila bei yake ni 35000+
 
Back
Top Bottom