Hivi ndivyo wafugaji wengi wa kuku wanavyotapeliwa kwa kuuziwa vifaranga vya uzao wa pili au tatu

Asante kwa ushauri ,mimi nahitaji kuku chotara iyo first generation je hayo makampuni makubwa wanauza vifaranga vya mwezi mmoja au wanauza vya siku tuu.?
Kuna ambao wanapatikana wa mwezi mmoja na wale wa day old chick...

Ni wewe unaangalia ni wapi wenye unafuu kwako, ila kama lengo lako ni kufuga kuku wa mayai ni vyema ukasubili wa mwezi mmoja ili kuepuka kuuziwa majogoo mengi au kama lengo lako ni kupata nyama ni vyema si mbaya ukachukua day one old chick maana proportion ya jogoo huwa juu zaidi ya matetea...

Pia, kws day one old chick ukipata mtaalamu mzuri anaweza akawatofoutisha...

Ahsante...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante,mimi ndo naanza kufuga nataka kwa ajili ya mayai ,nilikuwa nataka nianze na wa mwezi mmoja ili nipate uzoefu,sasa hao mwezi wanapatika au mpaka niweke oda nisubiri miezi kadhaa maana nataka nianze ufugaji mwezi huu
Kuna ambao wanapatikana wa mwezi mmoja na wale wa day old chick...

Ni wewe unaangalia ni wapi wenye unafuu kwako, ila kama lengo lako ni kufuga kuku wa mayai ni vyema ukasubili wa mwezi mmoja ili kuepuka kuuziwa majogoo mengi au kama lengo lako ni kupata nyama ni vyema si mbaya ukachukua day one old chick maana proportion ya jogoo huwa juu zaidi ya matetea...

Pia, kws day one old chick ukipata mtaalamu mzuri anaweza akawatofoutisha...

Ahsante...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana ujui ni kiasi gani umenisadia yani apa nilikuwa najiandaa kutafuta vifaranga kwa watu,sasa uyo Dr kessy awezi kunichakachua.na hao AKM Glitters wanapatikana wapi.?
Usinunue kwa watu, bora hiyo hela tukalewe Bia wanapatikana opposite to mlimani city, ile njia inayoingia sinza kivulini house namba 64...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki ulichoandika hapa nimekithibitisha SUA!!

Nilienda tu kujifunza kuhusu kuku!
MIONGONI MWA NILIYOSIKIA NI HILI ULILOANDIKA HAPA!!

exact the same!!
Mpk nikakumbuka hii thread!!
Sasa wao SUA wanatusaidiaje kutoibiwa? Maana kama wanaishia kueleza matatizo na wasitupe ufumbuzi, ni bora kubadili chuo kiwe hatchery. Labda wewe uliyefika kwao unifumbue macho, SUA wanauza vifaranga?
 
Acha kupotosha watu. Yaani hapo kwenye kuchambua f1 na f2
F1, ni uzao ilio toka kwa kizazi olijino ambayo ndio parents stork, na kizazi hiki kitakua na uwezo kama ilivyo parent stork.

Na f2 ndio hivi hawa wa mtaani. Unakuta kuku f1 wanacross na hawa wetu wa kiswahili unakuta ndio wanatoa chotara aliye changanyika kwa baba na mama so wengi waliopo mtaani ni f3.

Sasa ukisema kua parents stck ikizeeka wanachinja je uko wanakochukua parents stock inatoka wap. Parents stock inatoka kwa kizazi ambacho ni F1 wakiona hawa wanakaribia kuzeeka wanaanda kizazi kipya. Ikiwa kama wanachinjaa tuu ata huko wanakotoka wote wangechinjwa na kizazi kingeisha.

Sent using Jamii Forums mobile app

Umedhihirisha Hauna uelewa wa kutosha juu ya Uzalishaji wa kuku kibiashara ulivyo ikiwa hujui hata kuku wazazi (Parent stock) wanatoka wapi. ingekua ni Busara kusema “Mkuu tunaomba utuelezee zaidi, wengine hatuelewi vizuri haya mambo” na sio kusema mtoa mada anapotosha, kwa jibu rahisi ni kwamba wewe ndio unapotosha!!

Nirudi kwenye hoja yako ya kutaka kujua Kuku wazazi wanatoka wapi,
Ipo hivi!
Uzalishaji wa kuku kibiashara ni Mradi we thamani kubwa na Uzalishaji wenyewe upo Kibiashara zaidi
Mtiririko wa Uzalishaji ni upo katika mfumo wa kiukoo na Ukoo huishia kwa watoto (F1).

Ni watoto pekee ndio hutumika kwa matumizi ya Nyama(Broilers) au Mayai(Layers) kibiashara, maana ndio kusudio lao na Sio kwa uzazi sababu sio kuaudio lao.

Kabla ya kupata Watoto (F1) kuna Wazazi (Parent stock) waliozaliwa na Grand Parent stock (Mababu) waliozaliwa na Grand Grand PS (Mababu kwa mababu).

Ukiwa na GGPS unazalisha GPS tu,
Ukiwa na GPS unazaliaha PS tu
Ukiwa na PS unazalisha F1 (Production line) ambao wanauwezo mkubwa kukua haraka na Kutaga mayai mengi.

Yaliyobaki yamesemwa na mtoa uzi (rejea mada kuu)
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom