- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Madai
Kumekuwapo na picha inayosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo X, ikimuonesha Rais wa Kenya William Ruto akiwa amepungua mwili ikiambatana na ujumbe;
"Tunashindwa kuelewa Kasongo amepatwa na shida gani. Huyu siye Ruto tunayemjua. Wakenya mmefanya nini Kasongo"
Uhalisia wa picha hiyo ni upi?
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa picha hiyo imeharirirwa kwa kutumia nyenzo za kidigitali.
Picha hiyo imeharirirwa kutoka katika picha halisi ya Rais Ruto iliyochapishwa mtandaoni Machi 22, 2026 alipohudhuria Kasipul kwa ajili ya ibada kwenye shule y Agoro Sare Senior.
Vyanzo mbalimbali vilichapisha taarifa hiyo ikiambatana na picha hiyo ikiwemo Kenyans.co.ke ambapo Pichani anaonekana akiwa amepokelewa na Gladys Wanga ambaye ni Gavana wa jimbo la Hoba Bay.