Hivi ndivyo nilivyotapeliwa hapa JF kijinga

Hivi ndivyo nilivyotapeliwa hapa JF kijinga

Siku ya Jana kuna mdau hapa Jf Jina limenitoka kidogo alikuja na uzi wa kuuza bandle nafuu zijulikanazo kama supa bando.

Number yake ya simu ya mkononi ni 0620 434 183. SIMON MSUYA.

Dili lilikua nipewe GB 10 kwa Tshs6,000. Nikaona kwani 6k kitu gani ngoja nitume tu,.

Jamaa kanitumia link nidownload hiyo app ya super bando kwa maelezo nitumie opera mini ndio itafanya kazi.

Baba nimedownload kutumia power engines zote, sijui opra mini, Mozila fire fox, internet explorer, Chrome na zingine zote unazojua lakini app haikufanya kazi.

namrudia ananiambia nisubiri masaa manne nikajua nimeshaliwa.

Guys when the deal is tooo good think twice!!!!

Japo nilikua najaribu ila mwishowe nimejiona bwege
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]GB 10 kwa elf 6... Yeye anazitioa wapi? Kitonga hugharimu sana kama ukienda bila tahadhari
 
Cku zote pesa ya dhulma/wizi haimfikishi mtu popote, hata kama ameiba, amedhulumu mabilioni ya pesa kazi bure tu.
Mimi naona inategemea tu na siyo kwa wote waliodhulumu. Wengine baada ya kudhulumu hivyo uendelea kupeta na baadae sana ufariki kwa kifo cha kawaida tu kama wengine wasiodhulumu.
 
Mimi naona inategemea tu na siyo kwa wote waliodhulumu. Wengine baada ya kudhulumu hivyo uendelea kupeta na baadae sana ufariki kwa kifo cha kawaida tu kama wengine wasiodhulumu.
Pesa ya kudhulumu lazima ikutokee puani tuu, yaweza kuchukua hata miaka 50, lakn at the end lazma iblow up, solution ni kutubu na ikiwezekana rudisha Kwa mwenye nayo...
 
Nilijipanga kuwapa pole na kuwafuta machozi watakaolizwa.
 
Ndio maana matangazo yao hayaishi kumbe mabwege mpo kama ulivyojiita wewe mwenyewe,uwe makini
Sasa kuliko kukejeli bora mtoe angalizo kwa mods kwamba hilo tangazo kama bado lipo lifutwe na huyo member tapeli apigwe life ban.
 
Back
Top Bottom