Hivi ndivyo Jenerali Qasem Soleimani alivyouawa na Marekani

Status
Not open for further replies.
Mkuu rudi post number 149 upate ukweli namna Kamanda alivyouawa. Kamanda hakuwa kwenye fighting mode alikiwa pale kwa lengo la amani. Angekuwa pale kwa battle ningekubali kuwa ..hao jamaa wakali.

ukisikia mahaba niue ndio kama hivi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
wanasema ndege zisizo na rubani ndo zilifanya mashambulizi, sasa hizo sauti zinazosikia kwenye hiyo clip ni za nani?.
Iseje kuwa ni video game tu!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Lazima wawepo watu wa black operations special forces wa Kimarekani, kukusanya finger prints DNA blood group kuhakikisha person of interest kweli amekufa au la mara baada ya shambulizi kutokea na kama bado hajakata roho wanammaliza kwa risasi za kichwani.

Kisha watu hao wa Special Operations wanatambaa taratibu kwenda ktk safe house kufanya analysis ya sampuli walizo kusanya na kupelekea ujumbe makao makuu ya Special Operation Marekani kuwa mission accomplished na kuwa person of interest amemalizwa.

Hawa jamaa wa special operation hawataki tena kusikia kuwa mara ohoo jamaa ali survive, akatoweka kuibuka sehemu nyingine na kuicheka America.

Lazima mission iwe 100% accomplished na wao special operation forces ndiyo ndiyo macho na masikio ya drone ktk dakika ya mwisho kabla drone haijafyatua vitu vya maangamizi na baada ya kuwawasha magaidi . Hawa special forces wana supplement infrared heat seeking gears za drone kuhakikisha hata wakimbiao kwa miguu wote wanamalizwa.

Kongole kwa Special Operation forces kuwepo eneo kabla jamaa hajatua mpaka akatoka nje ya uwanja akiongozana na genge lake la walinzi waovu na kutoa order kitu kivyatuliwe kisha Special Operations soldiers wa Marekani wakasepa mdogo mdogo ktk giza na kutokomea.

Kwa kifupi hii drone pia inaweza kuwa ndiyo modern sniper (mlenga shabaha wa kisasa), huku askari wengine wa black Operations special forces wakiwepo na snipers wao ardhini kumaliza mchezo huu wa Paka na Panya.

God Bless America !

 
Ukweli umejulikana US waoga balaa...Kwa kifupi kwa uoga wao US waliwalazimisha Saud Arabia wajifanye wanataka suluhu na Iran na wakawaambia watumie Iraq kama mpatanishi , sasa kwa kuwa huyo mkuu wa Iraq bila kujua akaona ni jambo jema akawashirkisha Iran ilani wakamtuma general Solueiman (R.I.P) kwenda kusikiliza ni suluhu ya namna gani wanataka Saud Arabia! Kumbe ulikuwa mtego wa US... wakamvizia ametoka nje ya uwanja wa ndege wakamrushia kombora Kamanda na kumuua. Kamanda hakuwa kwenye fighting mode, kumbuka! Kwa staili hii tutaachaje kusema hao jamaa wa 'kombola la lremoti' siyo waoga!?

Haya maneno sijatunga ni habari kamili kutoka Asia ya magharibi kwa kaimu waziri Mkuu wa Iraq.Soma mwenyewe hapa chini.
We jamaa vip, Us iwe muoga?? Uwe muoga ukamuue mkuu wa majeshi wa adui yako tena karbu na nchi yake , thousands miles away Kutoka kwako?? Kwa taarifa yako huyo Mkuu wa majeshi ndo wa pili Kwa ukubwa Irani baada ya Raisi, huyo jamaa ndo alikuwa roho ya nchi ya Irani...
Hzo zingine ni mbinu tu za kumpata target Kwa urahisi na kumpiga , alaf inajulikana popote duniani Mkuu wa majeshi akipigwa na nchi imepigwa , ni heri afe Raisi na sio mkuu wa majeshi .....

Hata kama kutakuwa na actual combat , game field itakuwa kwenye nchi ya Iran , Kwa sasa Iran ipo pinned down pande zote , waliopo upande wa Marekani ni Weng na wenye nguvu kuliko waliopo upande wa Iran ambao ni wazee wa kubwabwaja Tu bila vitendo akina Kim , Putin na xing.....

Moja ya magenius waliowahi kutokea katika millitary warfare kwenye ulimwengu huu ni Mjapan aliyeitwa Isoroku Yamamoto alisema , "Unaweza kupambana na Us Kwa miez sita au mwaka Mmoja , lakn Zaid ya hapo lazima upigwe ", rate ya uzalishaji ya armament ya Us ni kubwa Zaid , viwanda vyote vilivyopo Marekani vimetengemezwa katika mazingira ya kwamba ikitokea vita vyote ndani ya sekunde vinageuka kuzalisha vifaa vinavyoendana na mahitaji ya kivita ...... Yaani hata wakipoteza askar 100k Leo kesho wanakuja wengine 100k wenye uwezo Sawa na waliotoweka Jana ...
Yamamoto ndo alikuwa roho ya Japan kwenye WW2 , wamarekani walifanya kitu kimoja tuu nacho ni kumtungua jamaa, tena walimuulia kwenye eneo lililokuwa linamilikiwa na Japan , Yamamoto alipokufa Japan iliyumba vibaya kwenye millitary planning na ikachezea kichapo heavy all around the Pacific....jamaa huwa wanatafuta mtu mhimu kwenye jeshi na wakishamchapa huyo mambo kwisha
 
Ulipizi wao siyo ule unaodhania, hawa wanakamata wanachinja, kesho unarushwa live kwa ndugu zako.
Hapa sawa sio vita ila ni visasi kupitia kwa mtu mmoja mmoja....
Mkuu rudi post number 149 upate ukweli namna Kamanda alivyouawa. Kamanda hakuwa kwenye fighting mode alikiwa pale kwa lengo la amani. Angekuwa pale kwa battle ningekubali kuwa ..hao jamaa wakali.
Kamanda anayejielewa anakuwa on high alert 24/7 hata kama an.atia
 
Ukiangalia picha utagundua ni tech ya juu sana inetumika.

Hakuna majanga pembeni mwaa gari alilotumia.

Mwili wa Qassem umeonakana kukatwa katwa vipande .

Pia inaonekana missile ilikua guided.


Watalaam wa haya mambo, marekani ametumia aina gani ya missile kuchakata mwili wa suleiman?

Watalaam wanasema sio hellfire missile ambazo hutumika kuhaeibu vifaru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa footage iyo...jeshi la USA ni noma sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Teknolojia ni raha sijui sisi tutafikia lini huko!!!!! Ni Usiku ndege isiyo na rubani inashambulia anayeiongoza yupo kwenye chumba ana place buttons tu then ukimaliza mission unarudi ku land na kupaki majini kwenye warship carrier. Kweli mabeberu wana uwezo...Ila cha ajabu Sana wanamuonea wivu rais wetu na nchi yetu kwa maendeleo tunayopiga ya viwanda tumekuwa threat kubwa kwenye uchumi wao. " Sisi ni donor country sio tuvae nguo za mitumba inatakiwa tuvae sisi halafu badae tuwape wao, jamani niwaambie tunawezaaaa" in...voice
 
Gari limechakatwa kama mboga iliyo katwa katwa. Ukiangalia pembeni haku a hata shimo .
IMG-20200107-WA0004.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iran bado hawajawa fit kuzipiga na USA, wanakwenda kutesa watu wao tu na migogoro isiyo na maana..Watu wa mashariki ya kati kitakachoweza kuwaokoa ni wao kuwa wamoja kupitia Arab legue yao.. Wasomeshe vijana wao, wajifunze teknolojia, watengeneze silaha zao, wajipe muda wa kujipanga.. Tofauti na hapo watakuwa kila siku wanasumbua raia wao.

USA mpaka sasa kwa maguvu aliyonayo vita inayoweza kumgharimu na kumtia hasara labda apigane na Mrusi au Mchina..hawa wengine kiukweli wanampa nafasi ya kutest teknolojia zake tu kila leo..
 
Vita ya sasa kama huna teknolojia yako mwenyewe kaa kimya tu vinginevyo utaumia. Huwezi kupigana vita kwa namna yeyote na mtu ambaye uchawi hajanunua namaanisha teknolojia ni yake na kila siku anaresearch na kutest vitu vipya.
 
USA anasilaha kulingana na kila stage ya vita, sasa usiombee kabisa afike ile stage three aka akose uvumilivu ndio utakutana na ile mwanaukome ya Hiroshima na Nagasaki iliyomfanya Japan mpaka leo atulie tu na utengenezaji wa magari aachane na vita..

Wanaofahamu kilichotokea baada ya Red Army la Mjepu kupiga pale Pearly Harbour na counter attack ya USA kule Japan wataelewa kwanini USA sio wakuchezanae kama hauko sawa kwenye teknolojia..

Iran wajifunze kwa Waarabu wenzao IRAQ, LIBYA nk juu ya hii michezo na USA.. Mashariki ya kati yote USA anabase kila mahala kuanzia SAUDIA, KUWAIT, BAKHRAIN, IRAQ, QATAR... hapo kifupi IRAN kashazungukwa na atakuwa amepark basi tu na mwenzie anashambulia muda wote na akishatia pua ndani ya IRAN utasikia kuna kikundi cha kigaidi ndani ya IRAN kinachinja watu tayari anadestabilize mambo ndani IRAN anaondoka anawaachia mazombie then anarudi tena baadaye kuwa mwokozi wenu mnampigia makofi... WAARABU WATAFUTE NAMNA NYINGINE YA KUDEAL NA USA HII YA VITA WAMESHASHINDWA JAMAA KILA SIKU ATAWAACHA MASIKINI TU..
 
Iran haiwezi kwenda na Marekani vita vya moja kwa moja. ila inachoweza ni mashambulizi ya kigaidi eneo la ghuba ambayo yatawagawa wanasiasa wa Marekani na kushinikiza kurudi kwenye mazungumzo kama yale ya Obama. Irani ni nchi ya 13 duniani kwa nguvu za kijeshi..
 
Iran haiwezi kwenda na Marekani vita vya moja kwa moja. ila inachoweza ni mashambulizi ya kigaidi eneo la ghuba ambayo yatawagawa wanasiasa wa Marekani na kushinikiza kurudi kwenye mazungumzo kama yale ya Obama. Irani ni nchi ya 13 duniani kwa nguvu za kijeshi..
Israel ni ya ngap?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom