Hivi ndivyo Freeman Mbowe na genge lake anavyotafuna pesa za CHADEMA!

Binafsi cjaona wapi wamemtaja mbowe. Na mnaosema mbowe kakopesha chama je yeye pekee Ndiyo mwenye uwezo kukopesha chama zaidi ya wengine? Ripoti haijamtaja jina mtu yeyote hivyo msitunge tuu kwa hisia. Pia mkopo haujaonesha riba yake kinachooneshwa ni malipo ya kodi ya mabango n.k. Mashirika ya Umma,Taasisi na Idara za Serikali Siyo Imprest zote zinakuwa retired Kwa hyo Hata Kwa Chadema Pia wanamapungufu hayo. Ijulikane kuwa Matumizi ya CCm kwa mwaka 14/15 ni makubwa na ya ajabu ILa mtoa post ameshindwa kulete full snap shot inayoendelea Inayobainisha Uovu Wa Ccm.
 
UBADHIRIFU NI UBADHIRIFU TU HATA UFANYWE NA MCHUNGAJI UNABAKI KUWA HIVYO. KUTETEA UBADHIRIFU WA AINA YEYOTE ILE NI UNAFIKI AMBAO HAUSAMEHEKI HATA KWA MUNGU. TUACHE USHABIKI WA KIPUUZI KWANI NCHI HII NI YETU WOTE NA HIZO PESA NI KODI YETU. HIVYO YEYOTE ANAYETUMIA PESA HIZO KINYUME NA UTARATIBU NI UFISADI
Wizi upo CCM nenda kawambie waache wizi
 
Mbowe anaikopesha CDM 2 billion, tena kwa riba kali hapa lazima kuna mgongano wa ki maslahi. Huyu “Kim Jong Un” wa CDM akipewa nchi atafilisi kila kitu.
Ila wakati akina mkapa na baba riz wanapiga nchi ilifilisika? Kasome na wewe upige, hata ingekua mimi nikipata fursa ya kupiga napigaaa mpaka nchi ifilisike ibaki magofu tuu, mbowe anatumia fursa kama tabia halisi ya sisi waafrica.
 
Mbona hujaonyesha ccm walivyopiga pesa za nchi yetu. Unahangaika na hela tu za chadema, ambazo wao ndio wanajua zimetumikaje baada ya kukopwa?
Hivi mtu na akili yako timamu unajiuliza wapi ccm wameiba?
Kila mkulu akisimama mahali lazima aseme uozo mahali flani ambao umefanywa ama na viongozi waliopita ama waliopo, au magu nae ni cdm hamumuamini?
 
Wale wa buku 7 wamepata sehemu ya kupumulia! Mizoga yote ya Lumumba yote imo humu. Huwezi waona kwenye zile nyuzi nyingine. Kama kweli ufisadi unawauma njooni mchangie na hizi nyuzi nyingine basi
CCM wengi ni wajinga wajinga kwani hata ambao wapo kwenye mitandao ni watumishi wa Le mutuz , Jerry muro na Cyprian msiba ni wajinga wote maana huwezi kuandika mawazo ya hao watu yakawa ya maana, kwa kifupi CCM hawataki Ruzuku yao iguswe kwani ikiguswa wengi watapata kesi.
 
Sijaona hela zilipotafunwa, zaidi ya kanuni kutokuzingatiwa wakati fedha zinakopwa. Ni kweli CHADEMA ina wenyewe na watu hao ni wana CHADEMA.
Kwa kuongeza hivi sasa ni marufuku,kuisema serikali vibaya kutokana na utendaji wake,serikali maana yake CCM,maana hats Mwenyekiti wa tawi ananguvu kuliko waziri .

Sent from my TECNO DP10A using JamiiForums mobile app
 
Sijaiona ripoti ya CAG nijuze imezungumuzia chochote kuhusu mapato na matumizi ya viwanja vya mpira ambavyo ccm walijimilikisha na sasa ni miradi ya watu huku vikiwa vyenyewe vinakuwa mapori?
 
Mimi nimeleta ya CHADEMA, hayo ya CCM ni kazi yako kuyaleta.

Kwa hiyo kama mahesabu ya CCM ni mabovu ndiyo inahalalisha pia mahesabu ya CHADEMA kuwa mabovu.

Huu ujinga umejifunzia wapi?
CCM inayowajali wanyonge imepiga pesa za wazee wastaafu kwenye vibubu vyao vya mifuko ya jamii! hata huruma hawana!
 
Sasa ulitaka atoe pesa yake mfukoni bure? Kuba ubaya kukikopesha chama?
 
Hebu kabla ya kusema hivi ungeleta na hesabu za CCM kujua bora iko wapi
Hilo ndio tatizo lenu,mkibanwa hasua mnasingizia ccm
Haya ccm wezi,kwa hiyo na nyie ruksa wezi sio kwa sababu ccm wezi?Ndio maana ccm itatawala mpaka itake yenyewe kuondoka kwa upuuzi kama huu
 
Mkaguzi Mkuu wa serikali(CAG) ameanika wazi jinsi ambavyo mabilioni ya pesa za CHADEMA yanatafunwa bila huruma na wajanja wachache huku chama kikiendelea kuwa na ofisi Kuu katika kibanda kwenye mtaa wa Ufipa Kinondoni wakati huo huo Mbowe akidai chama hakina pesa za kuwalipa watumishi mikoani na wilayani.

Haya yamebainishwa katika repoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha 2016/2017.

Hii inazidi kudhihirisha kuwa CHADEMA ina wenyewe kwa sababu hakuna kiongozi au mwanachama atakayethubutu kuhoji sana sana watajitokeza wapambe wake kumtetea kwa kutumia hoja za nguvu badala ya nguvu za hoja.

Kwa mtaji huu wa kujichotea pesa bila kuulizwa au kuwajibishwa, Mbowe hawezi kuachia nafasi ya Uenyekiti wa Chama Taifa!

Kinachoshangaza zaidi ni kuwa CCM ya sasa katika ukaguzi huu haina ufisadi kama wa CHADEMA pamoja na kwamba ni chama kikubwa na chenye pesa nyingi na miradi mingi.

Kwa maelezo zaidi nimekuwekea hapa chini sehemu ya uozo ndani ya CHADEMA uliobainishwa na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya serikali 2016/17.

View attachment 741889
View attachment 741896
View attachment 741901
Inzi wa kizungu
FB_IMG_1504379126733.jpg
 
Back
Top Bottom