Hivi namba za vocha za simu za kuongezea salio zinatengenezwa na programme gani?

NI SAWA NA KUBETI TU....NAWASHANGAA SANA HAWA MADOGO WANAOWEKA MIKEKA KILA SIKU INAUNGUA TUU
 
-Vocha creator is a special customized software that generate random keys using range defined by your services provider, kaka so sio rahisi kupata hiyo software-ila ukiwa mjanja wa kupata "range" na "fomula" wanayotumia kuzalisha hizo key, utaweza kuunda vocha creator ya kwako ikawa inaweza lutoa namba inayofuata badala ya vocha uliyonunua but sio busara kufanya hivyo coz hutotia hasara company pekee bali hata wauza vocha wa mikononi coz watakua wanarajeshewa vocha na kuambiwa zimetumika-
Kuna mda unaweza nunua vocha kuiweka unaambiwa imetumika.hii inakuaje
 
Kila mtu na topic yake

mara proba, sequence n series, comb an permutation.

basi mm nasema ni set ile

ila pale kwenye kubahatisha ni pure PROBABILITY

mpangilio ni comb and permu
 
Swali hili liliwahi kuulizwa na Michael Ngusa Dec 2014 na nilimjibu kwa kirefu na kitaalam kama ifuatavyo:

Hesabu lake liko hivi:

Kuna digits 10 tu yaani 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9

Namba za siri kwenye vocha zipo 14

Ukianza kubahatisha, uwezekano wa bahatisho la kwanza kuwa sahihi (kwa mfano kama namber sahihi ni 4) ni:
1/10

uwezekano wa bahatisho la pili kuwa sahihi (yaani number ya kwanza ambayo ni 4 na ya pili tuseme ni 7 (yaani 47) ) ni:
1/100

uwezekano wa bahatisho la tatu kuwa sahihi (yaani number ya kwanza ambayo ni 4 na ya pili ambayo ni 7 na ya tatu tuseme ni 9 (yaani 479) ) ni:
1/1000

tukiendelea hadi number zote 14 zipatikane kwa usahihi itakuwa hivi kwa kifupi:

bahatisho (event) na uwezekano (probability)


la kwanza 1/10
la pili 1/100
la tatu 1/1000
la nne 1/10000
la tano 1/100000
la sita 1/1000000
la saba 1/10000000
la nane 1/100000000
la tisa 1/1000000000
la kumi 1/10000000000
la kumi na moja 1/100000000000
la kumi na mbili 1/1000000000000
la kumi na tatu 1/10000000000000
la kumi na nne 1/100000000000000

Uwezekano wa mabahatisho yote 14 kuwa sahihi ni:

1/10 x 1/100 x 1/1000 x 1/10000.................................x 1/10^14

ambapo jibu lake ni 1x10^105 au 1/10^14! (! siyo alama ya mshangao bali ni alama ya kihesabu (factorial) kama vile 5!=5x4x3x2x1)

hivyo basi uwekano wa kupata numba zote 14 zikiwa sahihi ni:

0.0000000000000000000000000000000000000000000000..............endelea mpaka zifike sifuri 105! (! hapa ni alama ya mshangao)

AMBAYO KWA MANENO YA KITAKWIMU NDIYO KUSEMA TU NI VIGUMU MNO (ALMOST NO CHANCE)!!!

HITIMISHO: UWEZEKANO WA KUBAHATISHA VOCHA NI MDOGO MNO!.

USHAURI: NENDA KANUNUE KWA WAUZAO KAMA UNA FEDHA.
Probability kuwa ndogo sana haimaanishi uwezekano wa kubahatisha haupo.au haimaanishi unatakiwa ufanye majaribio mara nyingi sana. hata kama probability ni 1/100000000000 jaribio la kwanza tu unaweza kupatia
 
Haka kamchezo nilishawahi kukawazaga lkn dah.. hawa jamaa wanachezaga sana hii ngoma iwe ngumu kumesa
 
Mi nadhani za Tanesco ni ngumu kwani pia zinahusisha mita number.
Lakini sijui kwanini za simu inakua ngumu ku guess.
 
wengi mnashindwa kuelewa. Kubahatisha namba za vocha ni kazi moja. unaweza kubahatisha namba ukapatia, lakini bado kuna kuactivate hizo namba. hili hufanywa na service provider mwenyewe.
 
Back
Top Bottom