Hivi namba za vocha za simu za kuongezea salio zinatengenezwa na programme gani?

Hesabu lake liko hivi:

Kuna digits 10 tu yaani 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9

Namba za siri kwenye vocha zipo 14

Ukianza kubahatisha, uwezekano wa bahatisho la kwanza kuwa sahihi (kwa mfano kama namber sahihi ni 4) ni:
1/9

uwezekano wa bahatisho la pili kuwa sahihi (yaani number ya kwanza ambayo ni 4 na ya pili tuseme ni 7 (yaani 47) ) ni:
1/100

uwezekano wa bahatisho la tatu kuwa sahihi (yaani number ya kwanza ambayo ni 4 na ya pili ambayo ni 7 na ya tatu tuseme ni 9 (yaani 479) ) ni:
1/1000

tukiendelea hadi number zote 14 zipatikane kwa usahihi itakuwa hivi kwa kifupi:

bahatisho (event) na uwezekano (probability)


la kwanza 1/10
la pili 1/100
la tatu 1/1000
la nne 1/10000
la tano 1/100000
la sita 1/1000000
la saba 1/10000000
la nane 1/100000000
la tisa 1/1000000000
la kumi 1/10000000000
la kumi na moja 1/100000000000
la kumi na mbili 1/1000000000000
la kumi na tatu 1/10000000000000
la kumi na nne 1/100000000000000

Uwezekano wa mabahatisho yote 14 kuwa sahihi ni:

1/10 x 1/100 x 1/1000 x 1/10000.................................x 1/10^14

ambapo jibu lake ni 1x10^105 au 1/10^14! (! siyo alama ya mshangao bali ni alama ya kihesabu (factorial) kama vile 5!=5x4x3x2x1)

hivyo basi uwekano wa kupata numba zote 14 zikiwa sahihi ni:

0.0000000000000000000000000000000000000000000000..............endelea mpaka zifike sifuri 105! (! hapa ni alama ya mshangao)

AMBAYO KWA MANENO YA KITAKWIMU NDIYO KUSEMA TU HAIWEZEKANI (NO CHANCE)!!!

HITIMISHO: HUWEZI KUBAHATISHA NAMBA YA VOCHA.

USHAURI: NENDA KANUNUE KWA WAUZAO KAMA UNA FEDHA.

Na je vipi kubahatisha luku ya hawa tanesco??? Nayo uwezekano upoje?
 
Hahaaaa, kufulia kubaya mno kwani unakuwa na mawazo ya ajabu, mie nakumbuka kuna kipindi nilipigika hadi nikatoa nguo zote kwa kabati na kuanza kuzipiga sachi lakini wapi sikuambulia hata mia.

hahaha mbinu hii hadi leo ninaitumia nikiwa nimefulia. juzi nilijipiga sachi kumbe kuna elfu24 niliisahaugi ikaniokoa!
 
Hivi umetumia vocha za simu mara ngapi? huwezi hesabu. Na zile ni namba tu kati ya 0-9, kwanini huwezi otea/bahatisha kuandika na ikawa vocha? kuna waliojaribu wakafanikiwa? mbinu gani zinatumika?

Asanteni.
Kuna mtu m1 alikuwa shabiki wa kutuma salamu redioni, alikuwa akijiita mtaalamu wa kuingiza vocha bila kukwangua. Mtafute atakusaidia
 
Hivi umetumia vocha za simu mara ngapi? huwezi hesabu. Na zile ni namba tu kati ya 0-9, kwanini huwezi otea/bahatisha kuandika na ikawa vocha? kuna waliojaribu wakafanikiwa? mbinu gani zinatumika?

Asanteni.

Matumizi ya Check Digit yanasaidia sana kuzilinda hizo namba
 
Wakuu, hivi ni akili gani imetumika kutengeneza hizi namba za vocha kiasi hata ufanyaje hauwezi kupatia kuingiza namba hizi kwa kubuni na ukapata salio,ni nini kimefanyika?

Wajuvi mtujuze mkijuacho,nimeamua kuwaza tu kwa sauti...
 
Kuna mtu aliniambia kuwa itakulazimu urudie mara zaidi ya 1500 ili angalau uingize vocha moja.
Kwa hiyo kazi ni bora ukafanye kibarua uingize pesa ununue vocha.
 
Inawezekana ila muda probability ya kupatia ni ndogo sana bora ukanunua tu maana utakesha
 
Back
Top Bottom