Hivi nadharia sahihi ya maisha ni ipi?

Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,328
2,000
Habari za leo Great thinker!

Bila kupoteza muda niingie moja kwa moja keenye mada

Kwanza kabisa je! Ni kweli kuwa Mungu yupo? Kama ndio je! Mungu aliwaumba wanadamu huku akiwa amewapa matabaka kuwa huyu ataishi maisha ya dhiki maisha yake yote na huyu ataishi maisha ya raha na furaha maisha yake yote? Au huyu ataishi maisha ya huzuni

Na au tuseme kuwa maisha anayoishi mwanadamu fulani hapa duniani ndivyo ambavyo he\she destinied to live?? So anapaswa kukubali hali au maisha ambayo mungu kampangia kuishi hapa duniani?

Kwa mfano mtoto anazaliwa na mama kichaa anakulia jalalani na anafia jalalani,mtoto anazaliwa na wazazi wakulima maskin wa kutupwa anakulia shamba na anakufa akiwa mtu mzima kwa njaa,mtoto anazaliwa taahira na anakufa akiwa mzee taahira pia,anazaliwa kipofu na anakufa kwa kugongwa na gari na mifano mingine kama hiyo

Halafu upande wa pili anazaliwa tajiri na anakufa akiwa tajiri,anazaliwa maisha ya kawaida yakiyojaa furaha na anakufa maisha ya kitajiri yaliyojaa furaha na mifano inayoendana na hiyo

Swali,je! Kwanini mungu anawaweka wanadamu wenye thamani sawa katika hali tofauti maadam hawa wateseke na hawa waishi maisha ya raha mustarehe wakati anajua kuwa kila mwanadamu anapenda maisha mazuri na ya raha?

Kwanini wengine tutiwe ulemavu au udhaifu fulani ambao unatufanya tuishi maisha yasiyo na furaha? Au tuseme tumelaaniwa tu na tunatakiwa tukubali hali hiyo kwa maana ndio destiny yetu hapa duniani?

Kwanini wale wanaomuomba sana mungu hubaki palepale huku wale waliomsahau kabisa wakiwa na maisha ya furaha na raha mustarehe?

Sasa nadharia halisi ya maisha ni ipi? Kusema kuwa wenginr tumetiwa madhaifu kwa maana tumelaaniwa kwa sababu mungu ametaka tu tuwe hivyo? Mbona tunamlilia kila leo? Au ndo tukubalu tu kuwa haya ndo majaaliwa yetu?

MI HATA SIELEWI KWAKWELI!
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,150
2,000
Ayubu 21:22 Je! Mtu awaye yote atamfundisha Mungu maarifa?Naye ndiye awahukumuye walioko juu.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,150
2,000
Warumi : Mlango 11

33 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
7,374
2,000
Nina imani hata wewe Unajua kuwa ukiachilia magonjwa/ kilema, mengine yote yanaweza kubadilika.
Si lazima ukizaliwa katika hali duni basi kuishi katika hali hiyo hiyo mpaka mauti, na si lazima ukizaliwa katika hali bora tutaishi katika hali hiyo mpaka mauti.
Tumeumbwa na akili, utashi na dhamira ambazo tukizitumia vizuri, vibaya au kutokuzitumia kabisa, ndio itakapotupa mustakabali wa maisha yetu. Tumejaaliwa werevu wa kuyatawala mazingira yoyote yale tunayojikuta tumo. Je tunatumia aje vipawa hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi lakini je! Ina maana gani pale tuzaliwapo wakamilifu kisha tukatiwa madhaifu ambayo yanapelekea kupata upinzani mkali katika kuyatawala haya maisha yetu?

Inakuwa vipi mungu anatupa vyote hivyo ulivyovitaja lakini udhaufu anaotupatia katika kupindi fulani cha maisha yetu ukasababisha tupoteze karibu kila kitu alichotupa?
 
Ungetoa mfano. Ila maisha ni kujipanga. Changamoto za maisha zipo na zinatofautiana jinsi zinavyomkabili mtu binafsi, na pia zinatofautiana jinsi zinavyochukuliwa na zinazomkabili.
Wakati mtu mwingine akikabiliwa na changamoto zinammaliza kabisa, mwingine changamoto zinamjenga na kumuimarisha. Hivyo bado ni werevu, ujasiri, akili na utashi wa mtu binafsi ndio vitamuangamiza au kumuokoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,328
2,000
Ungetoa mfano. Ila maisha ni kujipanga. Changamoto zacmaisha zipo na zinatofautiana jinsi zinavyomkabili mtu binafsi, na pia kinatofautisha jinsi zinavyochukuliwa na zinazomkabili.
Wakati mtu mwingine akikabiliwa na changamoto zinammaliza kabisa, mwingine changamoto zinamjenga na kuliimarisha. Hivyo bado ni we revu, ujasiri, akili na tutaishi wa mtu binafsi ndio vitamuangamiza au kumuokoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu fikiria hii!

Unazaliwa kijana mwenye afya njema!

Unafika darasa la pili unapata ukiziwi so unakua kiziwi!(ina maana gani mungu kulifanya hili kwa mwanadamu?)

So hali hiyo ya kuwa kiziwi
-inakufanya upoteze marafiki
-inakufanya uwe mpweke bila marafiki
-upendo toka kwa ndugu unakwisha na unaonekana mzigo
-unasoma kwa shida
-unakonda kea mawazo ya kupuuzwa na marafiki nduguwalimu na hata walimu wa dini
-unakulia maisha ya kubaguliwa shuleni na hata kitaa so unaishi maisha ya kutokua na rafiki wa kudumu
-unamaliza masomo ya chuo unakua mwalimu mhitimu
-ni kiziwi huna uwezo wa kuchagua kazi badala yake kazi ndizo znakuchagua wewe so huna uwezo/uhuru wa kusema ujichanganye na vijana wenzio kupambana kitaa(unashindwa kumudu kazi nyingi zilizipo kitaa hali yako inakulazimu utafute kile ueezacho kumudu)
-employer wanashiw ubaguzi kutoa shavu coz uko deaf
-relatives wanakuona mzigo tu nothing you can do!
-your family ipo na hard life na wewe ndo kidume mkubwa your situation (deaf) inahinder wewe kutoa mchango wako uko jobless na things ni very tight

Hapa ndo unajiuliza why God kakupa deafness that cause unapoteza kila kitu on your life?

Then for sure hujawahi kuea happy in ur life au hata ukiipata hailast long 80% ni maumivu tu!

Sasa hapo werevu na ujsiri upi utakuokoa mkuu!
 
Nami pia nina mfano hai. Nimesoma na mwenzetu mpaka la saba, kipindi tunasubiri matokeo, mwenzetu kapata upofu wa macho.
Kwa nini kapata upofu, kama ambavyo unauliza juu ya ukiziwi, sijui kama utapata jibu la Mungu. Ila kitabibu watakupa sababu.
Wakati wewe unaongelea kubaguliwa, kutojichanganya, ufinyu wa fursa n.k., huyu mwenzetu alikwenda shule maalum kujifunza kusoma, akaendelea sekondari, Shahada ya kwanza, ya pili na sasa anafanya PhD. Ameoa na ana watoto, anajichanganya kwenye jumuiya na hakuna anayembagua.
Narudia tena, kwangu Mimi ni jinsi gani unatumia werevu, akili na utashi wako, ndivyo utakavyoyakabili mazingira yoyote yale unayojikuta umo. Kilema hutaweza kukibadili, bali mengine yote yawezekana.

Uko sahihi je! Safari ya kutoka seko hadi kuitafuta PhD yupo mwenyewe yaani kwa juhudi na werevu wake mwenyewe? Bila sponsor?? I mean amesoma na akaingia mtaani kutafuta ajira yake binafsi? Au niulize hvi ameweza vipi kumudu maisha na akafanikiwa hadi kuoa?

Je! Ikiwa penye ajira unabaguliwa no kibarua na sometime unaonekana wa ajabu kutokana na mtazamo wa jamii wewe sio mwerevu? Huna akili na huna utashi?
 
Yalimpata akiwa mtoto, hivyo wazazi walimtafutia shule maalum, ni za serikali, na hata elimu yote ya baadae ni katika mifumo wa serikali, hakuwa na udhamini(sponsorship) maalum.
Ajira za serikali kama kawaida, ila kwenda kuongeza elimu hiyo ni juu ya mtu binafsi, bali vyuo ni hivi vya Tz.
Kuoa, sina uhakika Mwenza alipatikana vipi, ila ni mwelewa na amekuwa msaada mkubwa.
Kuna sheria za kutowabagua wenye matatizo kama haya. Ni juu yako kujua haki na wajibu wako kwa jamii na jamii juu yako. Unabaguliwa, usikae kimya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,328
2,000
Yalimpata akiwa mtoto, hivyo wazazi walimtafutia shule maalum, ni za serikali, na hata elimu yote ya baadae ni katika mifumo wa serikali, hakuwa na udhamini(sponsorship) maalum.
Ajira za serikali kama kawaida, ila kwenda kuongeza elimu hiyo ni juu ya mtu binafsi, bali vyuo ni hivi vya Tz.
Kuoa, sina uhakika Mwenza alipatikana vipi, ila ni mwelewa na amekuwa msaada mkubwa.
Kuna sheria za kutowabagua wenye matatizo kama haya. No juu yakockujua haki na wajibu wako kwa jamii na jamii juu yako. Unabaguliwa, usikae kimya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alipitia wapi kuweza kupata ajira yake serikalini?
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
7,374
2,000
Alipitia wapi kuweza kupata ajira yake serikalini?
Muda unaweza kuwa ni tofauti na sasa, ila nina imani kipaumbele kinatolewa kwa wenzetu hawa. Hakupitia popote, kamaliza masomo kapangiwa kazi. Kafanya Shahada ya pili akajiunga na taasisi tofauti ila ya serikali kwa kuomba kama wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
3,443
2,000
Nina imani hata wewe Unajua kuwa ukiachilia magonjwa/ kilema, mengine yote yanaweza kubadilika.
Si lazima ukizaliwa katika hali duni basi kuishi katika hali hiyo hiyo mpaka mauti, na si lazima ukizaliwa katika hali bora tutaishi katika hali hiyo mpaka mauti.
Tumeumbwa na akili, utashi na dhamira ambazo tukizitumia vizuri, vibaya au kutokuzitumia kabisa, ndio itakapotupa mustakabali wa maisha yetu. Tumejaaliwa werevu wa kuyatawala mazingira yoyote yale tunayojikuta tumo. Je tunatumia aje vipawa hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unasemaje kuhusu hilo kundi jingine la mambo ambayo hauwezi kuyabadilisha kwa mfano kuzaliwa taahira ili kujibu hoja ya mleta hoja?
 
Nyaka-One

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
3,443
2,000
Nami pia nina mfano hai. Nimesoma na mwenzetu mpaka la saba, kipindi tunasubiri matokeo, mwenzetu kapata upofu wa macho.
Kwa nini kapata upofu, kama ambavyo unauliza juu ya ukiziwi, sijui kama utapata jibu la Mungu. Ila kitabibu watakupa sababu.
Wakati wewe unaongelea kubaguliwa, kutojichanganya, ufinyu wa fursa n.k., huyu mwenzetu alikwenda shule maalum kujifunza kusoma, akaendelea sekondari, Shahada ya kwanza, ya pili na sasa anafanya PhD. Ameoa na ana watoto, anajichanganya kwenye jumuiya na hakuna anayembagua.
Narudia tena, kwangu Mimi ni jinsi gani unatumia werevu, akili na utashi wako, ndivyo utakavyoyakabili mazingira yoyote yale unayojikuta umo. Kilema hutaweza kukibadili, bali mengine yote yawezekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kutumia huo huo mfano ulioutoa ni kwa nini kuwe na vipofu wawili mwingine apewe uwezo wa kutumia akili zake vizuri na kuwa na utashi kama huo wa kufanya makubwa na mwingine asiwe na uwezo huo? Je, akili au utashi huo unazaliwa ndani ya mtu mwenyewe na siyo kwamba unatoka mahali pengine nje ya huyo mtu (mfano Mungu mgawa vyote)?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom