Hivi nadharia sahihi ya maisha ni ipi?

Ni sawasawa tu na tofauti iliopo kati ya mtu na mtu bila ya kujali ulemavu. Kuna mwenye mambo mengi na kujituma zaidi na mwingine hafanyi lolote.
Kwa kutumia huo huo mfano ulioutoa ni kwa nini kuwe na vipofu wawili mwingine apewe uwezo wa kutumia akili zake vizuri na kuwa na utashi kama huo wa kufanya makubwa na mwingine asiwe na uwezo huo? Je, akili au utashi huo unazaliwa ndani ya mtu mwenyewe na siyo kwamba unatoka mahali pengine nje ya huyo mtu (mfano Mungu mgawa vyote)?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu fikiria hii!

Unazaliwa kijana mwenye afya njema!

Unafika darasa la pili unapata ukiziwi so unakua kiziwi!(ina maana gani mungu kulifanya hili kwa mwanadamu?)

So hali hiyo ya kuwa kiziwi
-inakufanya upoteze marafiki
-inakufanya uwe mpweke bila marafiki
-upendo toka kwa ndugu unakwisha na unaonekana mzigo
-unasoma kwa shida
-unakonda kea mawazo ya kupuuzwa na marafiki nduguwalimu na hata walimu wa dini
-unakulia maisha ya kubaguliwa shuleni na hata kitaa so unaishi maisha ya kutokua na rafiki wa kudumu
-unamaliza masomo ya chuo unakua mwalimu mhitimu
-ni kiziwi huna uwezo wa kuchagua kazi badala yake kazi ndizo znakuchagua wewe so huna uwezo/uhuru wa kusema ujichanganye na vijana wenzio kupambana kitaa(unashindwa kumudu kazi nyingi zilizipo kitaa hali yako inakulazimu utafute kile ueezacho kumudu)
-employer wanashiw ubaguzi kutoa shavu coz uko deaf
-relatives wanakuona mzigo tu nothing you can do!
-your family ipo na hard life na wewe ndo kidume mkubwa your situation (deaf) inahinder wewe kutoa mchango wako uko jobless na things ni very tight

Hapa ndo unajiuliza why God kakupa deafness that cause unapoteza kila kitu on your life?

Then for sure hujawahi kuea happy in ur life au hata ukiipata hailast long 80% ni maumivu tu!

Sasa hapo werevu na ujsiri upi utakuokoa mkuu!
Kwanini usianze kuhoji hiyo hali ya kuzaliwa na afya kwamba kwanini umezaliwa na afya njema? Kuliko kuanza kuhoji kuondoka kwa hiyo afya njema hali ya kuwa hujui kwanini ulizaliwa na hiyo afya njema.

Lazima pia ujiulize ulikuwa na haki gani za msingi zilizofanya uzaliwe na afya njema kiasi kwamba ukiondokewe hiyo afya njema ndio uhoji?
 
Kwa nini mambo kama hayo yapo kati yetu, Mimi pia sina jibu. Ila ni kuishi nayo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ndio tuseme tu kuwa mungu kaamua tu huyu awe taahira na huyu awe tajiri mwenye furaha,Soon huyu taahira akikutana mbinguni na huyu tajiri then tajiri amkumbushe kuwa kule duniani we ulikua taahira usiejielewa sasa je huyu taahira atafeel vipi?? Atamuonaje au atamureleeaje huyu Mungu?
 
Kuwa na afya
Kwanini usianze kuhoji hiyo hali ya kuzaliwa na afya kwamba kwanini umezaliwa na afya njema? Kuliko kuanza kuhoji kuondoka kwa hiyo afya njema hali ya kuwa hujui kwanini ulizaliwa na hiyo afya njema.

Lazima pia ujiulize ulikuwa na haki gani za msingi zilizofanya uzaliwe na afya njema kiasi kwamba ukiondokewe hiyo afya njema ndio uhoji?
Kuwa na afya njema ni jambo la kawaida ambalo kila binadamu huzaliwa nalo na ndilo la msingi linalimwezesha binadamu kuishi kwa amani na furaha na ili uwe binadamu kamili sharti uwe na afya njema,lakini je kukuondolea afya njema kitendo ambacho kinakufanya upoteze almost everything na kuvuruga kila ndoto njemauliyoota,nachouliza nimepokonywa afya njema nitaabike,nisiwe na furaha na niishi maisha magumu yaliyojaa huzuni ndio anachotaka Mungu yaani niteseke tu while wengine waishi kwa raha mustarehe?? Hiko tu ndo anachotaka yeye? Then wanadamu wote tuna thamani sawa na Mungu anatupenda sana sio?
 
Habari za leo Great thinker!

Bila kupoteza muda niingie moja kwa moja keenye mada

Kwanza kabisa je! Ni kweli kuwa Mungu yupo? Kama ndio je! Mungu aliwaumba wanadamu huku akiwa amewapa matabaka kuwa huyu ataishi maisha ya dhiki maisha yake yote na huyu ataishi maisha ya raha na furaha maisha yake yote? Au huyu ataishi maisha ya huzuni

Na au tuseme kuwa maisha anayoishi mwanadamu fulani hapa duniani ndivyo ambavyo he\she destinied to live?? So anapaswa kukubali hali au maisha ambayo mungu kampangia kuishi hapa duniani?

Kwa mfano mtoto anazaliwa na mama kichaa anakulia jalalani na anafia jalalani,mtoto anazaliwa na wazazi wakulima maskin wa kutupwa anakulia shamba na anakufa akiwa mtu mzima kwa njaa,mtoto anazaliwa taahira na anakufa akiwa mzee taahira pia,anazaliwa kipofu na anakufa kwa kugongwa na gari na mifano mingine kama hiyo

Halafu upande wa pili anazaliwa tajiri na anakufa akiwa tajiri,anazaliwa maisha ya kawaida yakiyojaa furaha na anakufa maisha ya kitajiri yaliyojaa furaha na mifano inayoendana na hiyo

Swali,je! Kwanini mungu anawaweka wanadamu wenye thamani sawa katika hali tofauti maadam hawa wateseke na hawa waishi maisha ya raha mustarehe wakati anajua kuwa kila mwanadamu anapenda maisha mazuri na ya raha?

Kwanini wengine tutiwe ulemavu au udhaifu fulani ambao unatufanya tuishi maisha yasiyo na furaha? Au tuseme tumelaaniwa tu na tunatakiwa tukubali hali hiyo kwa maana ndio destiny yetu hapa duniani?

Kwanini wale wanaomuomba sana mungu hubaki palepale huku wale waliomsahau kabisa wakiwa na maisha ya furaha na raha mustarehe?

Sasa nadharia halisi ya maisha ni ipi? Kusema kuwa wenginr tumetiwa madhaifu kwa maana tumelaaniwa kwa sababu mungu ametaka tu tuwe hivyo? Mbona tunamlilia kila leo? Au ndo tukubalu tu kuwa haya ndo majaaliwa yetu?

MI HATA SIELEWI KWAKWELI!
Ee bwana pole; pia kwanza tafadhali ondoa kwanza hiyo avatar yako. Hiyo inasema mengi tu kuhusu wewe na hali yako ikiwa ni pamoja na destiny yako na pia inajibu maswali karibu yote unayouliza.

Ukweli ni kwamba matatizo ya wanadamu yanatokana na wanadamu wenyewe na jinsi wanavyotumia uhuru wao. Wengi wanateseka kwasababu ya maamuzi yao mabaya au maamuzi ya watu wengine.

Hata siku moja Mungu hampangii mwanadamu mabaya.

Unaweza ukaandamwa na mabaya kutokana na jinsi wewe unavyofanya mfano ukiweka avatar mbaya yaweza kukuathiri kwa namna ya kiroho kwa kukaribisha ulimwengu wa roho kukutendea kulingana na kile unachotumia kujitambulisha.
 
Kuwa na afya

Kuwa na afya njema ni jambo la kawaida ambalo kila binadamu huzaliwa nalo na ndilo la msingi linalimwezesha binadamu kuishi kwa amani na furaha na ili uwe binadamu kamili sharti uwe na afya njema,lakini je kukuondolea afya njema kitendo ambacho kinakufanya upoteze almost everything na kuvuruga kila ndoto njemauliyoota,nachouliza nimepokonywa afya njema nitaabike,nisiwe na furaha na niishi maisha magumu yaliyojaa huzuni ndio anachotaka Mungu yaani niteseke tu while wengine waishi kwa raha mustarehe?? Hiko tu ndo anachotaka yeye? Then wanadamu wote tuna thamani sawa na Mungu anatupenda sana sio?
Haujajibu nilichouliza,nimekuuliza ni haki gani inayotufanya tuzaliwe wazima na afya njema? Unajibu kuwa ndio kawaida,ni wazi hujataka kujiuliza hili mwenyewe unaona ni haki yako kuzaliwa hivyo bila kujua hiyo haki umeipataje? matokeo yake ukiondokewa na hiyo afya njema ndio unahoji!!
 
Ee bwana pole; pia kwanza tafadhali ondoa kwanza hiyo avatar yako. Hiyo inasema mengi tu kuhusu wewe na hali yako ikiwa ni pamoja na destiny yako na pia inajibu maswali karibu yote unayouliza.

Ukweli ni kwamba matatizo ya wanadamu yanatokana na wanadamu wenyewe na jinsi wanavyotumia uhuru wao. Wengi wanateseka kwasababu ya maamuzi yao mabaya au maamuzi ya watu wengine.

Hata siku moja Mungu hampangii mwanadamu mabaya.

Unaweza ukaandamwa na mabaya kutokana na jinsi wewe unavyofanya mfano ukiweka avatar mbaya yaweza kukuathiri kwa namna ya kiroho kwa kukaribisha ulimwengu wa roho kukutendea kulingana na kile unachotumia kujitambulisha.
Asante sana nimekuelewa so nitabadili avatar hii kama ulivyonishauri,

Umesema binadamu wengi tunateseka kutokana na matendo yetu,maamuzi yetu na maamuzi ya watu wengine!

Nakuunga mkono kuwa maamuzi ya watu wengine husababisha mateso kwa wengine na si madogo maamuzi ya watu wengine yanapaswa wakati mwingine kuwa na ubinaadamu sometime!

Nashindwa kukuelewaunapisema maamuzi yetu wenyewe nayi huchangia tuteseke,sasa je kuoata Ukiziwi ningali darasa la tatu hayo ni maamuzi yangu? Mimi nimevumilia mengi hadi nimehitimu chuo(maamuzu yangu licha ya ulemavu ni kuvumilia yote hadi nitimize ndoto hiyo) lakini maamuzi ya watu wengine Waajiri na hata ndugu yanapelekea kuumizwa zaidi lakini hilo sio la kujali zaidi ya kutazama mbele!

Uvumilivu wangu,juhudi na ari ya kupigania elimu yangu na ari ya kusaka kibarua/ajira ni maamuzi yanayostahili kuumizwakiasi hiki??

Kwanini Mungu hakuniachia Masikio yangu nipambane kama wenzangu wanavyopambana kwa maana through fursa na mazingira kama sio hili tatzo ningekua mbali mno!

Ina maana gani kufanywa mtu wa kutaabika mno? Kwann wanadamu wanatunukiwa furaha amani na upendo na kwanini wengine watunukiwe MATATIZO? Na ukitazama utakuta wale wenye hali duni!MATATIZO ndio ambao hawaishi kumuomba mungu usiku na mchana na wale wenye furaha na kila kitu ni kama hawamjui mungu,KWANINI MUNGU ASIWAPE WAMUOMBAO badala yake wale wamuombao na kumcha usiku na mchana wanazidi kutopea katika lindi la matatzo huku hawa wenginr wakizidishiwa maradufu??
Hivi kuna Mungu ndugu yangu??

Nae kaumba wa kuishi maisha mazuri na wa kutaabika?
 
Naelewa ndugu ni vigumu sana kuelewa kwanini kuna matatizo na dhuluma nyingi duniani hata kwa wale wasio na hatia kama vile watoto wachanga.

Kama nilivyosema ni either hutokana na maamuzi au makosa ya mtu mwenyewe au watu wengine. Na makosa hayo yaweza kufanywa katika mwili au katika roho. Kwa mfano mtoto anaweza kuteseka hata kufa kutokana na makosa ya wazazi wake. Mathalani mzazi ambaye ni mshirikina manake anashirikiana na ulimwengu wa giza huweza kuleta matatizo makubwa kwa uzao wake wote mpaka kwa wajukuu na vitukuu.

Ni kutokana na maamuzi yake yaliyompa shetani nafasi ya kutenda uovu.

Kuna madhara ambayo yalishatendeka katika mwili hubaki hivyo siku zote. Mfano ukipatwa ajali mguu ukakatwa usitegemee siku moja mguu wako utaota.

Sio kwamba hakuna matumaini, la hasha Mungu anaweza akakupa amani na furaha hata katika hali hiyo ukawa na furaha kuliko wale wenye miguu yote. Lakini yakupasa kumwomba Mungu na kuwa pamoja naye badala ya kumlaumu kwani kufanya hivyo husababisha shida zaidi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom