Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 12,484
- 19,516
Huko kwenye Nishati wala sijautafuta sababu kinachoendelea hata kipofu asiyeona anasikia...
Nikajaribu kuutafuta kwenye Kilimo; ila sintofahamu za kuuza na kutokuuza, vyakula kupanda bei na hali ya mkulima (peasant kuendelea kushuka) sidhani kama utakuwa huko....
Lakini nadhani upo kwenye Utalii; na matokeo ya Royal Tour yanatakuwa yanajionesha (sadly kwa kutokuwepo dollar nadhani hata huku utakuwa haupo sababu matokeo ya kule tungeyaona huku)
Kwenye michezo labda, hizi faranga za hapa na pale zinazowekwa huenda zinasaidia (lakini nikipikicha macho na kuangalia naona kwamba kuwasaidia Simba na Yanga pekee bila kuwekeza kwenye grassroots ni kuongeza matabaka wala hakukuzi soka; na kama hawa watu wa soka waliweza kula mapesa ya FIFA ya kila mwaka sidhani kama hizi faranga chache zitaleta mabadiliko)
Lakini sikati tamaa huenda tuna undugu na umoja wa kitaifa..., ila nikiona ndugu zangu wa makabila tofauti na Imani tofauti wanabaguana na kuona wenzao duni kuliko hata kabla..., (nadhani huku mwingi ndio haupo kabisa)...
Ngoja lakini..., Madarasa je yale maelfu kwa maelfu yaliyojengwa na Zahanati ? (Nadhani hata mpingaji hawezi kusema huu sio mwingi)..., Lakini najiuliza sasa haya Madarasa na Zahanati mbona haviendani na ongezeko la wataalamu na wakufunzi wa kuweza kuyatumia hayo ? (Sijaona Ajira zinaongezeka)...., Au siku hizi Teknolojia imefanya hadi matofari kuweza kutoa Elimu na Kutoa Tiba ?
Demokrasia Je ? nadhani huko nisipoteze muda kuangalia ingawa tunaambiwa vyombo vimekuwa huru lakini wanachohabarisha ni kama kinatoka sehemu moja (yaani wamekuwa propaganda machines)..
Najiuliza tena huu Mwingi unapigwa wapi ? Binafsi sijauona au umekuwa mwingi hadi hauonekani ?