Nimeona mahali fulani Rais Mstaafu akisema tunakwama wapi hadi sasa kuna walimu wa daraja la 3A.
Yeye akifikiri kuwa suala hilo ni mindset tu ya watunga sera lakini ni suala linalowezekana.
na mimi namuunga mkono kuwa suala hili linawezekana sana iwapo serikali itajali maslahi ya elimu.
Wale wamama wanaofundisha KKK huku wakiimba na kuruka kwenye madarasa ya vumbi ama chini ya mti,Mungu awabariki sana. Kuna viongozi wanaamini wamama hao hawana masters kwa sababu ni vilaza.Lakini elimu ya Tanzania imefanywa kama anasa.
Wako watu wengi wameshindwa kufikia malengo yao ya elimu kwa sababu ya gharama za masomo.
Wafanye kutoa scholarships kwa kila mtu anayetaka kusoma hasa walimu hao wanaowaita wa daraja la 3A waone kama kuna mtu ataishia hapo alipo.
Pia nimeshangazwa na mtu kama yeye aliyewahi kuwa Rais hajui kuwa maslahi ndiyo chanzo cha kuwa na walimu wenye kiwango kidogo cha elimu.Serikali iweke kiwango cha mshahara wa milioni 3 kwa mtu mwenye masters anayefundisha shule ya msingi washangae jinsi walimu watakavyojitokeza kujiendeleza na watazipata hizo masters.
Pia ijaribu kuajiri walimu wa masters kwa mshahara wa laki 4 na kuwapeleka vijijini iwapo watawapata.Wakiwapata watakopa na kununua boda boda na wataacha kazi na kuwa waendesha boda. Mwendesha boda ana uhakika wa kupata laki 6 akiwa mvivu sana hadi milioni 1 kwa mwezi akijituma kazini.
Mwisho nadhani tuna mitaala ya kipumbavu sana ambapo tunayofundisha ujinga mwingi kupoteza muda badala ya kufundisha mambo ya msingi yanayoweza kutatua changamoto zetu.
Hii mitaala ni kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu. Haya yote yanahitaji Rais mwehu kabisa kufuta huu upumbavu.
Kwa wagombea wanajitokeza sasa sijaona mtu mwenye fikra kama hizi.
Tunapaswa kuanza upya kabisa na kufikiri kwa namna yetu.Tuchague kwa umakini sana vitabu vya kusoma. Tuache mawazo ya wajinga wanaoamini elimu mfumo wa kubagua watu waliofeli na kuwaita hawana akili na waliofaulu kuwaita wana akili.
Tukiingia mtaani unakutana na wasio na akili ndio matajiri wenye akili ni wezi wa mali za umma na wauza nchi kupitia dili za mikataba.Wasomi wakitunga sheria kujipendelea na kutumia vyombo vya dola kulinda maslahi yao.
Wasomi wetu wanatengeneza kama kundi la kigaidi ili kuendelea kuwatawala wengi.Watachukua kodi zao,watazitumia wapendavyo na kurudisha ziada kwa walio wengi.
Turudi tufikiri upya tukitaka kuwa wakweli.