Tanzania tunazidi kurudi nyuma kwenye Teknolojia

Nicklaus

JF-Expert Member
Sep 24, 2014
451
455
Wakati dunia ikiienda kasi kwenye technology hasa mifumo ya kifedha, inayorahisisha malipo, hali imekuwa tofauti kwenye baadhi ya taasisi za fedha nchini.

CRDB hasa kwenye mfumo wao Internet banking, umekuwa na shida za mara kwa mara unaolalamikiwa na wateja lakini hakuna linalofanyika kurekebisha.

Mara ya kwanza nilishidwa kupata OTP (one time password) kupitia sms za kawaida, nikiwasiliana nao, hapa tulisumbuana kwa week nzima, niseme tu wana huduma mbaya za customer services; hawajibu kwa wakati na wengi hawajui wanachokifanya.

Wakashauri niwezeshe huduma kupokea OTP kupitia Whatsapp, hili nalo likiwa mtihani, ilichukua week kuweza kuwa active, kumbuka wakati huu wote siwezi kufanya lolote kwenye account yangu.

Atimaye huduma ikawezeshwa na nikaweza kutumia tena kufanya miamala kama kawaida, lakini kinachonisikitisha haikudumu ndani ya week mbili, tatizo likarudi palepale, mpaka mda huu ninapoandika siwezi kufanya miamala kwenye account. Nimewasiliana nao lakini kimya hakuna msaada toka juzi.

Sasa najiuliza, hii mifumo imewashinda? wameitoa wapi? mana huku duniani watu wako mbali sana hasa kwenye mifumo ya kifedha.

NB: Sipo nchini ila ningekuwepo hakika ningehama hii bank mara moja, CRDB na bank kama hizi ni mzigo kwa ustawi wa taifa.​
 
Back
Top Bottom