Hivi muda wa MWANAMUME kurudi nyumbani ni saa ngapi?

inategemeana na kazi unayoifanya,uamuzi wa mwanaume,tabia ya mwanamke,...lakn kwa upande wangu mimi kutokana na kazi ninayofanya na tabia ya mwanamke wangu napenda zaidi kurudi asubuhi,akiwa mke wangu anajiandaa kwenda kazini

Igwe watoto hawakawi kukuita "ANKO" utajisikiaje?
 
Majukumu hayakwepeke....ila kuwa na ratiba ya kurudi 12 kama kuku hapana...
Kurudi inakua muda wowote toka sa 11 jioni hadi saa 11 asubuhi.....

Hebu tupindue shilingi upande mwingine itakuaje?
 
Hebu tupindue shilingi upande mwingine itakuaje?

Upande wa pili?
Hebu pindua wewe LF.....
By the way, haimaanishi kwamba kila siku unarudi umechelewa....mostly waweza kuwahi (kutimiza majukumu yako nyumbani)....ila kuchelewa sio mwiko....
 
Hebu niendelee kuwasikiliza kina baba hapa ...

haya endeleeni kutwambia ni muda gani muafaka kuingia home?

mwanaume huwa anachelewa kazini na kwenye mishemishe zake tu sio nyumbani, hii kitu inabidi mfundishwe kwenye ile party yenu........
mi sijawahi kuchelewa kuingia home, koz hakuna muda muafaka kwa mwanaume kurudi maskani!!
umenipata hapo FirstLady1
 
]Makubwaaaaa[/COLOR]

hakuna makubwa hapo,kwani na nyie muda wenu wa kufika nyumbani ni saa ngapi vile?...ngoja nimsubiri Black Woman alete hoja hapa..namuona hapo chini akipitia hoja za wenzake
 
............wanawake wana kazi sana, mtu linarudi saa nane usiku. hajali watoto wamekula, wamelala, wanaumwa wanahitaji kucheza na kuzungumza nae kupata ukaribu wa baba mke ana hitaji nini, alipatwa na tatizo gani au amekwazwa anahtaji faraja akaaaaa yeyey bia. mwanaume wa namna hiyo akiulizwa watadai alikua na wenzie wanajadili madili madili gani hayo mpaka saa nane usiku. hivi na wanawake wakiamua hivyo inakuwaje?

kesho na keshokutwa watoto watakapoharibika atasema mama yao hakuwaangalia vyema anasahau yeye anarudi saa nane, au watoto wakikosa upendo kwake atalalamika kumbe hakujenga bond toka mwanzo na mbaya zaidi jirani yake akimmegea atalalamika mkewe mzinzi wakati hakuwepo kumfariji mkewe kuzungumza kuliwazana na kuwa pamoja....
 
Jana jirani yangu wamebwatizana na mkewe kisa jamaa karudi nyumbani saa Nne usiku wakati kawaida yake saa mbili huwa anakuwa sebuleni anaangalia TV.

Nikajiuliza kwani ni haki kwa mwanaume kupangiwa na mke wake muda wa kurudi nyumbani? Muda wa mwanaume kurudi nyumbani ni upi?
Baba hachelewagi nyumbani bana....! Na akipitia mahali, atakuwa amepitia kwake pia....! So, no limitation of time to husbands to be at home....!
 

Upande wa pili?
Hebu pindua wewe LF.....
By the way, haimaanishi kwamba kila siku unarudi umechelewa....mostly waweza kuwahi (kutimiza majukumu yako nyumbani)....ila kuchelewa sio mwiko....

Upande wa pili Mrs. anapoamua nayeye arudi muda wowote kati ya saa kumi na 11 jioni na saa 11 asubuhi.
 
RR... fika utoke huo ndo ubaba(tangu jadi)... unaogopa nini?...kutembea usiku kucha bila sababu za maana tukuitejee..
Majukumu hayakwepeke....ila kuwa na ratiba ya kurudi 12 kama kuku hapana...
Kurudi inakua muda wowote toka sa 11 jioni hadi saa 11 asubuhi.....
 
Muda wa mwanaume kurudi home ni pale mke wake anaifanya home inavutia na inatamanisha kurudi home. full stop (na muda wa mke pia unategemea juhudi za mume wake)
 
Muda wa mwanaume kurudi home ni pale mke wake anaifanya home inavutia na inatamanisha kurudi home. full stop (na muda wa mke pia unategemea juhudi za mume wake)

kwahiyo wanaweza kurudi hata kama kazi hazijaisha ili mradi panavutia?
 
Mimi kwangu sina muda maarumu,mara 11 jioni,mara saa 2,mara saa 5,sometime saa 8 na ukiona mkeo anakupigia kelele ooooh sijui nini, toka nae na siku hiyo uhakikishe mnarudi alfajiri ili ajionee asinzie mezani aliwe na mbu akisema baba watoto twende we unamwambia subiri kidogo tu mpenzi tunaondoka sasa hivi,uone kama atarudia tena ukimwambia tena twende atakataa ila atakwambi usirudi alfajiri.

hahahahaah nimecheka mpaka basi ndo zako hizo eeh.Na unaendaga sehemu gani mwenzetu hizo zenye mbu? dah bonge la technique
 
Back
Top Bottom