Hivi muda wa MWANAMUME kurudi nyumbani ni saa ngapi?

Yes he is...hapa ndo waasia/arabs wanapotuacha...kuwahi kurudi ni wajibu sasa hiyo fatherhood exercise unaifanya saa ngapi?,rudi afu toka tena jirani, kama kuna bomoa bomoa ujipange na wenzako...au kuna ka vitz ka blue kanakujakuja kwa home pia wakuhabarishe..
Are u serious mkuu?
 
Hebu niendelee kuwasikiliza kina baba hapa ...

haya endeleeni kutwambia ni muda gani muafaka kuingia home?
 
........Mwanaume anatakiwa kurudi home baada ya muda wa kazi kuisha. Rudi nyumbani mapema ucheze na mtoto/watoto, mle dinner pamoja na familia yako inapendeza kwa kweli.
 
........Mwanaume anatakiwa kurudi home baada ya muda wa kazi kuisha. Rudi nyumbani mapema ucheze na mtoto/watoto, mle dinner pamoja na familia yako inapendeza kwa kweli.
Kuna wengine tukiwahi, watoto wanakosa amani.....ili wawe na amani tunarudi wakiwa wameshalala, na tunaondoka kabla hawajaamka.... Watoto tunaonana weekend...........
 
si vyema kumuuliza sana mwanaume unarudi saa ngapi na hata akichelewa akigonga saa 8 mfungulie tena umpe na busu na kumwambia pole na kazi, na kama hakukwambia kitu kuhusu kula muulize mume wangu umekula au nikutayarishie chakula, wanawake wenzangu neno linasema mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba kwa mikono yake, ila kwa kaka zangu muwe mnatufikiria mkeo anakupenda ndo mana anapenda atleast uwahi kurudi, jamani kuna raha unapopika chakula mumeo ale na akifurahie na mule wote kama familia, na kama mna watoto malezi ni ya wote, msituachie watoto tulee wenyewe, sasa kama baba unarudi saa 8 kila siku kweli utajua maendeleo ya mwanao? Neno linasema mwanaume ndo kichwa cha familia
 
dear...tumesema inategemea jamani....kama mimi ungependa nirudi saa ngapi?

Saa mbili mpaka saa nne usiku ikizidi hapo kuwe na sababu ya kueleweka sio ooh ikaenda ikarudi nilipata emergency oh
mnatakiwa muwe karibu na family zenu ,mjue maendeleo ya watoto wenu..kuna matatizo gani nyumbani sitegemei uingie home saa sita muanze kupeana update na wife wakati ni muda wa kulala
Hii ratiba ya kuingia saa tano au sita usiku unalala asubuhi kazini kurudi tena saa sita usiku ...aggggh habari za familia mtazijuaje?
 
mimi sinywi pombe,sivuti,sipendi anasa za aina yeyote!
Lakini,sipendi kurudi home mapema make mishemishe zangu hazitafanikiwa,nikikaa na walevi bar,napata michongo mingi ya kueleweka.
 
Mimi kwangu sina muda maarumu,mara 11 jioni,mara saa 2,mara saa 5,sometime saa 8 na ukiona mkeo anakupigia kelele ooooh sijui nini, toka nae na siku hiyo uhakikishe mnarudi alfajiri ili ajionee asinzie mezani aliwe na mbu akisema baba watoto twende we unamwambia subiri kidogo tu mpenzi tunaondoka sasa hivi,uone kama atarudia tena ukimwambia tena twende atakataa ila atakwambi usirudi alfajiri.

duh,kweli wewe kichomi
 
Hebu niendelee kuwasikiliza kina baba hapa ...

haya endeleeni kutwambia ni muda gani muafaka kuingia home?

inategemeana na kazi unayoifanya,uamuzi wa mwanaume,tabia ya mwanamke,...lakn kwa upande wangu mimi kutokana na kazi ninayofanya na tabia ya mwanamke wangu napenda zaidi kurudi asubuhi,akiwa mke wangu anajiandaa kwenda kazini
 
hahahahahah IGWE mbona una vituko wewe asubuhi ..mie nakumwagia kikaango cha mayai usoni ..am kidding inakupasa ubadilike huwezi jua ni kiasi gani unamkwaza mwenza wako
 
Saa mbili mpaka saa nne usiku ikizidi hapo kuwe na sababu ya kueleweka sio ooh ikaenda ikarudi nilipata emergency oh
mnatakiwa muwe karibu na family zenu ,mjue maendeleo ya watoto wenu..kuna matatizo gani nyumbani sitegemei uingie home saa sita muanze kupeana update na wife wakati ni muda wa kulala
Hii ratiba ya kuingia saa tano au sita usiku unalala asubuhi kazini kurudi tena saa sita usiku ...aggggh habari za familia mtazijuaje?

maendeleo ya familia na matatizo ya nyumbani wewe kama mama ni jukumu lako kuniambia,...kama yapo anyway......ngoja turudi kule walikotoka wazazi wetu nadhani heshima ya ndoa inaweza rudi....mpo hapo?
 
hahahahahah IGWE mbona una vituko wewe asubuhi ..mie nakumwagia kikaango cha mayai usoni ..am kidding inakupasa ubadile huwezi jua ni kiasi gani unamkwaza mwenza wako

ukinimwagia tu_naingia bafuni,..baada ya hapo hatuonani mpaka w/end.,unajua siku hizi mmezidi kuhoji kila kitu eti kiende kwa muda na ratiba....maisha na mihangaiko yetu kina iwe hairuhusu kujipangia ratiba.
 
maendeleo ya familia na matatizo ya nyumbani wewe kama mama ni jukumu lako kuniambia,...kama yapo anyway......ngoja turudi kule walikotoka wazazi wetu nadhani heshima ya ndoa inaweza rudi....mpo hapo?

kUKWAMBIA SAA NGAPI WAKATI WEWE UNARUDI ASUBUHI IGWE?
 
Yes he is...hapa ndo waasia/arabs wanapotuacha...kuwahi kurudi ni wajibu sasa hiyo fatherhood exercise unaifanya saa ngapi?,rudi afu toka tena jirani, kama kuna bomoa bomoa ujipange na wenzako...au kuna ka vitz ka blue kanakujakuja kwa home pia wakuhabarishe..

Majukumu hayakwepeke....ila kuwa na ratiba ya kurudi 12 kama kuku hapana...
Kurudi inakua muda wowote toka sa 11 jioni hadi saa 11 asubuhi.....
 
Ndoa ni kuheshimiana. Wewe muda unaotoka kazini rudi home, kama kuna mahali unapita mtaarifu mapema mkeo. Jamani, mwanamke anahitaji matunzo na haki ya kuongea katika nyumba. Akiona unachelewa na hajui ulipo inam'bidi akuulize na ana haki ya kukuuliza. Jamani tuwapende wake zetu na tuwape nafasi ya kuongea.
 
Back
Top Bottom