Hivi mtu akifariki kwanini asemwe kafariki dunia?

Hivi mtu akifariki kwanini asemwe kafariki dunia?

Hiki kiswahili kinanipa tabu mtu kafariki magomeni badala ya kusema kafariki magomeni mtu unasema kafariki dunia kwani magomeni ndio dunia?
Neno 'fariki' linamaanisha 'ondoka, achanisha, tenga na...'.
Kufariki Magomeni maana yake ni kuondoka Magomeni, labda ukaenda mtaa mwingine au mji mwingine. Kufariki dunia ni kutengana na dunia, kuondoka duniani, yaani kufa.
Katika kiswahili sahihi, neno "fariki" halisimami peke yake bila kusema amefariki wapi. Kama mtu amekufa, tungo sahihi ni kusema "Fulani amefariki dunia" na siyo kusema tu "Fulani amefariki", inakuwa haijitoshelezi.
 
Wakuja wanataka kujifananisha Kiswahili na Waswahili wa Magomeni! Majanga.
 
Hivi ni kikombe ndio kinabeba maji au maji ndio yanabeba kikombe?
Hiki Kiswahili kinanipa tabu mtu kafariki Magomeni badala ya kusema kafariki Magomeni mtu unasema kafariki dunia kwani Magomeni ndio dunia?

Jr[emoji769]
 
Kifupi maana yake hayupo kwenye ulimwengu wowote unaoonekana .kaenda Kule aliko toka yaani ulimwengu wa roho.
 
Back
Top Bottom