NDABANINGI STHOLE
Senior Member
- Mar 4, 2019
- 154
- 102
Big up mkuuMkuu naweza sema kwamba hayo maeneo ndiyo yalikaliwa na wasukuma mwanzon na kwa mda mrefu sana kumbuka walikua wanatoka upande wa maghalibi ng'weri na kuelekea mashariki ambapo walienda kukumbana na wamaasai na kuweza kupata mikikimikik hasa watoto wa kiume (hapa staliweka wazi sana ) lakin ushawahi fatilia kwenye maholelo ya kwetu chanzo cha kuwa wanapandwa na mizim na kuongea kimasai/ama kitaturu chanzo nin???
Kwain hifadhi ya maswa kwenye milima kuna nyumba nyingi za kale hata makaburi ya watu maalufu kama vile Nyendwa, Sita (huyu mpaka leo kuna nyumba ake na mabak ya ziz na ng'ombe wake waliobadilika na kuwa mawe na kisima chake na alisafir mpaka Butiama na alitabiri mpaka kuzaliwa kwa nyelele) mtemi wa mwisho wa meadu (ngwesa) .
Lakin pia fatilia story ya Ng'witulo gwa Ng'wawilyamu miaka ya 1950.
Kwa kifupi wasukuma wamegawanyika kuanzia zaman na hasa kufatana na utawala wao na hata maeneo yao na kuweza kuunda makundi yaliyopo mpaka sasa kama nilivyo yataja.
Na ikumbukwe kwamba kikwetu asili aridhi yote ni yawanawake na ndio walikua watawala japo kulingana na wakati walikua wanapinduliwa na waume zao .
Lakin ti kwa hekima mpaka leo tunawaanzi hao watawala wa mwanzo kwa salam japo sku izi watu hawajui ata maana ya hizo hekima za salam (lwimbo) na kwa hawa watawala kunawaliokuwa na maeneo makubwa sana na wanaonekana kuwanaidadi kubwa ya watu kama vile MINZA,( wanatumia EMINZA), Wengine ni akina.
NKWAYA,SEGA,NKWIMBA,SABHE,NG'WASHI,n.k
Na kuna hawa wanasalimiwa NG'WAKADILU walifata kwa huyu mama KADILU hakuwa mtemi na alizaliwa tu kwa kufata jua na asubuhi na alipaya pia wa kumuunzi kwa salam