Hivi mradi wa DARTS aliubuni nani? Was it the best/cheaper option

.....Haitopunguza foleni hata kwa asilimia 1 isipokuwa itawasaidia sana wanaotumia public transport.

Itapunguza foleni mkuu....siwezi kujua kwa asilimia ngapi....ila sio asilimia moja...ni zaidi sana.
Watu wanatumia magari binafsi kwa kero za usafiri wa umma. Ni ghali sana kuingia mjini kwa gari binafsi.
 
Kwahiyo wasitishe mradi? Binadamu kweli huwezi kumridhisha! hata ufanyeje,utalaumiwa tu..
Nakwambia ukiwajengea flyovers kesho watakuja na hiliii yaani sijui uvumilivu unawashinda nini kuna watu wanaona project ime fail hata kabla ya kuanza ila wanaosimamia wanasema tusubili wao hawajashindwa sasa si tusubili then tutaangalia nani ni mkweli na nani awajibishwe kutokana na matokeo husika sababu ile sii nyumba ni barabara iliyotumia billions of money sasa kama una conclude hata kitu bila kuanza ni ku halalisha tumetupa helaaa
 
Itapunguza foleni mkuu....siwezi kujua kwa asilimia ngapi....ila sio asilimia moja...ni zaidi sana.
Watu wanatumia magari binafsi kwa kero za usafiri wa umma. Ni ghali sana kuingia mjini kwa gari binafsi.
Kam watu wataamua kupaki magari yao binafsi na kutumia public, then magari barabarani yatakuwa machache na hence folenmi itapungua.
I agree.
 
  • Thanks
Reactions: RR
Kam watu wataamua kupaki magari yao binafsi na kutumia public, then magari barabarani yatakuwa machache na hence folenmi itapungua.
I agree.

Lengo kuu la brt ni hilo...efficient public transport!
Bila usafiri wa umma kuwa thabiti uchumi unadumaa! Na uchafuzi wa mazingira kwa moshi wa magari mengi zaidi. Kwa hali ilivyo sasa, kila mtu anatamani kuwa na gari dogo.
 
Nimekuwa nikitafakari namna ambavyo nchi yangu inaendeshwa naomba kuwashirikisha GT wenzangu juu ya potential white elephant iliyotengenezwa kwenye DARTS.
- Je ni kweli DARTS ilikuwa ndiyo best option (in terms of cost, efficiency and priority)ya kupunguza msongamano Dar?
- Je hizi nyumba za kusubiria wasafiri zilikuwa zina ulazima wa kujengwa kwa gharama kama ilivyofanyika sasa
- Je namna ambayo barabara zimejengwa itapunguza foleni kweli?

Kwa maoni yangu (I stand to be corrected), DARTS haitapunguza msongamano na huenda ikaongeza, na kama kweli mradi huu ulijadiliwa kwa mapana yanayostahili then kuna umuhimu wa watu waliodhani huu ndio mwarobaini wa msongamano wa magari Dar(ni muhimu kuwafahamu ili tuweze kujiridhisha na weledi wao, au hata IQ zao)

Kama ningekuwa mimi ningeanza na kujenga fly overs kwanza, then barabara za pembezoni kwanza na kama pesa bado ipo ningeimalisha usafiri wa reli ndani ya jiji la Dar pamoja na kuimalisha uchukuzi wa mizigo kutokea bandari ya Dar kwa kuweka dry port kubwa Ruvu au Mlandizi.
Ukiziwekea lami barabara za Kinyerezi-Mbezi Lousi, Makongo Juu-Goba, Tangi Bovu-Morogoro Rd, Mbagala-Kipawa/Banana/Ukonga utapunguza msongamano kwenye barabara ndani ya jiji la Dar kwa kiwango kikubwa na kwa gharama ndogo kuliko huu wendawazimu wa DARTS.
tusubiri tuone tija kwanza baada ya hapo ndo ulete uzi wako hapa pamoja na ulicho kiona kwani mradi haujaisha, na hujui serikali imejipanga kwa vipi hayo ulio leta tayari wamesha yaona na wanajua watadili nayo vipi unacho kisema ni sawa na KUJICHAMBA KABLA HATA UJAJISAIDIA HAJA KUBWA
 
Nimevutiwa na mwamko wa wengi kutaka kujua kama huu mradi utasaidia kupunguza msongamano. Hii ni topic pana na ni vizuri kuwa wengi mnatoa maoni yanayotoka moyoni na kwa nia njema. Kinachokosekana ni maoni a wataalamu wanaoijuia writeup ya huo mradi. Nianze kwa kukiri kuwa mimi pia sijaiona proposal ya huo mradi ila natoa maoni yangu tu kuongezea ya wachangiaji waliopita.

Ni vizuri tufahamu kuwa performance ya barabara yoyote inategemea factors tatu kubwa: roadway (geometric), traffic, and environmental conditions. Kama mbili zikibakia constant na moja kati ya hizo inabadilika, kwa mfano mvua ikanyesha (one of the environmental conditions), basi performance ya barabara itakuwa poor. Likewise, kama barabara ni ya wima (tangent), ukabadilisha sehemu yake ukaweka a sharp curve, au barabara iwe na mashimo (roadway factors), basi performance itapungua hata kama traffic and environmental conditions zitabaki constant. Sijaona michoro ya huo mradi ila ninafikiri kuwa watakuwa wameongeza at least one lane for BRT kwa hiyo one of the important geometric factors imeongezeka. Kuna wadau wanaongelea kupunguzwa kwa upana wa individual lanes ila nafikiri anamaanisha lane ya BRT sio pana. Kutegemea na design speed hawahitaji ziwe nene sana kwa sababu zimetenganishwa na normal traffic kutumia a barrier, preferably, a raised curb (sina uhakika sababu sijaona michoro).

Sasa tuje kwenye swali la msingi, je itapuguza foleni? Ni vizuri tukajua kuwa kupungua au kuongezeka kwa congestion ni swala la demand and supply. Hili la congestion ni complex na kulijibu kwa sentensi chache na fupi ni kutolitendea haki. Ukiangalia barabara moja peke yake, say, Kimara to Kivukoni, tuanze kwa kuangalia demand in terms of trips badala ya magari. Wapo wengi waliopo kwenye lower na middle class ambao hawatumii mabasi kwa sababu ya karaa za usafiri huo ulivyo. Kama mabasi yatakuwa na ratiba zinazoeleweka na yawe mazuri, kwa wengi wanaoenda ofisini au shuleni na kutokuwa na secondary trips, lower na middle class wengi watafanya modal migration from automobile to transit based for most of their trips. Kama ninaishi Kimara na kuna park-and-ride facility nzuri kwenye vituo vikubwa, kama time savings and fuel savings ni significant, nitabadilisha mode of transportation kirahisi. Watu wengi wakitumia mabasi hayo kwenda kazini, congestion itapungua kweye hizo barabara, hususani kwenye AM and PM peak kama watumiaji wa barabara nyingine hawatahaia hapo. Tatizo ni kuwa baadhi ya wanaoenda mjini kutumia barabara za mabibo through Kigogo au wanaokatiza Sinza kwenda Mwenge, wanaweza kuhamia Morogoro road (path of the least resistance). Ila watakaoamua kutumia transit watafika mapema kuliko wanaoendesha magari yao. Ikumbukwe kuwa kutakuwa na routes za express pia ambazo hazisimami kila kituo.

Naomba niwaulize swali. Kama hayo mabasi yakiwa mazuri sana na quality of service iwe nzuri na yawe efficient, hamuoni kuwa vipanya na madaladala mengine yatatoweka taratibu kwenye hizo routes? Madaladala yakitoweka au hata yakipungua morogoro road (change in traffic conditions) kwenye normal lane, traffic stream ita improve sana, hata automobiles zitatembea vizuri. Ukiondoa mabasi madogo u replace na makubwa yanayofuata sharia, na ukumbuke yatakuwa na prepaid cards option ambayo itafanya ridership iwe stable, traffic will improve.

Naomba pia nisisahau kusema kuwa BRT ni part of solution na sio the whole package. Ring roads zitasaidia sana kupunguza foleni za Dar. Hata hizo flyovers mnazozisema zinapunguza foleni kwenye junctions ila kukiwa na bottleneck downstream, utashangaa foleni itakuwa mbaya zaidi ya mataa, ila itachukua muda kulielezea hilo kwa urefu.

Kuna mmoja wetu hapa amesema kuwa kuna mhandisi wa wizara ya ujenzi amemweleza kuwa hata Magufuli hawezi kubadilisha chochote kwenye huu mradi. Tuache maneno ya mitaani. Magufuli hana ruhusa ya kubadilisha ujenzi wa barabara yeyote, yeye ni mwanasiasa, barabara inajengwa na wajenzi, si wanasiasa. Yeye kama mwanasiasa anasimamia policy, anaweza kupiga mkwara kama wako behind schedule au quality is visibly poor. Magufuli hawezi kubadilisha upana wa barabara kama unavyoelezea. In fact, hata contractor hawezi kubadilisha kilichopo kwenye mchoro, ni gharama sana kufanya design modification wakati wa ujenzi. Huu ujenzi wa hii BRT sio mrahisi kama nitakavyoelezea kwenye aya ifuatayo.

Kama una nyumba uliijenga wakati umeanza maisha, baadaye mambo yamekukubali unataka kuifanya iwe ya kisasa, uweke choo cha ndani, bathtub, ubadilishe interior and exterior design iwe kama nyumba za kileo zinazojengwa Mbweni, Ununio au Bahari beach, utakubaliana na mimi kuwa sio kazi rahisi na pia haitakuwa exactly the same. Kuna restrictions kwa sababu unachofanya ni retrofitting. The original design did not consider kuwa baadaye utakuwa na hela na kutaka nyumba yenye amenities za kisasa zaidi. Hicho ndicho kinachofanyika kwenye mradi wa mabasi yaendayo kasi ya Dar kwa sababu mabasi yaendayo kasi hayakuwa part of the original plan. Kuna constraints nyingi mno kubwa ikiwa right-of-way.

Sitaki kuwachosha na hoja zangu naomba niishie hapo kwa leo. Ninachowashauri tu ni kama unamfaamu mtu anayefanya kazi kwenye huu mradi muwaombe waje kuchangia hoja na tuwaulize maswali. Pia ijulikane kuwa huu ni moja ya miradi michache ya aina hii barani Africa na kama ukiwa executed vizuri una potential of proof of concept na wengi watakuja kujufunza kwetu.

Title ina swali, was it the best/cheaper option? Cheaper option, for this size of infrastructure project, don't go for a cheaper option, pursue the most effective and feasible option. Was it the best option? it is hard to tell!

Samahani kwa typos, for some reasons editor ya JF inanisumbua.


Asanteni.
Very nice professional analysis haya ndiyo tunayohitaji kuna vitu ni vya kitaalamu sasa watu wanaleta story za vijiweni na ofisini bwana swala traffic jam hata developed countries lipo pamoja na mi flyovers. Jamani vitu vingine tuwe wavumilivu tu
 
Kwa kutazama tu huu mradi wamekosea sana. Mimì nilitarajia angalau wangeongeza barabara mbili pembeni kumbe la.
Na pia reli walizotumia kujenga hivi vituo ukizitandaza kwenye hiyo barabara ya zege zinatosha kabisa kinachobaki hapo ni kununua tu vichwa vidogo vya treni.
Tungewaomba Hata wale matajiri wetu wa viwanda vya juis na na soda aliotuambia Muhongo watununulie then warejeshewe kidogokidogo nadhan wasingeshindwa

Tehe! tehe! tehe!, wewe iko jua chuma ya reli?
 
Very nice professional analysis haya ndiyo tunayohitaji kuna vitu ni vya kitaalamu sasa watu wanaleta story za vijiweni na ofisini bwana swala traffic jam hata developed countries lipo pamoja na mi flyovers. Jamani vitu vingine tuwe wavumilivu tu

Huhitaji kusubiri mpaka mradi uanze kufanya kazi ili ujue ufanisi wake! Wewe utakuwa designer mbabaisha usichojua unachofanya! Na huo jamaa unaseyesema eti ametoa ''nice professinal analysis'' kaandika bla bla za wataalamu wa kiafrika wenye maneno meeeengi na marefu lakini output sifuri. Unapoanza mradi mkubwa kama huo unaanza na research ambayo itakupa majibu yote na mambo ya eti ''tu assume'' hayana nafasi. Huhitaji kusubiri mpaka mradi uanze kufanya kazi ili ujue kuwa input iliyotumika kwenye huu mradi ni kubwa sana na output itakuwa ndogo sana. Zilikuwepo njia nyingne za kutumia gharama ndogo na kupunguza msongamano kwa asilimia kubwa kabisa. Lakini kama kawaidia ya Afrika na waafrika hilo sio tatizo. Wewe kama unasubiri endelea kusubiri lakini wenye upeo walishajua matokeo hawahitaji kusubiri!
 
major mwendwa 13:15 14th May 2014 Elewa kuwa hii si barabara ya kwanza ,mbona zile zilizo pita
hatukulalamika Kwa sababu
tunajuwa zuri na baya.Huu mradi wa DART ni kioja tena ni scandali ya mwanzo wa karne hii ya 21 Tanzania.Tumeacha priority tumeamza na yasiyo na umuhimu.
 
Kam watu wataamua kupaki magari yao binafsi na kutumia public, then magari barabarani yatakuwa machache na hence folenmi itapungua.
I agree.

Ndugu yangu kwa bongo haitatokea watu wapaki magari yao binafsi na kutumia usafiri wa umma. Magari binafsi yanasaidia movement ya safari fupi fupi! Na katika hali ya kawaida BRT inahusika na main roads tu! Kwa mafno nipo mlimani city natka kwenda sinza nitapabda Darts? nitasubiria daladla za kuninginia? Natka kwenda mabibo sokoni nitatumia Dart au nitasubiria daladala? Kwa ufupi ni kwamba kuendana na hali ya Dar hakuna uwezekano kwamba watu wataacha kutumia magari yao binafsi.

By the way Dart itasabibisha msongamano mkubwa wa watu wanaomwagwa kwenye mabasi makubwa kwenye sehemu zile za kufaulishia kwenye daladala za kawaida. watu watakaomwagwa kimara kwa mfano watakuwa wengi kiasi kwamba daladala zinazowapeleka mbezi na kwingineko hazitaweza kuhimili wingi wa watu! Ukiachilia mbali ufinyu wa barabara ya kimara mbezi! Maana yake ni kwamba kuna uwezekano wa abiria kusubiria kimara kwa saa mbili na zaidi ili kupata gari ya kumsogeza mbele. kama sasa hivi wakati wa peak hours pale kimara abiria wa mbezi wanagombania daladala, je mibasi hiyo ya dart itakapokuwa inawamwaga hapo ikwa mamia kwa wakati mmoja itakuwaje?Na hii inaaply kwa sehemu zote mabasi ya dart yatakapokuwa yanaishia au kumwaga watu. Ndio maana tunasema kwamba Dart bila kuimarisha barabara nyingine ni kazi bure ni sawa na kutoa tatizo upande mmoja unalihamishsia upande mwingine! Ndio maana tunaquestion vipaumbele vya serikali katika kuubuni huu mradi!
 
Ndugu yangu kwa bongo haitatokea watu wapaki magari yao binafsi na kutumia usafiri wa umma. Magari binafsi yanasaidia movement ya safari fupi fupi! Na katika hali ya kawaida BRT inahusika na main roads tu! Kwa mafno nipo mlimani city natka kwenda sinza nitapabda Darts? nitasubiria daladla za kuninginia? Natka kwenda mabibo sokoni nitatumia Dart au nitasubiria daladala? Kwa ufupi ni kwamba kuendana na hali ya Dar hakuna uwezekano kwamba watu wataacha kutumia magari yao binafsi.

!
Ikumbukwe, hii ni awamu ya kwanza ya mradi.
Lengo ni kuweka katika bara bara zote za dDar.
Tuwe na subira kidogo jamani tuone kwa vitendo phase one kama itasaidia au laa.
 
Huhitaji kusubiri mpaka mradi uanze kufanya kazi ili ujue ufanisi wake! Wewe utakuwa designer mbabaisha usichojua unachofanya! Na huo jamaa unaseyesema eti ametoa ''nice professinal analysis'' kaandika bla bla za wataalamu wa kiafrika wenye maneno meeeengi na marefu lakini output sifuri. Unapoanza mradi mkubwa kama huo unaanza na research ambayo itakupa majibu yote na mambo ya eti ''tu assume'' hayana nafasi. Huhitaji kusubiri mpaka mradi uanze kufanya kazi ili ujue kuwa input iliyotumika kwenye huu mradi ni kubwa sana na output itakuwa ndogo sana. Zilikuwepo njia nyingne za kutumia gharama ndogo na kupunguza msongamano kwa asilimia kubwa kabisa. Lakini kama kawaidia ya Afrika na waafrika hilo sio tatizo. Wewe kama unasubiri endelea kusubiri lakini wenye upeo walishajua matokeo hawahitaji kusubiri!
Tuombe uzima ninatamani sana kuja kuyaona haya maneno mradi utakapo isha
 
major mwendwa 13:15 14th May 2014 Elewa kuwa hii si barabara ya kwanza ,mbona zile zilizo pita
hatukulalamika Kwa sababu
tunajuwa zuri na baya.Huu mradi wa DART ni kioja tena ni scandali ya mwanzo wa karne hii ya 21 Tanzania.Tumeacha priority tumeamza na yasiyo na umuhimu.
Mkuu mimi siongei 2015 si mbalii kile nitakacho kiona nitafananisha na kile tulichoahidiwa afu ndo tutwajibishana au kupongezana
 
Ikumbukwe, hii ni awamu ya kwanza ya mradi.
Lengo ni kuweka katika bara bara zote za dDar.
Tuwe na subira kidogo jamani tuone kwa vitendo phase one kama itasaidia au laa.

Yaani sijui kwanini tunashindwa kuelewana kuhusu sawla la priorities. Yaani kwamba tuemetoa kiapaumbele kwa jambo ambalo lilitakiwa lifanyike baadaya mengine kuwekwa sawa. mpaka huo mfumo wa barabara ukamilike si ni kama twenty years to come? Huku wananchi wakiendelea kuteseka wakti cheaper options zilikuwapo?
 
Mkuu ni kweli hii ni Kati ya miradi iliokosewa sana, katika nchi kama hii ambapo barabara hakuna, walitakiwa kujenga barabara angalau za 3lanes pamoja na overpass za kutosha. Wangeweza kuwa na motorway ambayo ni express ambayo inalipiwa kwenye toll booth ili kupita kwa wasio taka foleni. Kinachojengwa sasa hata kama mm sio engineer naona kabisa ni ufujaji wa fedha na ongezeko la foleni. Hv bwana mkubwa akisafiri huwa anaagalia nini? Au anajifinza nini? Maana haya ni mambo ambayo hata hapo kwa bwana uhuru tu yapo sio mpaka kwa malkia au kwa jaluo. Nchii hii hakuna uwajibwishaji kwa hivyo hakuna anaejali.
 
Yaani usubiri kitu kikamilike wakati failure inaonekana wazi? Barabara ya moro itatumikaje? malori humo humo, gari ndogo humo humo, halafu barabara nyembamba! halfu inaishia Kimara wakati mbezi siku hizi ina umati wa watu km ubungo au manzese! Watu watakoamwagwa hapo Kimara na hiyo mibasi wataendaje mbezi. Kutoka kimara mpaka mbezi tayari traffic jam ni kali sana kwa sababu ya malori, daladala na magari binafsi. Mradi wa kupunguza foleni unaongeza foleni!!!!

Wamekosea sana kuacha kupanua barBara toka Kimara.hadi Mbezi kwa Yusufu foleni haitapungua huko ubungo kisa nitokea Kimara hadi mbezi pamebana sana
 
Mkuu udasa99,
Kwanza kabisa ingawaje umesema hujaona michoro ya DART lakini ulichozungumza ndio hasa kilichopo kwenye mradi huu! Kwanza, tukianza na hilo suala la daladala, lengo sio kupunguza daladala bali kuziondoa kabisa... which means, mradi ukishaanza hapatakuwa tena na daladala kwenye barabara husika! Wamiliki wa daladala wenyewe wanalifahamu jambo hilo na wameshapewa elimu na nini wanatakiwa kufanya to go on with the business! Hawa wanatakiwa kuunda kampuni, kwa wale wasio na uwezo mkubwa, wanaweza ku-join force. Lengo ni kwamba, kampuni hizi nazo ziwe zina-operate through DART lakini sio kwa daladala bali kwa mabasi maalumu yanayokizi vigezo vya DART/BRT!

Kuhusu ratiba maalumu ya mabasi! Unless wakiuke matakwa ya BRT lakini ratiba maalumu lazima iwepo! Kama nilivyosema hapo awali, BRT ni system ambayo eneo fulani la dunia likitaka kutumia mfumo huo basi ni lazima wafuate standards za BRT duniani! Moja ya standard za BRT ni ratiba... kama kituoni unatakiwa kukaa dakika moja, haijalishi kama umepakia au hapana, kama dakika moja imeisha ni lazima uondoke coz' nyuma yao kutakuwa na gari lingine linakuja!

Je, itapunguza foleni? Hii itategemea sana na wananchi wenyewe! Kama ulivyosema, ikiwa watu wata-switch from using private cars to DART, basi foleni inaweza kupungua ingawaje, kama ulivyosema, watu ambao hivi sasa hawatumii Morogoro Rd wanaweza kuhamia na hivyo kutoonekana tofauti! Lakini hata kama watu hawata-opt kuacha magari yao nyumbani bado watakaoathirika ni wao na wale wa DART hawataathirika coz' DART roads ni only kwa mabasi ya DART na hivyo kuondoa uwezekano wa msongamano ambao leo hii unasababishwa na daladala kusimama popote, malori, kupigana bao, kuchomekeana n.k!!

Hilo la Magufuri, si tu kwamba Magufuri ni mwanasiasa lakini pia mradi huu haupo chini ya Wizara ya Ujenzi! Kumbukumbu zimenitoka lakini kama haupo chini ya TAMISEMI basi itakuwa City Council kwa sababu, kimsingi huu si mradi wa barabara bali mradi wa mabasi yaendayo haraka!

Huu mradi una potential kubwa sana. Mpaka sasa umepitia vizingiti vingi lakini unaonekana unaendelea kuisha na kufanikiwa. For full disclosure, sifanyi kazi kwenye huo mradi wala sijawahi kuajiriwa na consulting or construction company yeyote inayojihusisha na mradi ila huu ni mradi wetu watanzania inatubidi tuchangie mawazo ya kuufanya uwe successful na kama ikiwezekana tuwekeze whether ni kwenye mabasi wakiruhusu kuuza shares au kwa jinsi yeyote ile. It is one of the flagship projects Africa japo wengi hapa jamvini wamekuwa negative kwa sababu ni mradi wa gharama. Investments kama hizi sio cheap. Nashauri uongozi wa Jamiiforums u organize tour kwenda kwenye ofisi za mradi ili wenye maswali, maoni, dukuduku, na hoja wazitoe kwa wahusika. Natumaini maswali mengi yatapata majibu.
 
Heshima mbele wakuu : kuhusu mfano abiria wanaotoka/kuingia kwenye mabasi ya BRT! Rule No. 1 hakuna Bus la Abiria litarusiwa ku-cross/katisha juu ya BRT lines. Mfano abiria wa Bunju-Tegeta to G/mboto au Mbagala watalazimika kushuka UBT main stand kisha kuvuka kwa mguu kupanda jingine lililopo upande mwingine hivyo hivyo kwa wale wa G/mboto au Mbagala kwenda Bunju
 
Back
Top Bottom