RE/MAX Coastal, Coral Property zazindua mradi wa nyumba za gharama nafuu jijini Dar

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
398
648
Katika mpango unaolenga kuunga mkono juhudi serikali za kuhakikisha kunakuweko na nyumba za makazi bei, kampuni ya ya RE/MAX na ile ya Coral Property zimezindua mradi wa nyumba mpya za bei nafuu wa Sky Royal, mtaa wa Morocco Jijini Dar es Salaam.
IMG-20240506-WA0005.jpg

Waziri wa Ardhi. Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. Jerry Slaa (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua rasmi mradi wa nyumba kwa bei nafuu wa Sky Royal Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hainan International Ltd Bw. Zhou Tao, Mkurugenzi wa Ardhi wizarani, Upendo Matotola na Mkurugenzi Mkuu wa Coral Property Co.Ltd Bw. Li Jun

Hafla hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali katika sekta ya nyumba, ambapo pamoja na mambo mengine, uzinduzi huo ulionyesha dhamira ya dhati ya ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi unaolenga kuwapatia watu makazi ya bei nafuu na yenye ubora wa hali ya juu.

Akizindua mradi huo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Jerry Slaa, aliyapongeza makampuni hayo mawili kwa mpango huo ambao alisema umekuja wakati mufaka haswa ikitiliwa maanani ongezeko la uhitaji wa nyumba za makazi Jijini Dar es Salaam.

"Ujenzi wa nyumba za bei nafuu ni muhimu sana hapa nchini; uamuzi wa kampuni hizi mbili wa kujenga nyumba bora ni mfano bora w akuigwa na taasisi nyingine hapa nchini ili kukabiliana na changamoto inayohusiana na mahitjai ya nyumba bora za makazi”, alisema.
IMG-20240506-WA0006.jpg

Waziri Silaa aliendelea kusema kuwa, hatua zilizochukuliwa na makampuni hayo mawili zinaunga juhudi za Serikali zinazolenga uweko wa nyumba bora za makazi na za gharama nafuu kwa wananchi hapa nchini.

"Nichukue fursa hii kutoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hii ya uweko wa nyumba nzuri za makazi; ni matumaini yangu kuwa uwekezaji wa nyumbanzuri za makazi katika soko kutaiwezesha Serikali kufikia azma yake ya uweko w anyumba nzuri za makazi hapa nchini”, alisema.

Waziri Silaa alitoa wito kwa makampuni ya RE/MAX Coastal na Coral Property kujiongeza na kupanua panua wigo wa uwekezji wao kwa kuwekeza maeneo mengine hapa nchini ikiwemo Jijini Dodoma ambapo alisema idadi ya watu inakuwa ikongezeka kila siku na hivyo kusababisha ongezeko la mahitaji ya nyumba za makazi na zenye gharama nafuu.

Tukio hilo mbali na kuwa la uzinduzi, pia lilitoa fursa ya washiriki kuona fursa za uwekezaji mzuri na wa uhakika unaliofanywa na makampuni hayo.
IMG-20240506-WA0007.jpg

"Washiriki watapata fursa ya kujionea wenyewe uwekezaji unaohusu nyumba zenye chumba kimoja, viwili na hata vitatu, ambazo zinagharimu kati ya dola za Marekani 81,186, USD 147,427, na USD 191,838 mtawalia; zaidi ya hayo, wawekezaji hao watatoa punguzo la asilimia 8 ya bei ya kila nyumba kama ilivyoorodheshwa, ambapo pounguzo hilo litahusu siku ya uzinduzi tu”, ilisema taarifa ya pamoja iliyotolewa na uongozi wa makampuni hayo mawili.

Akiongea ktia hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Coral property Holdings Bw. Li Jun, alisema, “Uwekezaji huu umelenga kuunga mkono juhudi za Serikali zinazolenga kuhakikisha kunakuwa na nyumba nzuri za makazi na zenye bei nafuu; kupitia ,iradi ya maendeleo kama vile Sky Royal, pia tunalenga si kuwekeza kwenye nyumba tu, bali pia kuhakikisha wananchi wanakuwa na maisha endelevu, yenye ufanisi na ambayo yatachangia ustawi wa familia kwa ajili ya Watanzania.”

Alisema kampuni yake pia imejikita katika kuhifadhi na kulinda mazingira nakwamba mpango huo ni endelevu. Aidha alisema mradi huo wa Sky Royal unahusu mpango kabambe wa kiteknolojia unaolenga uwekezji wa nyumba bora unaohakikisha mazingira rafiki na kwamba mradi huo umeidhinishwa kituo cha uwekezaji nchini TIC.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kanda wa kampuni ya RE/MAX Pwani, Bw. James Prevost, alisema, “Ushirikiano wetu wa kampuni ya Coral Property Holdings hususan katika mradi huu wa Sky Royal, umetuwezesha kuwapatia wananchi Jijini Dar es Salaam maisha bora kupitia nyumba nzuri za makazi na zenye unafuu; punguzo la bei siku hii ya uzinduzi pia ni wito kwa wateja kunufaika na uwekezji wa huu mzuri”.

Alisema mradi wa Sky Royal haulengi uwekezaji wa nyumba za makazi tu, bali pia ni kielelezo cha uwekezaji wa nyumba nzuri na za uhakika ambao unalenga kutoa makazi mazuri na endelevu kwa wananchi na kwa bei nafuu.

"Eneo la kimkakati la maendeleo na huduma kamili kwa jamii, inalenga kutengeneza mazingira bora kwa wataalamu wa aina malimbali wakiwemo vijana, kwa wanafamilia na wamiliki wa biashara aina mablimbali," alisema.

Kampuni ya RE/MAX Coastal inasifika kwa utaalamu wake katika maswala ya mauzo na masoko ya majengo, ikiwa na dhamira ya kuwapatia wateja kilicho bora na chenye thamani kulingana na soko lililoko nchini Tanzania.

Kwa upande wake, kampuni ya Coral Property Holdings imekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza uwekezaji wa uhakika wa majengo aina mbalimbali ikiwemo nyumba bora za makazi huku ikizingatia ubunifu wa hali ya juu na endelevu sambamba na ubora hali ya juu katika kuhakikisha kunakuweko na suluhisho la uhakika katika sekta ya makazi nchini Tanzania.

Ushirikiano kati ya RE/MAX Coastal na Coral Property Holdings kwenye uzinduzi wa mradi wa Sky Royal ni juhudi za kihistoria zinazolenga kuimarisha mandhari ya jiji la Dar es Salaam.

Kwa kuoanisha malengo yao sambamba na ile ajenda ya Taifa inayolenga kuhakikisha uweko wa makazi bora, kampuni zote mbili zimedhamiria kuimarisha sekta ya ujenzi hususan ujenzi wa majengo aina mbalimbali kwa lengo la kustawisha maisha ya Watanzania wote kwa ujumla.
 
Mbona nzuri hivyo, yaani zinapendeza kiulayaulaya.
 
Nyumba ya chumba kimoja, viwili, n vitatu.

Bei ndio dola 80k, dola 147k na 190k

Yaani chuma kimoja nikanunue kwa zaidi ya milioni 180!¡ 😳 au macho yangu hayajaona vizuri.
 
Usd 81k 147k na 190k chumba kimoja, viwili na vitatu.. Hapo iliyo nyumba iko eneo mitaza mraba kiasi gani?.
Hovyo kabisa
 
...kampuni zote mbili zimedhamiria kuimarisha sekta ya ujenzi hususan ujenzi wa majengo aina mbalimbali kwa lengo la kustawisha maisha ya Watanzania wote kwa ujumla.
Kustawisha maisha ya Watanzania wote?!
Picha tafadhali
 
Nyumba ya chumba kimoja, viwili, n vitatu.

Bei ndio dola 80k, dola 147k na 190k

Yaani chuma kimoja nikanunue kwa zaidi ya milioni 180!¡ 😳 au macho yangu hayajaona vizuri.
Halafu sasa hizo possibly zitakuwa ni apartments. Hiyo ya chumba kimoja ya dola 80K ukijenga mwenyewe unatoa kitu kikali tena nyumba inayojitegemea. In the other hand, Bongo mitaani nyumba zenye sifa ya kuitwa nyumba ni chache sana. Wengi wameunganisha matofali na kufanya finishing lakini hakuna ufundi.
 
Back
Top Bottom