Hivi mkeo huwa anachukulia vipi unapokuwa katika kipindi kigumu cha kukosa fedha?

Wanawake ambao kutwa kukucha eti siwezi kumlea mwanaume mimi,ila mume yeye anakulea na kukuvisha bila kuchoka miaka yote ila akipata majanga kiuchumi unamgeukia hivi mtu wa aina hii akitoa hela yake alishe familia week tu sindio na deki utapigishwa kabisa?

Sijajua.
 
Mume mtamu jamani.

Akiwa na stress mliwaze na msaidie majukumu yake pale unapoweza.

Mpe hope kwamba mambo yatakaa Sawa tu.

Believe in him, pray for him.
Mke wangu yuko na hii tabia kama hatabadilika hapo baadae
 
Pesa ni sabuni ya roho kibao chake Aziz Abdi na Orchestra Benga Africa
hapo inabidi uvumilie kununiwa
 
saa zingine wamama inabidi waelewe utafutaji mgumu unahitaji maombi na uvumilivu siyo kutukalia kooni kama sisi ni wahaini sana
pesa siyo mkodombwe kwamba kila mtu anayo ipo tofauti jama
 
Sio mke ila ni mchumba, nilikwama kidgo kwenye biashara zangu japo ni ndogo bado nipata loss, alinipa kiasi cha fedha na wala ajanidai hadi sasa yapata miezi minne N.B pesa alizonisaidia ni ndogo mnoo kulinganisha ambazo mimi nimempatia.
yani kama mkeka bana 🤣 🤣
 
Ila na mimi....
kelphin kepph hii kitu inaitwa Pesa inaharibu sana ndoa...cha muhimu ni kuhakikisha mume na mke muwe same team inapokuja suala la mapato na matumizi kwenye familia....

Sio ile ya mimi zangu na wewe zako....mkijiwekea hela ni zenu wote, hata siku mkiishiwa...mtakuwa wawili kwenye Stress na mtafarijiana jinsi ya kutoka huko....

Tatizo linakuja wengi wetu hatupendi kuunganisha vipato vyetu, kugawana majukumu na bila kusahau kuongelea jinsi ya kusaidiana kujiendeleza huko mbeleni.
Tatizo la kina mama wengi pesa ya mme ni yenu wote, na ya mke ni yake mwenyewe na hapo ndio uchungu unaanzia 🤣 🤣 🤣
 
Habari wakuu.

Unapokuwa katika kipindi kigumu cha kukosa pesa mkeo nyumbani uwa anakutazama vipi huwa anaikubali hiyo hali mnaishi nayo au ndo mtu wa kuzila na kukusanya vilago kama huyu wa kwangu make naona subira yake ipo kwenye vingine sio pesa.

Hebu tupe mtazamo kwa huyo wa kwako.
Pole sana, huyo sio mke, na sio kila mwanamke ni mke, mke ni yule ambae mnasimama pamoja katika vipindi vyote vya maisha bila kujali, ndio maana hata kiapo cha ndo kinasema wazi kwamba mtakua pamoja kwa shida na raha, magonjwa dhiki na tabu

Ukiona mwanamke hawezi kuheshimu hayo maneno ya kiapo cha ndo basi hapo umepigwa pakubwaa
 
Mwanamke naye anatakiwa awe na balance ya mahitaji yake madogomadogo na siyo kulialia njaa tu kila wakati.
 
Ndicho kipindi mwanaume huwa anatakiwa kuchaguwa katika mambo matatu ili kunusuru maisha yake.

1/ achaguwe kuvumilia mateso na dhihaka za mkewe ili akifa aende mbinguni Kwa uvumilivu alioufanya.

2/aamue kuwa na mchepuko ili ndoa iweze kudumu.

3/aamue kuachana na mkewe ili kulinda heshima yake.

Hii ikikutokea ukiwa na umri chini ya 35 huwezi kuelewa, ila ikikukuta ukiwa na umri wa zaidi ya miaka 45 ndipo utaelewa kwa nini wanaume hufa haraka kuliko wanawake kwenye ndoa.
 
Back
Top Bottom