Hivi mbona sioni raha ya hii dunia?

Hivi mbona sioni raha ya hii dunia?

Joined
Nov 30, 2022
Posts
27
Reaction score
18
"Nilpokua mdogo nilipambana sana kusoma na kufanya kazi mbalimbali nikiaminishwa kua nikiwa mkubwa nitakua na msingi bora wa maisha."

"Nimesoma sana, tena ngazi zote za elimu namaanisha hadi degree level, na kufanikiwa kuwa katika taasisi moja ya selikarini japo mshahara sio mkubwa ila kiasi flani unatosha kunywea soda."

"Shida inakuja, sioni raha yoyote ambayo niliitegemea nitaipata before, nimekua sio mzuri wa
 
Ndo madhara ya kujua mambo mengi we si unajidai kipanga genius ukajaribu madudu yote vilevi vyote ukanyonya sehemu zote ukabet kila aina ya option [emoji1787][emoji1787] sasa umebakiza kutest kifo kipoje pole yako
 
Jicheki wewe mwenyewe tabia na mwenendo wako wa maisha, sisi wengine kutupa uhai na afya tunamshukuru sana Mola wetu na hatuna mshahara wa kunwyea soda kama wewe, nyie uwe unaridhika mambo mengine ulio pewa.
 
Ndo madhara ya kujua mambo mengi we si unajidai kipanga genius ukajaribu madudu yote vilevi vyote ukanyonya sehemu zote ukabet kila aina ya option [emoji1787][emoji1787] sasa umebakiza kutest kifo kipoje pole yako
Ww jamaa sio mtu mzuri aiseh
 
Dunia haiwezi kukupa vyote raha ya dunia unayo sana ila hujaizingatia tu.

Siyo mgonjwa,kazi unayo unapumua na huna ulemavu wowote vaa viatu vya wagonjwa,wale wanaokimbizana na migambo katikati ya miji wakitafuta kula yao kisa wanaonekana wachafuzi wa mazingira wapo wenye elimu sawa na wewe hawajapata hata pa kujitolea ili waonekane wapewe ajira,waza pia mtu ambaye sasa hivi yupo kwenye kitanda cha mauti akiivuta pumzi yake ya mwisho.

Ni vitu vingi itoshe kusema tenga muda kushukuru ulipofikia usikae kutafuta kujua vitu vilivyo nje ya uwezo wako.
 
"Nilpokua mdogo nilipambana sana kusoma na kufanya kazi mbalimbali nikiaminishwa kua nikiwa mkubwa nitakua na msingi bora wa maisha."

"Nimesoma sana, tena ngazi zote za elimu namaanisha hadi degree level, na kufanikiwa kuwa katika taasisi moja ya selikarini japo mshahara sio mkubwa ila kiasi flani unatosha kunywea soda."

"Shida inakuja, sioni raha yoyote ambayo niliitegemea nitaipata before, nimekua sio mzuri wa
Walikudanganya hao nduguzo hapo awali.Duniani ni mateso kwenda "mbere"!Ukitaka starehe,tenga muda wako na "ujifurahishe"!Usitarajie kuletewa furaha viganjani mwako.
 
Dunia haiwezi kukupa vyote raha ya dunia unayo sana ila hujaizingatia tu.

Siyo mgonjwa,kazi unayo unapumua na huna ulemavu wowote vaa viatu vya wagonjwa,wale wanaokimbizana na migambo katikati ya miji wakitafuta kula yao kisa wanaonekana wachafuzi wa mazingira wapo wenye elimu sawa na wewe hawajapata hata pa kujitolea ili waonekane wapewe ajira,waza pia mtu ambaye sasa hivi yupo kwenye kitanda cha mauti akiivuta pumzi yake ya mwisho.

Ni vitu vingi itoshe kusema tenga muda kushukuru ulipofikia usikae kutafuta kujua vitu vilivyo nje ya uwezo wako.
Kidogo nimekupata japo sio sana
 
Mhubiri 1:2‭-‬18 SUV

Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua? Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake. Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena. Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia. Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua. Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi. Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye. Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu. Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo. Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki. Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa. Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kujilisha upepo. Yaani, Katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni; Naye aongezaye maarifa huongeza masikitiko.

Usipomjua Mungu na Yesu Kristo mwana wake hakika hutaweza kuifikia furaha ya kweli. Mkiri Yesu uanze kuishi kwa Roho hapo neema zitatiririka kwako
 
Kwakuwa umejiita kipanga basi inaashiria una akili mingi, ishathibitishwa kadri unavyojua mengi ndo huzuni inavyozidi, ignorance is bliss 🥴
 
Bila shaka wewe ni mvivu,kuna wengine hata kwenda tu msibani anaona anateseka na hakuna raha duniani
 
"Nilpokua mdogo nilipambana sana kusoma na kufanya kazi mbalimbali nikiaminishwa kua nikiwa mkubwa nitakua na msingi bora wa maisha."

"Nimesoma sana, tena ngazi zote za elimu namaanisha hadi degree level, na kufanikiwa kuwa katika taasisi moja ya selikarini japo mshahara sio mkubwa ila kiasi flani unatosha kunywea soda."

"Shida inakuja, sioni raha yoyote ambayo niliitegemea nitaipata before, nimekua sio mzuri wa
Una shida ya afya ya akili muone mtaalam
 
Duniani ni kuteseka tu bro, mwana wa Mungu mwenyewe alivyokuja duniani aliteseka. Subiri ufe ndio "upumzike kwa amani" maana hata pumziko la duniani bado mateso tu!
 
Kuna nafasi huwa haijazwi na elimu Wala kitu kingine chochote ila kile ulichozaliwa uje kukifanya na hapo ndipo ulipo moyo wako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom