Hivi mbona sioni raha ya hii dunia?

Hivi mbona sioni raha ya hii dunia?

🤣🤣🤣🤣 kuna jamaa mmoja humu aliwakuja na hii nadharia .

" Watu woteeeeee tuliomo kwenyee hii dunia ni wafungwa , yan dunia ni gereza na sisi binadamu wotee pamoja na viumbe vingine vyote vilivyomo duniani ni wafungwa ni vile tu tumetolewa kumbumbuku zetu za huko tulipo kuwa awali na hatukumbuki hasa ni makosa gani yalipelekea tujaja kwenye hili gereza (dunia) , kwamba tupo humu kutimiza muda wa vifungo vyetu na hatimae tutarudi zetu huko tulikokuwa awali .

Hivyo huwezi kupata furaha ukiwa gerezani hivyo vyote ulivyofanya kama sijui kusoma sanaa na utakavyofanya vitakusaidia tu just to kill time ukisubilia muda wako wa kifungo uishe uondoke zako.
 
"Nilpokua mdogo nilipambana sana kusoma na kufanya kazi mbalimbali nikiaminishwa kua nikiwa mkubwa nitakua na msingi bora wa maisha."

"Nimesoma sana, tena ngazi zote za elimu namaanisha hadi degree level, na kufanikiwa kuwa katika taasisi moja ya selikarini japo mshahara sio mkubwa ila kiasi flani unatosha kunywea soda."

"Shida inakuja, sioni raha yoyote ambayo niliitegemea nitaipata before, nimekua sio mzuri wa
Asikudanganye mtu. Kuwa na pesa, mali na elimu ya juu sio kigezo cha kuwa na furaha.

Hata akina Bill Gates, Elon Musk, Jack Ma nk licha ya mapesa waliyonayo lakini hawana furaha hata kidogo.

Kuna kipindi malkia Elizabeth enzi za uhai wake aliwahi kusikika akisema hana furaha.

Mfalme Suleiman, ndiye mfalme pekee tajiri kupita wote waliowahi kuishi duniani. Tena ndiye mfalme pekee aliyeoa wanawake zaidi ya 1000 lakini bado alisema hana furaha.

Wewe nani uwe na furaha hapa duniani? Hata sisi tunaojaribu kuzishika Amri za MUNGU bado hatuna FURAHA maana katika ulimwengu huu tunayo dhiki, lakini, tunajipa moyo kwakuwa KRISTO BWANA wetu ameushinda ulimwengu. (YOHANA 16:33)
 
"Nilpokua mdogo nilipambana
Raha jipe mwenyewe ndugu, Ukisubiria raha ije yenyewe haiji, baada ya majukumu yako serikalini fikiria nin unakipenda nenda kakifanye ujipatie furaha, kama ni kunywa kanywe kwa kiasi, kama ni kusoma kasome sana, kama ni kucheza kacheze utakavyo, as long unajua ukikifanya iko kitu utapata furaha basi kakifanye baada ya majukumu yako ya kukupatia ugali mezani.
 
Mhubiri 1:2‭-‬18 SUV

Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua? Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima. Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake. Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake. Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena. Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia. Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua. Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi. Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye. Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu. Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake. Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo. Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa, Wala yasiyokuwapo hayahesabiki. Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa. Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kujilisha upepo. Yaani, Katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni; Naye aongezaye maarifa huongeza masikitiko.

Usipomjua Mungu na Yesu Kristo mwana wake hakika hutaweza kuifikia furaha ya kweli. Mkiri Yesu uanze kuishi kwa Roho hapo neema zitatiririka kwako
Andiko katika Qur-an, surat "Asri"
1)Naapa kwa jioni ya Alasri
2)hakika mwanaadam yumo hasarani
3)Isipokuwa wale ambao wameamin wakasimamisha sala,wakahimizana kushikamana na Haki na wakahimizana kuwa na Subira.
Maelezo binafsi- hapa inaonekana mwanaadamu hakuandaliwa kufaidi Starehe au Raha za Dunia na badala yake niyeye mwenyewe anaetakiwa kuzitafuta na kufaidika nazo kwa kufuata muongozo huu aliopewa >
Kumuabudu M/ungu,kutenda haki na kuwa na Subira.
Na andiko jingine kwenye Qur-an
1)M/mungu anasema>hakika tumemuumba mwanaamu katika hali nzuri kabisa
2)kisha tukamrejesha chini ya waliochini(tukamshusha thamani)
3)Isipokuwa wale ambao wameamini wakasimamisha sala wao wanamalipo mema yasiyo na mwisho.
Maelezo binafsi-katika hili na tujilinganishe sisi binaadam na viumbe wengine, ni dhahiri mwanaamu ni bora kwa maumbile na maarifa kuwazidi wanyama,wadudu na viumbe wengine wote ulimwenguni lakini ni sisi binaadamu tunaotaabika zaidi kwa ajili ya maisha, tunapambana kila siku na kwakila hitaji ili kujitimizia haja zetu wakati viumbe wengine maisha yao ni mteremko kabisa.
Nb:kwa upande wa maelezo binafsi nakubali kusahihishwa.
 
Andiko katika Qur-an, surat "Asri"
1)Naapa kwa jioni ya Alasri
2)hakika mwanaadam yumo hasarani
3)Isipokuwa wale ambao wameamin wakasimamisha sala,wakahimizana kushikamana na Haki na wakahimizana kuwa na Subira.
Maelezo binafsi- hapa inaoneka mwanaadamu hakuandaliwa kufaidi Starehe au Raha za Dunia na badala yake niyeye mwenyewe anaetakiwa kuzitafuta na kufaidika nazo kwa kufuata muongozo huu aliopewa >
Kumuabudu M/ungu,kutenda haki na kuwa na Subira.
Na andiko jingine kwenye Qur-an
1)M/mungu anasema>hakika tumemuumba mwanaamu katika hali nzuri kabisa
2)kisha tukamrejesha chini ya waliochini(tukamshusha thamani)
3)Isipokuwa wale ambao wameamini wakasimamisha sala wao wanamalipo mema yasiyo na mwisho.
Maelezo binafsi-katika hili na tujilingsanishe sisi binaadam na viumbe wengine, ni dhahiri mwanaamu ni bora kwa maumbike na maarifa kuwazidi wanyama,wadudu na viumbe wengine wote ulimwenguni lakini ni sisi binaadamu tunaotaabika zaidi kwa ajili ya maisha, tunapambana kila siku na kwakila hitaji ili kujitimizia haja zetu wakati viumbe wengine maisha yao ni mteremko kabisa.
Nb:kwa upande wa maelezo binafsi nakubali kusahihishwa.
Umeandika vyema ndugu kwa mujibu wa kitabu ulicho na maarifa nacho.

Sikuweka maelezo binafsi ya kitabu hicho cha mhubiri ila naona ni vyema nifanye hivyo kuwafaa watakao hitaji maarifa haya.

Muhtasari
Mwandishi wa kitabu cha mhubiri ni Sulemani mwana wa Daudi miongoni mwa binadamu waliokuwa na utajiri na hekima nyingi sana katika ulimwengu huu.
Mhubiri 2:7,9
Nami nikanunua watumwa na wajakazi, nikawa na wazalia nyumbani mwangu; tena nikawa na mali nyingi za ng’ombe na kondoo, kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; pia hekima yangu nikakaa nayo.
Kitabu cha mhubiri kimeandikwa kwa mtindo wa dhihaka mwandishi akidhihaki kila aina ya juhudi mwanadamu anayoitafuta hapa duniani kuwa ni kazi bure.
Mwandishi kadiri ya historia na uhalisia wake alikuwa na vyote tunavyovitamani kibinadamu amejaribu kila uzuri na anasa ambazo hata leo wengi wa wasio ijua kweli ya Kristo wanakimbizana navyo.
Niweke baadhi ya nukuu za mwandishi mwenyewe
Mhu 2:1‭-‬3‭, ‬8
Nikauambia moyo wangu, Haya, nitakujaribu kwa njia ya furaha basi ujifurahishe kwa anasa. Na tazama, hayo nayo yakawa ubatili. Nikasema juu ya kicheko, Ni wazimu; na juu ya furaha, Yafaa nini? Moyoni mwangu nikapeleleza jinsi ya kuuburudisha mwili kwa mvinyo, na (moyo wangu ukali ukiniongoza kwa hekima) jinsi ya kushikana na upumbavu, hata niyaone yaliyo mema ya kuwafaa wanadamu, ili wayafanye hayo chini ya mbingu siku zote za maisha yao. tena nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na za kutoka katika majimbo. Nikajipatia waimbaji, waume kwa wake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana.
Kumbe vile tunatafuta wanawake wengi au machawa/wapambe na fahari nyinginezo za dunia bado hazifaidi kitu kwani kiu ya nafsi ya mwanadamu haiwezi kutulia bila ya kujishikamanisha na Mungu.

Mhu 6:1‭-‬6‭, ‬12
Kuna baa nililoliona mimi chini ya jua, nalo linawalemea wanadamu kwa uzito; mtu aliyepewa na Mungu mali, ukwasi, na heshima, hata asipungukiwe na kitu cho chote kwa nafsi yake, katika yote anayoyatamani walakini Mungu hamwezeshi kula katika hizo; bali mgeni hula. Hayo ndiyo ubatili hasa, nayo ni ugonjwa mbaya. Mtu akizaa watoto mia, akaishi miaka mingi, nazo siku za maisha yake ni nyingi, lakini nafsi yake haikushiba mema; tena ikiwa, zaidi ya hayo, amekosa maziko; mimi nasema, Heri mimba iliyoharibika kuliko huyo; yaani, hiyo huja katika ubatili, na huenda gizani, nalo jina lake limefunikwa giza; tena, haikuliona jua wala kulifahamu; basi, hii imepata kustarehe kuliko yule; naam, ajapoishi miaka elfu mara mbili, asijiburudishe kwa mema; je! Wote hawaendi mahali pamoja? Kwa maana ni nani ajuaye yaliyo mema ya mwanadamu katika maisha yake, siku zote za maisha yake ya ubatili, anayoishi kama kivuli? Kwa maana ni nani awezaye kumweleza mwanadamu mambo yatakayofuata baada yake chini ya jua?
kimsingi maisha ya mwanadamu pasipo kumpata Mungu ni mbio zisizo na mwisho. Yote yanayotafutwa kutii haja za mwili ni mambo ya maumivu maana hayaleti ukamilifu ndani yake. Wengi wa watu duniani hawajui kusudi la Yesu kuja duniani kwani wengi wanamfungamanisha Yesu Kristo na dini fulani fulani kitu ambacho sio sahihi. Yesu amekuja duniani kuurejesha utukufu wa mwanadamu uliopotea katika bustani ya edeni. Mwanadamu ni mtawala wa dunia yaafa asishughulikie mambo madogo madogo kama kuwaza kula na kunywa kwa sababu ya ukuu wake. Jawabu alilolitoa Yesu kwenye ubatili wa maisha ndilo hilohilo Sulemani anahitimisha nalo
Mhu 12:13
Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Yesu Kristo yeye alivyolizwa juu ya maisha haya ndio majibu yake.
Mt 6:25‭-‬34
Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

aliyeandika uzi huu ni miongoni wa wengi ambao bado hawajamtambua Kristo na nguvu zake maana kwake ndipo ulipo utimilifu wa maisha. Pindi mtu apatapo neema ya kumvaa Yesu kwelikweli hakika anapata vyote mwanadamu avitamanivyo ndani ya dunia hii. Lazima ieleweke furaha ya roho ni kuishi ukijua upo kwenye tumaini la umilele maana tumeumbwa katika kutafuta utimilifu huo. Bahati mbaya wengi wanakwama kwenye udini ambayo ni ngazi katika kuutafuta ufalme wa Mungu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom