Hivi mbona CCM wako kimya mpaka sasa?

Hivi mbona CCM wako kimya mpaka sasa?

Tatizo la kukatwa kwa umeme litaligharimu sana CCM. Hapa Mwanza umeme ulikatwa saa 1.00 asubuhi na kurudishwa saa 4.00 usiku. Katika vijiwe watu wanalaani sana na wanasema ni tatizo la EL kuhamia CHADEMA. Ikumbukwe umeme ndiyo kila kitu kuanzia mashine za kusaga, viwanda, saloon, stationey n.k. bila umeme ni tatizo. Wananchi uamuzi ni tarehe 25.10.2015.
 
Huyu Mzee anataka sifa

Tena sifa za kitoto ambazo ameshauriwa na watoto hivyo hawezi kupata lolote zaidi ya kuendelea kutumia pesaaaaaa nasi tutazipokea na kuzitafuna. Alishindwa kuwarubuni wanaccm,sasa kafanikiwa kwetu. Karibu baba yetu. Mgeni njoo mwenyeji apone kwani tulikuwa na njaa mwaka huu.
 
Tokea siku ya Jumatatu pale ambapo makao makuu ya CCM mtaa wa Lumumba walipewa taarifa za mhshimiwa Lowasa kuhama chama na kutimkia UKAWA.

Kwa kuwa vijana wa masuala ya propaganda chini ya katibu mwenezi Nape Mnauye walidhani ulikuwa utani au masihara wakapuuzia onyo hilo sasa imekuwa ngumu kutoa taarifa ya kupokea uamuzi huo.

Katika ulimweigu wa sasa wanasiasa nao wakiwa kama binadamu wengine nao wana utashi na moja ya matunda ya utashi huo ni kuweza kufanyamaamuzi na kuyatakeleza.

Pia katika nchi mbalimbali duniani vyma vya siasa vinakuwa na washauri wao ambao moja ya kazi zao ni kujaribu kuoanisha taarifa zinazopishana kuhusu sera, itikadi na suala Zima la mbinu na mikakati.

Lakini Chama cha Mapinduzi wamekuwa kimya hata baada ya kuona kwenye mitandao kwamba Tumaini Makene, mkuu G Sam na wengine walikuwa wakifanya kazi usiku na mchana, na Nape Nnauye akawa hajajiandaa angalu kujibu uamuzi huo wa mzee Lowasa kuhama CCM.

CCM si chama lelemama na kipo kinatawala nchi hii tangia ilipokuwa TAA, TANU hadi CCM ilozaliwa tarehe 5 mwezi wa 7 mwaka 1977.

CCM mtaa wa Lumumba vipi mmekaa kimya au Nape Nnauye bado ametahayari?

CCM mtaa wa Lumumba isiwaache vijana wasofahamu siasa kuja jamii forums kujaza taarifa za kizushi kuhusu UKAWA na Dr Slaa, au mjinga mmoja anakuja na kichwa cha habari kinachosema Dr Slaa is dead!.

"Spin Doctors" wa CCM wapo wapi?

Mkuu kumbe umeliona hilo,naona ccm kwa sasa inabidi wajipange vema kusudi wakija waje na tamko lenye mashiko kwa wanachama wao kwani wakikurupuka ndio watazidisha petrol kwenye msitu unaoteketea kwa moto
 
mkuuu wewe jidanganye tuu hakuna kazi nzuri ambayo chadema wameifanya kama ya kuhamasisha vijana aiseee.ukitaka kulijua hili kama ulishiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakuwa ushajua nn na maanisha.

na kama utakuwa umetembelea kwenye vituo vya kupigia kura hakika pia utakuwa ushapata jibu.

vijana wana mwamko sana siku hizi.

Je na matokeo yake yalikuwaje?
 
Richard,
Binafsi katika mambo ambayo siku nyingi nilijua yanakipeleka kuzimu CCM ni kufa kwa idara ya Propaganda,au kukua kwa Propaganda machine ya Chadema,kiasi kwamba ika-counter ile ya CCM. Maana miaka ya nyuma CCM walikuwa wanaweza kuaminisha uma kuwa Majambia haya yenye rangi nyekundu ni na blue ni ya CUF,au Chadema ni chama cha dola ya KIchaga,na Ikaaminika..na wananchi wakakipigia ccm kula,ikawa jioni,aikawa asubuhi,miaka mitano ,kumi,...adfinitum!

Jambo la kushukuru ni elimu ya uraia kwa wananchi,hizo shule za kata kwani hawa vijana waliomaliza elimu ya form four na wengine ambao wanaendela kusoma wamekuwa walimu wazuri kwa ndugu na wazazi wao huko vijijini
 
Last edited by a moderator:
Siasa za Tanzania ni ngumu sana, unaweza kushangaa kibao kikawageukia UKAWA ghafla na wao wakawa mabubu kama LUMUMBA hivi sasa.

Jambo hilo sahau kwa sasa kwani ni hao hao ukawa ndio wameifikisha hapa ccm ilipo,kwahiyo ukawa cdm wapo kimkakati muda wote.
 
Salaam Watanzania,

Nathani kuna thred nyingi sana za Mh.Lowassa toka atoke CCM na hata wakati wa uchaguzi ndani ya chama cha ccm.
Lakini kwa ufupi ningependa kuongelea ni jinsi gani ujasiri wa lowassa uliyoadimu kwetu watanzania na hasa sisi vijana kwa taifa la leo.

Asikudanganye mtu,maamuzi ya leo ndio matokeo ya kesho.Uamuzi wa lowassa uliwacha wanasiasa wengi midomo wazi na hasa watanzania kwa udhubutu wake kuondoka ndani ya chama alichokuwa kwa zaidi ya miaka 30.Huu hata mimi leo naamini haukuwa uwamuzi wa haraka na wala wa kukurupuka.Lakini pamoja na lowassa kutoka CCM kwa jambo lolote lile,uthubutu wake unatisha na unatia moyo kwamba watanzania wote tunaweza kuthubutu na kuamua maamuzi magumu.Lowassa ameonyesha kwamba inawezeka.CCM huwa wana maneno yao kwamba bila CCM,nchi itayumba;hii ni thana potofu na isiyo na ukweli wa nusu.

Kwa mantiki hiyo basi,mimi binafsi namwona Lowassa kama my hero.Vijana wenzangu tunahitaji kufanya maamuzi magumu kama mzee lowassa aliyofanya.Potelea pote hata asipoingia ikulu,lakini alifanya maamuzi na kuamua kwamba hii inatosha.
Nchi yetu inapaswa kuwa mbali sana.Masuala ya maji na nishati sio mambo ambayo kama Tanzania ingekuwa na viongozi makini isingekuwa mahali hapa.Nasi tunapaswa kufanya maamuzi magumu.Tanzania ni ya watanzania wote bila kujali dini,kabila wa rangi.Tusiwe wepesi kuogopeshwa na maneno ya akili ndogo,watu wenye kutaka kuhothi uongozi wa nchi kwa maslahi yao binafsi huku sisi tulio wengi tukiteseka.

namaliza nikiomba watanzania tufanye maamuzi magumu sasa.Hakuna kurudi nyuma.Kwa miaka 50,CCM haijafanya chochote.Tuangalie kenya,walithani kwamba hakuna chama kingine kinachoweza kuleta maendeleo zaidi ya KANU.leo kanu ipo wapi??

Heko mzee lowassa.

Dalili zote zinaonyesha mkamio uliopo Kwenye kambi kuu za vyama vwili ccm na cdm < ukawa ni kiini macho tu> ni kuwa ktk uchaguzi wa mwaka huu kupita mingine yote, kiu ya kuingia ikulu ni kubwa, hii inatokana na kuwa nchi iko kwenye mazingira mazuri kiuchumi kuliko wakati mwingine wowote kwakua karibuni nchi inategemea kuingia kweye utajiri wa mafuta na gesi, kwa hali hiyo mosi,
ccm ni kufa na kupona ku consolidate power, siamini wataacha nchi kwa urahisi hivyo, hiyo inapaswa kuzingatiwa sio kitu cha kupuuzia. Hata ningekua mimi nisingekubali, nihangaike kutafuta halafu nije ni waachie wengine wavune!!Ni wachache wenye ubavu huo, <omar bongo, Dos santos na obien nguema ni mifano hai, hawatoki ngo!! Nchi zao tajiri wa mafuta >na
Pili, iwe iweje Lowasa nae kwa mwendo wake huu wa fisi mlafi na jinsi alivyo ukamia ukuu ni wazi kuwa kaona pesaaa!!! mhemko wote huu wa kuhangaika usiku kucha mashariki na magharibi na maswahiba zake ni kwa kuwa wanajua kuna harufu ya pesa !! na wanaitaka kwa udi na uvumba, pili anataka pia kulipiza visasi, majibu yake ya hasira ni kielelezo tosha,
kwa ccm usalama wao kwa huyu jamaa ni ndogo sana pindi itokeapo kushinda, hiyo nayo inaongeza msumari wa kufa na kupona kubakiza nchi mikononi mwao, Cdm nayo inamilikiwa na wafanya biashara kwa hiyo nao wameshanusa harufu ya pesa, ndio maana wameziba masikio pua na vinywa ili kumyaka mmasai, wao wenyewe walimnanga fisadi, ni ile kiu yao ya lazima ikulu iingiwe kwa njia yoyote! Funika kombe mwanaharamu apite!
wanajua iwapo wataingia ikulu matarajii yao ya kuvuna, njia nyeupeeee!! itakua within their reach hivyo msishangae kufunga macho na masikio na huku wakiwadanganya wapiga kura wao kwa visababu vya kipuuzi, ni kuhakikisha kwa hali, mali na hila wanaingia ikulu, hapo ndio watanzania wata lijua jiji, nawaomba wa TZ kupima kwa weledi hapo october nani anastahili kuingia ikulu, zimwi ulijualo au jini ndani ya chupa!! Kazi kwenu...
 
Napenda utendaji na usimamizi wa Lowasa. Alianzisha shule kila kata kwa miaka miwili aliyokaa madarakani kama Waziri mkuu. Alipojiuzulu kama kondoo wa kafara hapakuwa na mtu mwenye ile vision ya shule zile na hazikuendelea kwa spidi ile. Nafikiria kuwa kama angeendelea kuwa Waziri mkuu hadi sasa, kila sekondari ingelikuwa na kidato cha tano na sita, na huenda kila kata ingekuwa na kutuo cha afya! Kwenye utendaji hana masikhara, ukileta mchezo unafukuzwa hapohapo. Napenda kipaumbele chake ambacho namba moja ni elimu na namba mbili ni elimu na namba tatu ni elimu. Lakini kinachonikuna zaidi ni uwezo wake wa kufanya maamuzi magumu. Hata hili la kutoka CCM na kuingia Chadema lilikuwa gumu kweli. Binafsi sikiamini kuwa angeweza kufanya hivyo. Tunahitaji Raisi wa namna hii!
 
Muangalie lowassa kwa picha kubwa, au tukuazime miwani ya macho,, shule za kata takataka gani hiyo!
 
Shule za kata ni gabage in gabage out,,, kwakua walimu wenyewe gabage . So end product must be gabage!!
 
Wakati wa mchakato wa kupata mgombea ccm ukiendelea watu tulidhania kuwa upinzani haupo, sasa mchakato wa wapinzani unaendelea inaonekana kama ccm haipo. Sasa ni zamu ya wapinzani kusikika.

Kwa hali ya siasa ilivyo tangu siku tatu zilizopita kinachoonekana ni upepo wa kisiasa tu ambao sidhani hata siku tatu zijazo tutausikia.

Juzi ilikuwa habari ya lowassa kuamia upinzani, jana ndio habari zikaanza kusomwa na kusikika, huku habari ya leo ni kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa nafasi ya urais baada ya hapo kesho magazeti yataripoti tukio la leo, kesho kutwa sijui kutakuwa na tukio gani litakalovuta media ukizingatia kuwa siasa ni umaarufu na ili uwe maarufu ni lazima kuwe na jambo zito linaloweza kutafsiriwa kama habari.

Binafsi naona kampeni itakapoanza ndio tutajua muelekeo sahihi wa siasa za nchi zinakokwenda na sio ushabiki kama ulivyo sasa wa kuchukulia mambo kwa upande mmoja.
 
Magufuli ni msanii wa nyimbo za asili na ana nyimbo mbili tu; Alenselema na Sitawaangusha. Prof.Mwandosya amesema Magufuli hajawahi kuwa hata kiongozi wa chama ngazi ya tawi.Ni mgombea pandikizi la waliomtangulia hivyo anaenda kulinda maslahi yao na siyo kuwatumikia wananchi.

kwani lowassa alishawahi kuwa kiongozi ndani chama cha chadema? achilia mbali uanachama wake ambao hauna hata wiki then anagombea urais
 
Richard,
Binafsi katika mambo ambayo siku nyingi nilijua yanakipeleka kuzimu CCM ni kufa kwa idara ya Propaganda,au kukua kwa Propaganda machine ya Chadema,kiasi kwamba ika-counter ile ya CCM. Maana miaka ya nyuma CCM walikuwa wanaweza kuaminisha uma kuwa Majambia haya yenye rangi nyekundu ni na blue ni ya CUF,au Chadema ni chama cha dola ya KIchaga,na Ikaaminika..na wananchi wakakipigia ccm kula,ikawa jioni,aikawa asubuhi,miaka mitano ,kumi,...adfinitum!

Umenifurahisha sana you make my day. asante
 
Last edited by a moderator:
Sasa ulitaka waseme nini? Kama mtu ameamua kuhama chama si basi. Mnataka chama kimlambe miguu? Ndo mjue lowassa is nothing kwa ccm.
 
Lowasa ni mwanachama wa kawaida kama wengine kwahyo Ccm haiwezi kutoa neno wakitoa neno itakua kama wanamuogopa,
&#304;la kumbuka mti mkavu ni ngumu kuchimbwa dawa, tusubir october
 
Tangu kuanza kwa drama za watu waliokatwa na wasiotakiwa ndani ya chama kuhama na wengine kutishia kuhama chama..naona ccm wako kimya tu,ukimya wao utakua unaashiria nini?

Waseme nini ilihali mikono yao imejaa maji kwa kukinga mafuriko kwa mikono wana hamu hata ya kuongea:cheer2:
 
Back
Top Bottom