Hivi Maprofesa na PhD candidates wanapublish wapi paper zao hapa Tanzania?

Kama mdau wa elimu ya juu, mi sina cha kujitetea hapa. Kiukweli mifumo yetu ya kufanya utafiti katika vyauo vyetu ni duni sana. Na matunda ya tafiti hizo ni duni sawia. Baadhi ya sababu zinazopelekea uduni huo ni za kihistoria lakini zingine ni za kujisababishia hivi karibuni.

Sababu za kihistoria ni kwamba falsafa na mazingira yaliyoanzisha vyuo vyetu vya kwanza kabisa(UDSM kwa mfano) kufanya tafiti zilizoiva na zenye kutatua matatizo au changamoto halisi za asili katika nyanja zote za maisha haikuwa kipaumbele.

Vingi vya vyuo hivi katika afrika vilianza kama taasisi za kutengeneza wasomi walau watakaoweza kuchukua nafasi za kiutawala mara baada ya wakoloni kuachia madaraka. Hiyo ndio falsafa, msukumo ulioanzisha vyuo hivi. Liberal arts universities. Na tumebaki katika mfumo huo hadi leo hii. Wasomi wengi usomi wao hutambulika PhD zao zinapowabeba kwenye siasa au kufanya waonekane katika mambo ya kisiasa.

Tanzania hatujawahi kuwa na vyuo ambavyo uwanzilishi wake kifalsafa(iwe ni mtu binafsi, watu binafsi, au serikali kwa maana ya vision) unalenga utatuzi wa matatizo halisi katika sayansi ya jamii, sayansi ya asili, applied science, na mengineyo.

Kuwa na msukumo sahihi wa kifalsafa kunapelekea hata aina ya chuo kinavyo operate kufikia malengo yake: namna kinavyoajili lecturers and professors, namna kinavyodahili wanafunzi, namna kinavyotaka wanafunzi wa graduate, namna kinavyotaka kitambulike na kuheshimika, na kadhalika.

Kwa mfano UDSM au chuo chochote Tanzania, hakina mfumo wa ulipaji mishahara kulingana na ubora wa tafiti za researchers wake. Pale nyote, so long as mnaitwa professors mtakuwa na mshahara mmoja. Uwe professor wa Kiswahili au professor wa medicine. Huyu awe anaingiza grant zero per year, mwingine anaingiza 1 M USD per year. Nyote ni mshahara mmoja.

Si ajabu UDSM au any other public university for that matter ni vigumu kushawishi watu innovative, wenye IQ kubwa, wenye weledi sawia kubaki bongo kufanya tafiti. Wapo Harvard huko(wakienda kusoma hawarudi), vyuo vya bongo vinabaki na makapi(si tusi mi ni mmoja wao, kama ni tusi najitukana pia).

Wenzetu msukumo wao ni kuzawadia ubunifu na ubora katika utatuzi wa matatizo halisi, sisi msukumo wetu ni upate PhD ili uitwe msomi miongoni mwa wasiosoma ili useme chochote kizuri kwa watawala ili uwe mmoja wao. Research Intensive universities versus Politically motivated universities!

Vitu viwili tofauti, matokeo tofauti kabisa.

Nimependa uchambuzi wako uliojaa maono ya hali ya juu,umegusa kwenye moyo wa tatizo hasa.
 
Naona umeamua fagilia ifakara kwa vile unafanya hapo.Na hiyo kusema nasema kitu nisichokijua ,ndipo unakosea sana.Bora ungetoa maelezo yako yenyewe ndio yaseme km najua au sijui.Hujajibu nilichokuuliza hapa ,Pia Hivi Ina maana watu wote ktk afya mpo kwenye Malaria tuu?Hizo project za malaria wazo la jumla limetoka kwa wenyewe na zinafanyika duniani kote.US wana historia ya kupambana sana na malaria na tafiri wanazofanya duniani kote ili kupata vimelea wa aina zote.Wamarekani waliwahi tuma marine wao kwenda kuiba dawa ya malaria ambayo ilikuwa ikipatikana ktk mmea ambao ulikuwa ukiota china na wachina waliwhai tangaza kuwa wana dawa inayoweza fagia wadudu haraka sana.Kwa US ilikuwa ni kitu cha kutafuta km dhahabu kwa ajili ya askari wao wanaotembea dunia nzima.Waliiweka operation kabisa na wakafanikiwa uiba huo mmea na kuupelea us na kufanya tafiti zote na kupata formula ya hiyo dawa.Unachoongea hapa ni km wakenya na MPESA..huwa wanaamini ni yao na wao ndio wagunduzi....wakati safaricome na wengine wanapigwa sana makato ya royalty ya patent na services.unasema mafua ya ndege...mbona usisem mabusha,ukoma, kukatika pua, makengeza kwa watz watoto na wakubwa..etc?Kuna shida sana jinsi mnavyofikiri...ndio maana mnaita washina na waarabu ndugu zetu..wakati wao hawataki mbegu zenu.Sidhani hata km setting nzima ni idea ya m bongo.Hizo kelele kuwa hata vyuo vya huko haviwezi na huku kuna sales branches ni lame excuses tuu..kwani Bill gate alipoleke miradi ya malaria Handeni na Ifakara Micorsoft walikuwa hata branch ya sales hapa TZ?Makampuni ya kihindi ya kipumbavu tuu yanamwagiwa hela hadi za kufanya upasuaji wa urembo.... Kuna mengi umeongea kutetea roho yako ktk maeneo uliyo na maslahi nayo...hembu nikuulize ktk vyuo vyetu ni ni asilimia ya masomo yanapata external invigilators kutoka hata nje ya east africa? Kuna fani ambazo hazihitaji labs za kutisha ,je ni patents kiasi gani zinafunguliwa pale UDSM?ujue kila tafiti ina nafasi ya kuja patent ambayo ni hela.Watu wengi wanapewa title na Maprof wao,wanaweza endeleza au anza km ni jipya,au wanaweza badilisha.Ku Excel kwa watu km nyie ni kawaida sana kwa vile ni masters wa concepts za watu,hilo halina shida mtacrame mnarudiarusia sana na kuandika vyema hata km hamuani mlichoandika ila baada ya hapo hakitokuwa na connection ktk real practice kwa vile hakina origine ndani yenu.
.Mkuu kwa moyo mkunjufu nimesoma contents zako zimenigusa it seems your among few analyst i can trust them here.MSAADA.Nina masters ya uchumi wa kilimo,nimekuwa nikifanya kazi halmashauri fulani hivi in peripheral areas.my dreams ni kusoma PHd abroad au hapa nyumbani,naomba kujua hatua za mwanzo kabisa niweze kuanza mchakato.Asante
 
Kama mdau wa elimu ya juu, mi sina cha kujitetea hapa. Kiukweli mifumo yetu ya kufanya utafiti katika vyauo vyetu ni duni sana. Na matunda ya tafiti hizo ni duni sawia. Baadhi ya sababu zinazopelekea uduni huo ni za kihistoria lakini zingine ni za kujisababishia hivi karibuni.

Sababu za kihistoria ni kwamba falsafa na mazingira yaliyoanzisha vyuo vyetu vya kwanza kabisa(UDSM kwa mfano) kufanya tafiti zilizoiva na zenye kutatua matatizo au changamoto halisi za asili katika nyanja zote za maisha haikuwa kipaumbele.

Vingi vya vyuo hivi katika afrika vilianza kama taasisi za kutengeneza wasomi walau watakaoweza kuchukua nafasi za kiutawala mara baada ya wakoloni kuachia madaraka. Hiyo ndio falsafa, msukumo ulioanzisha vyuo hivi. Liberal arts universities. Na tumebaki katika mfumo huo hadi leo hii. Wasomi wengi usomi wao hutambulika PhD zao zinapowabeba kwenye siasa au kufanya waonekane katika mambo ya kisiasa.

Tanzania hatujawahi kuwa na vyuo ambavyo uwanzilishi wake kifalsafa(iwe ni mtu binafsi, watu binafsi, au serikali kwa maana ya vision) unalenga utatuzi wa matatizo halisi katika sayansi ya jamii, sayansi ya asili, applied science, na mengineyo.

Kuwa na msukumo sahihi wa kifalsafa kunapelekea hata aina ya chuo kinavyo operate kufikia malengo yake: namna kinavyoajili lecturers and professors, namna kinavyodahili wanafunzi, namna kinavyotaka wanafunzi wa graduate, namna kinavyotaka kitambulike na kuheshimika, na kadhalika.

Kwa mfano UDSM au chuo chochote Tanzania, hakina mfumo wa ulipaji mishahara kulingana na ubora wa tafiti za researchers wake. Pale nyote, so long as mnaitwa professors mtakuwa na mshahara mmoja. Uwe professor wa Kiswahili au professor wa medicine. Huyu awe anaingiza grant zero per year, mwingine anaingiza 1 M USD per year. Nyote ni mshahara mmoja.

Si ajabu UDSM au any other public university for that matter ni vigumu kushawishi watu innovative, wenye IQ kubwa, wenye weledi sawia kubaki bongo kufanya tafiti. Wapo Harvard huko(wakienda kusoma hawarudi), vyuo vya bongo vinabaki na makapi(si tusi mi ni mmoja wao, kama ni tusi najitukana pia).

Wenzetu msukumo wao ni kuzawadia ubunifu na ubora katika utatuzi wa matatizo halisi, sisi msukumo wetu ni upate PhD ili uitwe msomi miongoni mwa wasiosoma ili useme chochote kizuri kwa watawala ili uwe mmoja wao. Research Intensive universities versus Politically motivated universities!

Vitu viwili tofauti, matokeo tofauti kabisa.

Asante sana mkuu kwa hii perspective

By the wa hakuna anayelaumu for the sake of it. Wengi wetu hapa ni wadau wa elimu ya juu.
 
.Mkuu kwa moyo mkunjufu nimesoma contents zako zimenigusa it seems your among few analyst i can trust them here.MSAADA.Nina masters ya uchumi wa kilimo,nimekuwa nikifanya kazi halmashauri fulani hivi in peripheral areas.my dreams ni kusoma PHd abroad au hapa nyumbani,naomba kujua hatua za mwanzo kabisa niweze kuanza mchakato.Asante

!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????
 
Na kurudi kwenye mstari itakuwa vigumu sana. Mazingira ya siku hizi kwenye vyuo vyetu yamezidi kuwa kongwa zito kwa wanataaluma hasa wanaochipukia kuweza kupenyesha mawazo yao yawe sera za vyuo.

Kwa mfano kuna sera ya ajabu imeanzishwa pale UDSM kuhusu publications hata hujui walioianzisha wana maana gani.

Ni kuhusu publications: kwamba ili upate points za kutosha kuwa promoted inabidi uwe single authored kwenye publcations zako. I mean, haimaanishi ukiwa multi authored (watu wawili na zaidi) hautapata promotion but itakuchukua muda mrefu sana kwa vile zile credits za kukupromote zinagawanywa sawa miongoni mwa collaborators wako kwenye hiyo paper.

Sasa matokeo ya sera hiyo ni kuzidi kudunisha ubora wa publications na ubora wa tafiti zinazofanyika.

Haiyamkiniki ni namna gani unaweza kufanya research ya biochemistry, physics, computational sciences and electronics, engineering, medicine na complex sciences kama hizo halafu upublish paper yako ukiwa single authored. High impact research huwezi kufanya kazi peke yako(ina maana hukuwa na assistants wowote, lab, field, data analysis, vyote hivyo umefanya peke yako?)

And guess what, high impact journals kama Nature, Science, PNAS, New England Journal of Medicine, hawapokei paper yako ukiwa single authored. Wanajua ni uwongo, modern science huwezi kufanya peke yako.

Matokeo yake ni nini? Wanaopata promotion ni akina nani? Akina Kitila Mkumbo, Benson Bana, na wenzao wa REDET(Kituo cha kidemokrasia kinachofanya opinion polls kuwa mgombea gani wa CCM anakubalika sana kwa urais akifatiwa kwa mbali sana na wa Chadema).

Wasiopata promotion ni akina nani. Ni wale madaktari wa moyo pale Muhimbili, oncologists wa Ocean Road, nuclear physicists wa Physics department pale UDSM, na fani nyingine zisohusiana na siasa kabisa.

Madhara yake ni nini? Tanzania itaendelea kubaki kwenye mgao wa umeme wa maji mpaka Yesu atakaporudi, diagnosis na matibabu ya cancer itabidi uwe tajiri kama Mengi kupata huduma sahihi India au US.
 
Bahati nzuri wasomi wengi wa Tanzania wamechukulia PhD zao Ulaya, Asia, na Marekani.

Grad school yoyote ya Kueleweka duniani ina-tie faculty members wao kufanya publication, hivyo hadi wakati unafanya VIVA si jambo la ajabu kuwa umefanya publication zaidi ya 5, kutokana na uwezo binafsi wa candidate na financial might ya faculty.

Shida yako unataka publication za kitaaluma ukazitoe kwenye google au JF. Si kila publication iko available to public, some of the most respected journals in the world are members only journals. Hivyo madenge wa kawaida ni ngumu kupata access.

Pili, kwenye baadhi ya Sekta, hasa sayansi ya jamii, medical research (diseases), Tanzanian academics and research centers are very good.the facilities at Ifakara for example are some of the very best in Malaria research. Kuna sehemu tuko nyuma kama tafiti za Engineering, lakini maprofesa wengi wa TZ wamesoma nje,ambako wamefanya publication kiasi, shida iko kuwa wakisharudi TZ Hakuna funding.

hivi leo hii serikali ikiambiwa itoe $100M kufanya setup ya telecommunications lab ya kueleweka,in 5 years itatoa hizo pesa?sasa hauwezi kufanya research wakati hauna proper lab setup. Ndio maana unaona wanaishia kufanya market research tu.aka Siasa.

Kuhusu hivi vyuo vichanga, you may have a point regarding their promotion practices, But there is nothing wrong with receiving promotion faster than another university since in some universities, someone might be an associate professor for longer than another university, because the university does not have enough positions to make him/her a full professor. Remember these universities started from scratch. The issue of being made full professorship hence becomes an administration issue and not an academic one.

I will give you an example, I work for a world class research company that has lots of Scientists that produces excellent research and are extremely qualified. From time to time big universities in UK and Europe would poach some of them for full professorship positions without having to go through the Senior lecture>Associate Professor>Professor route. Since when you have an opening at a university, you do not look at who is next in line, rather you look for who is the most qualified to lead a department. So, sometimes an expert from industry can catapult from being a Normal PhD guy with no teaching affiliation to being a full professor at a University. It's all based on Qualifications, and what the department is looking for.

1. Kwenye red hapo juu iweje shida yako useme shida ya mwingine? Google inasaidia ku-locate scholarly works ila sio rahisi kupata full text kama article haiko kwenye open access. Lakini summary au abstract ya peer reviewed journal articles zitaonekana,
2. kwenye hiyo world class research institution job position au title yako ni ipi?
3. ulaya kuna ufuatiliaji wa hali ya juu sio kama huku Bongo soma hapa Home : REF 2014
 
Naona umeamua fagilia ifakara kwa vile unafanya hapo.Na hiyo kusema nasema kitu nisichokijua ,ndipo unakosea sana.Bora ungetoa maelezo yako yenyewe ndio yaseme km najua au sijui.Hujajibu nilichokuuliza hapa ,Pia Hivi Ina maana watu wote ktk afya mpo kwenye Malaria tuu?Hizo project za malaria wazo la jumla limetoka kwa wenyewe na zinafanyika duniani kote.

Duh, ndugu, hujui malaria ni tropical disease?umeshawahi ona chuo kinafanya research ya mafua tanzania?sio primary concern yao, unapona bila hata dawa.
Nimetoa mfano wa IHI, kwa sababu they are a world class research facility in their field, I do know that for sure. Wewe usijejua ABC za research huwezi jua mchango wao katika tropical disease. Mimi sio mtaalamu wa tiba, mimi ni mhandisi mtafiti.

US wana historia ya kupambana sana na malaria na tafiri wanazofanya duniani kote ili kupata vimelea wa aina zote.Wamarekani waliwahi tuma marine wao kwenda kuiba dawa ya malaria ambayo ilikuwa ikipatikana ktk mmea ambao ulikuwa ukiota china na wachina waliwhai tangaza kuwa wana dawa inayoweza fagia wadudu haraka sana.Kwa US ilikuwa ni kitu cha kutafuta km dhahabu kwa ajili ya askari wao wanaotembea dunia nzima.
Unachanganya mambo drug development process ina-involve clinical trials ambazo ni lazima zifanyike sehemu active ya tatizo, ndio maana hata baada ya kupata "tiba" ya ebola, ilibidi kuwe na outbreak yenye significant sample specimen ili kuweza ku-validate clinical findings zao, bila validation hakuna tiba. Sasa ukichukua chain zima ya drug development kwenye dunia ya kwanza kila nchi/kampuni ina expertise yake, wengine wame-specialize kwenye testing, wengine clinical trials, wengine core research. Sasa ili ujue competence ya research institute ni lazima ujue area of competence and focus, kama hujui hilo hautakuwa na tofauti na mtu anayelaumu boti ya Azam kuchelewa wakati yuko Ubungo Bus Terminal, it will never come.

Waliiweka operation kabisa na wakafanikiwa uiba huo mmea na kuupelea us na kufanya tafiti zote na kupata formula ya hiyo dawa.Unachoongea hapa ni km wakenya na MPESA..huwa wanaamini ni yao na wao ndio wagunduzi....wakati safaricome na wengine wanapigwa sana makato ya royalty ya patent na services.

Sasa umeanza kuparanganya mambo, unachanganya scientific research na product development. Kwa kuwa umekuja kwenye kitu ninachokifahamu vizuri ngoja nikupe Darsa.

M-Pesa and many other mobile money services uses very simple messaging protocols developed many years ago,MPESA is an example of a product not of core research.Sasa kusema nimevumbua MPESA hakuna tofauti na kusema nimevumbua Whatsapp. They are just products, it's implementation that matters,which is why you are paying extra for an iPhone than you would for a Huawei Phone.Product.

Kuhusu MPESA as a product nani kaanzisha, that is Safaricom internal business, but looking from the outside, that is purely their product.on what platform did they build this product on, is a question that only they can answer.Sasa kuja hapa kubwatuka kuwa MPESA and mobile money was developed by westerners is lack of understanding on what MPESA as a product really is.Kama hujanielewa, kamata graduate wa MBA au IT management akueleze kuhusu Product development cycles.

unasema mafua ya ndege...mbona usisem mabusha,ukoma, kukatika pua, makengeza kwa watz watoto na wakubwa..etc?Kuna shida sana jinsi mnavyofikiri...
FYI, Dr. mwele, na Dr. Makani ni kati ya wataalamu watanzania wa kiwango cha juu zaidi kwenye hayo magonjwa uliyoyataja, huwezi kujua hayo kwa sababu wewe ni mwanasiasa,tafiti wanazofanya zinafanyika Tanzania kupitia Research institutes za Kitanzania.Huelewi ukipewa mfano, una matatizo gani?sasa unataka niweke bibliography ya magonjwa yote TZ hapa?

ndio maana mnaita washina na waarabu ndugu zetu..wakati wao hawataki mbegu zenu.Sidhani hata km setting nzima ni idea ya m bongo.Hizo kelele kuwa hata vyuo vya huko haviwezi na huku kuna sales branches ni lame excuses tuu..

I don't get connection ya ulichoandika na mada, seriously.

kwani Bill gate alipoleke miradi ya malaria Handeni na Ifakara Micorsoft walikuwa hata branch ya sales hapa TZ?Makampuni ya kihindi ya kipumbavu tuu yanamwagiwa hela hadi za kufanya upasuaji wa urembo.... Kuna mengi umeongea kutetea roho yako ktk maeneo uliyo na maslahi nayo...

Huwezi kutoa hoja bila kutoa assumptions na accusations zisizo na any profound evidences?huu ni utoto,kama unataka tuendelee kujadili kuhusu utafiti, achana na huu ujinga tujadili kuhusu utafiti.

hembu nikuulize ktk vyuo vyetu ni ni asilimia ya masomo yanapata external invigilators kutoka hata nje ya east africa?
Sifanyi na sijawahi kufanya kazi au kusoma kwenye High education institute Tanzania. Hili swali kuna wenye majibu, sio mimi.

Kuna fani ambazo hazihitaji labs za kutisha ,je ni patents kiasi gani zinafunguliwa pale UDSM?ujue kila tafiti ina nafasi ya kuja patent ambayo ni hela.

Again unachanganya madudu, Patents is an American IDEA that aims at protecting scientific innovations, hakuna scientific innovation isiyohitaji "Lab ya kutisha", kama ulivyoziita wewe, ukiona unafanya experiment cheaply jua most likely unawork on 1950's ideas and concepts, haufanyi kipya, ndio maana nikakueleza usichanganye madawa.

Kuhusu core competence ya UDSM nadhani ni kwenye maswala ya yasiyo ya kisayansi, haya hayana mambo ya patenting sana. umeshawahi kuona mtu anapatent social behaviour?child psychology?sidhani.

Watu wengi wanapewa title na Maprof wao,wanaweza endeleza au anza km ni jipya,au wanaweza badilisha.Ku Excel kwa watu km nyie ni kawaida sana kwa vile ni masters wa concepts za watu,hilo halina shida mtacrame mnarudiarusia sana na kuandika vyema hata km hamuani mlichoandika ila baada ya hapo hakitokuwa na connection ktk real practice kwa vile hakina origine ndani yenu.

Unaonesha kabisa hujui lolote kuhusu utafiti, Duniani kuna watafiti wengi sana, criteria kubwa ya kuwa mtafiti mbobezi sio kujua sana au kujua vingi, bali ni kujua vizuri kile unachokijua. Hapa namaanisha specialization. Ndio maana ya kuwa na faculty. watafiti wanafanya kazi kwa kushirikiana. njia rahisi ya kujua ubora wa aina ya utafiti na mtafiti mwenyewe ni kuangalia simple metrics kama citation by reputable papers,authors etc. hii inaonesha kuwa ulichokifanyia utafiti kina value kwenye scientific community. unaweza kuandika paper moja ikawa cited 1000 times, na kuna mwengine akaandika paper 10 zikawa cited 2 times. Hapa mtafiti bora ni yule mwenye paper moja.Bahati nzuri watafiti wengi hawana simple mindedness unayoonesha hapa.hivyo sio kitu cha kuwa na hofu nacho.

Research Impact ni kazi tofauti na Mtafiti, ingawa ina connection,inategemea aina ya mada unayofanya na aina ya connection iliyokuwepo kati ya tafiti na jamii. na sio lazima research impact itokee mwaka huohuo.

FYI Maxwell, who is arguably one of the smartest Humans to have ever lived, wrote about Electromagnetism 150 years ago. No one then understood jackshit of what he wrote and the scientific community simply discarded most of his theories as too difficult to understand, useless and not with any impact to the research work at a time.

It took several decades after his death, for a Human capable of understanding what he wrote to simplify the complex works and dozen equations into four fundamental equations of electromagnetism.By then Maxwell himself was long dead and rightfully forgotten at a time.So using your simple mindedness of wanting to classify research impact of a researcher immediately, it goes on to show how shortsighted you are, and the very reason why Tanzanian Politicians do not fund real core research.

Back to Maxwell, after a few decades of carefully simplifying his equations and opening them up to other researchers, other scientists began to realize how important the equations were,and within a few years we had radio communications,radar,TV, the internet inventions etc etc.People glorify Einstein because a guy named Maxwell made it possible for Einstein to invent the theory of photoelectric effect (yes! not relativity) that won him the Nobel Prize. You probably never heard of Maxwell before,nor know what he looks like, yet everyone knows what Einstein is. But, in the scientific community especially in physics and engineering, Maxwell is almost a God and referred to as father of Electromagnetism.You are discarding role of core research with no immediate impact (slow impact) on the internet that works because Maxwell was bold enough to tell everyone that invisible forces (magnetism/electricity) exist that can transmit information.How ironic is that?

So as long as you look at Tanzanian researchers with short term-ism that is common among Tanzanian bureaucrats, you will never appreciate their work.

Nobel Prizes award researcher for work they did 4-5 decades ago, Many developed Nations have several awards at National level,is there any in Tanzania?where is the motivation?zero.

I do not say that the scientific community in Tanzania is perfect, or it is excellent, but i showed you that the premise you brought forward is wrong and without any solid ground.

If you were conversant in research, this could have been a very good discussion, but you are intent on politicizing it. Which i think is wrong.

Blame game and short term-ism is exactly what got us to this mess.it will out get us out of it,
 
1. Kwenye red hapo juu iweje shida yako useme shida ya mwingine? Google inasaidia ku-locate scholarly works ila sio rahisi kupata full text kama article haiko kwenye open access. Lakini summary au abstract ya peer reviewed journal articles zitaonekana,

Si kila keyword google itakuletea research work unazotaka,pia sio kila research work iko indexed google, there are a lot of private,propriatery research in the world, these are full membership paid only research. How do i know?i work in a place with such restrictions to many of its publications.
Kuhusu abstract yes, you can get that from google, but i don't think it will tell you that the authors are Tanzanian.

Pia unatakiwa ujue unatafuta nini(keywords), na unatakiwa ujue unamlenga nani,sasa huyu bwana mdogo labda anadhania watafiti wa kitanzania ni shivji na wenzake tu.

Tazama mfano huu mdogo

Evaluating M-ary PSK multiple-subcarrier modulation over FSO links using aperture averaging(Conference Proceedings)
Authors:C. Ben Naila, A. Bekkali, K. Kazaura, et al.
Published:24 Aug 2010

Hiyo hapo juu ni kazi ya mtanzania, ambaye watu wengi watakuwa wanamfahamu humu ndani, lakini je? utawezaje kupata hiyo kazi kama hujui kitu gani unatakiwa ukitafute?
wengine wanaitwa John David na ni watanzania kutokea kilosa,morogoro.

Angalau huyu jina linaweza kukupa hint kuwa ni mtanzania likiwa in full

Spectral model of optical scintillation for terrestrial free-space optical communication link design(Journal Paper)
Authors:Kyung-Hwan Kim, Takeshi Higashino, Katsutoshi Tsukamoto, et al.
Published:01 Mar 2011

2. kwenye hiyo world class research institution job position au title yako ni ipi?

You might as well ask me my government name!

3. ulaya kuna ufuatiliaji wa hali ya juu sio kama huku Bongo soma hapa Home : REF 2014

Yeah, wenzetu wana institutions zenye centuries of foundation, this has made them strond and principled. Tanzanian bado sana, but as individuals, Tanzanian researchers are as excellent as the best in the world.Take it from me.
But in Research and many things in life, being excellent is not going to get you anywhere, many other matrixes are involved that work in parallel.
 
Kama mdau wa elimu ya juu, mi sina cha kujitetea hapa. Kiukweli mifumo yetu ya kufanya utafiti katika vyauo vyetu ni duni sana. Na matunda ya tafiti hizo ni duni sawia. Baadhi ya sababu zinazopelekea uduni huo ni za kihistoria lakini zingine ni za kujisababishia hivi karibuni.

Sababu za kihistoria ni kwamba falsafa na mazingira yaliyoanzisha vyuo vyetu vya kwanza kabisa(UDSM kwa mfano) kufanya tafiti zilizoiva na zenye kutatua matatizo au changamoto halisi za asili katika nyanja zote za maisha haikuwa kipaumbele.

Vingi vya vyuo hivi katika afrika vilianza kama taasisi za kutengeneza wasomi walau watakaoweza kuchukua nafasi za kiutawala mara baada ya wakoloni kuachia madaraka. Hiyo ndio falsafa, msukumo ulioanzisha vyuo hivi. Liberal arts universities. Na tumebaki katika mfumo huo hadi leo hii. Wasomi wengi usomi wao hutambulika PhD zao zinapowabeba kwenye siasa au kufanya waonekane katika mambo ya kisiasa.

Tanzania hatujawahi kuwa na vyuo ambavyo uwanzilishi wake kifalsafa(iwe ni mtu binafsi, watu binafsi, au serikali kwa maana ya vision) unalenga utatuzi wa matatizo halisi katika sayansi ya jamii, sayansi ya asili, applied science, na mengineyo.

Kuwa na msukumo sahihi wa kifalsafa kunapelekea hata aina ya chuo kinavyo operate kufikia malengo yake: namna kinavyoajili lecturers and professors, namna kinavyodahili wanafunzi, namna kinavyotaka wanafunzi wa graduate, namna kinavyotaka kitambulike na kuheshimika, na kadhalika.

Sijui Falsafa gani unayoizungumzia hapa, but i see a lot of technical colleges, medical colleges and recently tourism colleges, these are institutions started to address specific inadequacy in the society. SUA is an agricultural university and among the very best in Eastern,southern and Central Africa at that.

Nakubali kuna vyuo comprehensive kama UDOM,mara nyingi uwepo wa vyuo hivi hauepukiki wakati unataka kuongeza enrollment, vipo kote duniani.

Kwa mfano UDSM au chuo chochote Tanzania, hakina mfumo wa ulipaji mishahara kulingana na ubora wa tafiti za researchers wake. Pale nyote, so long as mnaitwa professors mtakuwa na mshahara mmoja. Uwe professor wa Kiswahili au professor wa medicine. Huyu awe anaingiza grant zero per year, mwingine anaingiza 1 M USD per year. Nyote ni mshahara mmoja.

Hili ni tatizo, kunatakiwa kuwe na performance bonuses at departmental level, sio individual level, kwani research ni team work.sijawahi kuona individual level bonuses kwenye research institute. Departmental level bonuses helps enhance cooperation and teamwork.

Si ajabu UDSM au any other public university for that matter ni vigumu kushawishi watu innovative, wenye IQ kubwa, wenye weledi sawia kubaki bongo kufanya tafiti. Wapo Harvard huko(wakienda kusoma hawarudi), vyuo vya bongo vinabaki na makapi(si tusi mi ni mmoja wao, kama ni tusi najitukana pia).

I am guilty of this as well, there is just too much politics in Tanzania at the moment, and this is mostly as a result of short term thinking of politicians and Tanzanians.

Wenzetu msukumo wao ni kuzawadia ubunifu na ubora katika utatuzi wa matatizo halisi, sisi msukumo wetu ni upate PhD ili uitwe msomi miongoni mwa wasiosoma ili useme chochote kizuri kwa watawala ili uwe mmoja wao. Research Intensive universities versus Politically motivated universities!
Vitu viwili tofauti, matokeo tofauti kabisa.

Very good insights, as we can all see, the problem is again neither the work carried down by our researchers nor their competence, rather its administrative incompetence, which are sometimes politically motivated.
Niliwahi sema, ukiwa kwenye bwawa la matope, ni vigumu kuwa msafi, vivyo hivyo ukiwa kwenye nchi yenye incompetence ni vigumu kuwa competent.
 
Kimweri, Maximum respect Mkuu ... Inasemekana watafiti wengi wa Africa wanainufaisha Ulaya na Marekani zaidi ya Nchi zao za Asili! kuna ukweli? ... Inasemekana Asia imeendelea kwa kujikita kwenye product development zaidi kuliko uvumbuzi! Sisi tujikite kwenye lipi?
 
Ukitaka kuona baadhi yao wanapo-publish papers zao nunua Journal ya"The Accountant" inayondaliwa na NBAA Tanzania.
 
Kimweri, Maximum respect Mkuu ... Inasemekana watafiti wengi wa Africa wanainufaisha Ulaya na Marekani zaidi ya Nchi zao za Asili! kuna ukweli? ... Inasemekana Asia imeendelea kwa kujikita kwenye product development zaidi kuliko uvumbuzi! Sisi tujikite kwenye lipi?

Yes and No, research zinazofanywa na watafiti duniani kote zina local and global impact. Kuna watanzania wengi wameshiriki kuifanya dunia iwe sehemu bora, salama na yenye tija kwa kila mmoja wetu, nawafahamu mimi mwenyewe nikiwemo. Locally wanaofaidika ni serikali zenye kuona mbali, zinazopoteza mamilioni ya dola ku-fund research, globally solution zinazotokana na hizi tafiti zinatatua matatizo mengi ya watu wengi duniani.

Ukiwalazimisha watu hao kuwepo TZ, hawatafanya yale wangeyafanya pale walipo sasa, hivyo global impact kutokana na huyu mtu inakosekana.

Kuhusu Asia, kuna ukweli mkubwa, kwani hata sisi tuna facilities Asia, na kule hatufanyi core research, nyingi ni applied research and product developement. Mwanzoni hawakuwa na capacity, kwani core research inahitaji timu ya wataalamu waliobobea hasa ili iweze kunawiri, a regular world class lab needs at least 30 creme de la creme researchers ili iwe operational, huwezi amini just a decade ago hiyo ilikuwa ngumu hata kwa nchi kama China. Sasa hivi wamebadlika, na wanaelekea kwenye correct direction. it took a lot of investment in education, continually "sinking" money at the problem.

Kwa TZ sina uhakika approach ipi itafanya kazi, lakini kusema ukweli basic infrastructure za kutengeneza research as core competence ya taifa bado sana, tuziweke kwanza hizo sawa.

Kama umeme shida, sidhani kama ni busara kuweka High energy Laser facility itakayotumia 100MW kila ikiwashawa. Facilities kama CERN zinatumia a lot of energy kuwa operational, kwa TZ sio feasible.

i see opportunity kwenye EAC kama tuki-pool together our research capacity and work together in key projects, that will be a good start. EU wanafanya hivyo.
 
Kuna machapisho mazuri na yaliyoenda shule mengi tu ambayo yameandikwa na watanzania, tena yapo katika majarida/jounal kubwa duniani. Tatizo watanzania wengi tu wavivu wa kusoma. Na pia hakuna pesa ya kutosha kufanya uwasilishaji wa yaliyoandikwa kwa jamii husika.
 
N jukumu la serikali kinvest kwenye utafiti na.elimu. Hizi blah blah za kutafuta mchawi wala hazitusaidii.Tunajua tatizo lilipo halafu tunaendelea kuwalaumu academics. Na wao ni watu kama sisi wana ahitaji yao. Kama serikali haiwajali kwa nini wao wajali? Tunataka vitu vikubwa bila kuinvest halafu tunakuja jamii fotums kuongea ujibga ujinga tu
 
Hivi mtu Kama Kitila Mkumbo utamweka ktk kundi lipi? maana anatia Huruma!!!!

Inasemekana alifanya vizuri alipiga viti kumi na sita [16] lakini sasa wasomi wetu hawa, findings zao kazi zake zinatufaidishaje umma...ebu ngoja tuone political labalotory kupitia ACT itazaa matunda mema.

Ila pia tuna tatizo linalochangia la baadhi ya makabila ya kiafrika kuendekeza tabia ya ubinafsi, na unafiki...ni kupitia Wasomi hao kwa haiba ya Ukabila wamevuluga maendeleo ya sekta hizo na yameshindwa kwenda mbele kwa kuwa tu mshauri ni msomi wa kabila ama la MKARA....au MKEREWE.

Mfano wa hivi vielement vya ukabila vimezaa matatizo pia kwenye kada ya wasomi na kujenga wasomi waendekeza ukabila na unafiki kupitia vinasaba vya ukabila.Si lahisi kuliona hili lakini walio kwenye taasisi za elimu ya juu wanajua madhara haya.

As a national ukweli tunapaswa kuona Tafiti na Maendeleo [R & D] bajeti yake ya kuwekeza kwenye tafiti muhimu kupitia Serikali inaongezeka na kuwa na asilimia kubwa...Mfano sijaona bajeti ya serikali kwenye sekta ya elimu ya juu hasa Research & Development [R&D] asilimia zake kwa bajeti zilizopita ni ngapi?, na uwiano wake na malengo ya Maendeleo kwa Taifa kulingana na kasi ya maendeleo ya Dunia ya sasa vinaendana KWA UHALISIA.

Vyuo kama UDSM vinaitajika, kufanya mageuzi jinsi ya kuwaza, kufikilia na kutenda. Wanaweza kufanya kazi japo na makampuni binafsi makubwa ya ndani hasa kama kwa sasa kwenye makampuni binafsi ya simu kama TIGo, VODA, AIRTEL NA ZANTEL katika eneo la Masoko na Biashara.

UDSM wakitengeneza Benchamark na kampuni hayoo, japo yana damu ya MULTINATIONS,lakini bado kupitia Serikali kuna mambo yanaweza kufanywa kati ya chuo [UDSM] na Mashirika hayo kupitia Customer Social Responsibility [CSR].Na manufaa ya matokeo ya Tafiti hizo yafanyiwe kazi hapa hapa Tanzania.Sioni kama ni tatizo Wanaweza kuwasilisha maombi pia kwenye Business Roundtable ya CEO wa Makampuni yalioko Tanzania Wakiwa na Chapisho la kuomba kufanya kazi na Roundtable hiyo kwenye angle ya Masoko, Biashara na Ujasiliamali Tanzania.Nina hakika Kupitia mjumuiko wa Makampuni hayo hawakosi 5M USD kusupport kazi hiyo.Na ikifanywa kwa manufaa ya Taifa nina hakika Tutapiga hatua na kupanua Masoko na Biashara sio tu kwa kuangalia soko la Tanzania na East Africa hata kufika Africa nzima na mabara mengine nje ya Africa.

Tuna wanasiasa wavivu wa kusoma, kujifunza na kupima uzito wa kujua umuhimu wa kuhamasiki na kuvutika kupitia hata haya machapisho ya hizi PHD za watanzania wenzao na kuona umuhimu wa kuzipa nguvu ziweze kufanyiwa kazi.
 
Tanzania tuna maprofesa wengi na wabaheshimika nje kutokana na research wanazofanya, ukitaka kulijua na kufahamu hilo tembekea COSTECH uone n research ngapi zinaendelea na zipi zimefanikiwa , pia ukitaka kujua hilo tembelea vyuo vya allied science , mfano SUA ,IHI, MUHAS n.k , UD wako well known sababu ya kisiasa , kuna idadi ya maprofesa wengi nawafahamu wanaofanya publication ya research zao katika international journal na kuzifaham lazima uwe interested lakini ukiwa NGWINI utabaki kupiga kelele kwenye mitandao

Tatizo kubwa kwa Tanzania ni kuwa wataalam tumesomesha wenyewe ila wanatumika na mataifa ya nje sababu ya siasa kuwa nyingi hadi kwenye taaluma,
Tatizo lingine, ni kuwa hatuwekezi pesa za kutosha katika research
 
Back
Top Bottom