TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,559
Kama mdau wa elimu ya juu, mi sina cha kujitetea hapa. Kiukweli mifumo yetu ya kufanya utafiti katika vyauo vyetu ni duni sana. Na matunda ya tafiti hizo ni duni sawia. Baadhi ya sababu zinazopelekea uduni huo ni za kihistoria lakini zingine ni za kujisababishia hivi karibuni.
Sababu za kihistoria ni kwamba falsafa na mazingira yaliyoanzisha vyuo vyetu vya kwanza kabisa(UDSM kwa mfano) kufanya tafiti zilizoiva na zenye kutatua matatizo au changamoto halisi za asili katika nyanja zote za maisha haikuwa kipaumbele.
Vingi vya vyuo hivi katika afrika vilianza kama taasisi za kutengeneza wasomi walau watakaoweza kuchukua nafasi za kiutawala mara baada ya wakoloni kuachia madaraka. Hiyo ndio falsafa, msukumo ulioanzisha vyuo hivi. Liberal arts universities. Na tumebaki katika mfumo huo hadi leo hii. Wasomi wengi usomi wao hutambulika PhD zao zinapowabeba kwenye siasa au kufanya waonekane katika mambo ya kisiasa.
Tanzania hatujawahi kuwa na vyuo ambavyo uwanzilishi wake kifalsafa(iwe ni mtu binafsi, watu binafsi, au serikali kwa maana ya vision) unalenga utatuzi wa matatizo halisi katika sayansi ya jamii, sayansi ya asili, applied science, na mengineyo.
Kuwa na msukumo sahihi wa kifalsafa kunapelekea hata aina ya chuo kinavyo operate kufikia malengo yake: namna kinavyoajili lecturers and professors, namna kinavyodahili wanafunzi, namna kinavyotaka wanafunzi wa graduate, namna kinavyotaka kitambulike na kuheshimika, na kadhalika.
Kwa mfano UDSM au chuo chochote Tanzania, hakina mfumo wa ulipaji mishahara kulingana na ubora wa tafiti za researchers wake. Pale nyote, so long as mnaitwa professors mtakuwa na mshahara mmoja. Uwe professor wa Kiswahili au professor wa medicine. Huyu awe anaingiza grant zero per year, mwingine anaingiza 1 M USD per year. Nyote ni mshahara mmoja.
Si ajabu UDSM au any other public university for that matter ni vigumu kushawishi watu innovative, wenye IQ kubwa, wenye weledi sawia kubaki bongo kufanya tafiti. Wapo Harvard huko(wakienda kusoma hawarudi), vyuo vya bongo vinabaki na makapi(si tusi mi ni mmoja wao, kama ni tusi najitukana pia).
Wenzetu msukumo wao ni kuzawadia ubunifu na ubora katika utatuzi wa matatizo halisi, sisi msukumo wetu ni upate PhD ili uitwe msomi miongoni mwa wasiosoma ili useme chochote kizuri kwa watawala ili uwe mmoja wao. Research Intensive universities versus Politically motivated universities!
Vitu viwili tofauti, matokeo tofauti kabisa.
Nimependa uchambuzi wako uliojaa maono ya hali ya juu,umegusa kwenye moyo wa tatizo hasa.