Hivi Makonda alipokuwa anatenda uhalifu wake viongozi wakuu wa Nchi kama Rais na Waziri Mkuu hawakuwa na Taarifa? Hawakujua ama hawakufahamu?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,679
218,188
Ikiwa kama Paulo Makonda ametenda unyama uliotajwa na Serikali ya Marekani na ambao umepelekea kudhalilisha nchi yetu kuliko ilivyowahi kudhalilishwa tangu Mungu aumbe mbingu na ardhi, nina swali dogo sana la kuuliza.

Je alipokuwa anatenda uhalifu huo viongozi wakuu wa nchi hii akiwemo Rais, Makamu wake na Waziri Mkuu hawakujua ? Je viongozi wa idara za Usalama wa Nchi nao hawakujua? ikiwa kama raia ambaye hakuwahi hata kuhudhuria mafunzo hata ya JKT au Mgambo anaweza kutenda mambo mabaya kiasi hiki na vyombo vya usalama vikashindwa kumuona hadi waone wazungu basi nchi yetu inahitaji huruma ya Mungu.

Vinginevyo Serikali ya Tanzania ikanushe jambo hili na kuitangaza Marekani kama Taifa la waongo wakubwa ili dunia ituelewe

Hhaiwezekani jambo kubwa la kudhalilisha nchi kama hili likapita bila kujadiliwa, hatulengi kutukana wala kuhatarisha chochote, hii ni kwa sababu kilichotajwa kufanywa na Makonda ndio cha hatari zaidi kwa Taifa letu kuliko kuhoji

Naomba kuwasilisha
 
Je alipokuwa anatenda uhalifu huo viongozi wakuu wa nchi hii akiwemo Rais , Makamu wake na Waziri Mkuu hawakujua ? Je viongozi wa idara za Usalama wa Nchi nao hawakujua ? i

Walikuwa wanamtuma ndio maana matendo yote ya Wasiojulikana Polisi walikuwa wanajikanyaga sana kuyatolea maelezo kwa kuwa walikuwa wakijua wazi ni maagizo toka juu.
 
Toka maktaba
August 18, 2019

Mabalozi wa Tanzania tuna wakati ngumu

Dr. Wilbroad Slaa ambaye ni balozi wa Tanzania nchini Sweden : Maajabu zaidi yanakuja, wenzetu wana maadili na demokrasia. Dr. Slaa anasema wao kama wawakilishi wa Tanzania nje ya nchi wanapata wakati ngumu sana kutetea nchi kwa vile 'wapinzani' wanatoa siri za matatizo ya haki za binadamu na demokrasia nje kwa wadau wa maendeleo



Dr. Slaa amefilisika kimaadili tayari anatetea mfumo wa kikadamizaji wa CCM Mpya
 
Makonda hakuna anayempenda ndani ya Serikali. Kuanzia Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu, Mawaziri, wakuu wa Mikoa wenzake hadi watendaji wakuu wa serikali ikiwemo vyombo vya dola.

Hata kwenye Chama hawamtaki na ameonywa hadi na Katibu Mkuu wa Chama. Shida ni mamlaka ya uteuzi wake na isiwe tabu kuliko CCM kupoteza kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu au Taifa kuingia kwenye economic crisis ni bora waende yeye na ayembeba. Hata Jumbe alikuwa one term president Zanzibar
 
Sio Marekani tu, hata airlines washampiga ban.
tapatalk_1580647906191.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda ametenda uovu wake wote kwa baraka za Rais Magufuli, haiwezekani Makonda afanye uhalifu wake huku akilindwa na walinzi wa kikosi maalum cha Rais (PSU) halaf eti Rais asijue....afterall Rais amemsifia mara kwa mara kuwa anafanya "KAZI NZURI" na akamtaka aendelee "KUCHAPA KAZI".

Magufuli anajua kila kitu
 
Makonda ametenda uovu wake wote kwa baraka za Rais Magufuli, haiwezekani Makonda afanye uhalifu wake huku akilindwa na walinzi wa kikosi maalum cha Rais (PSU) halaf eti Rais asijue....afterall Rais amemsifia mara kwa mara kuwa anafanya "KAZI NZURI" na akamtaka aendelee "KUCHAPA KAZI".

Magufuli anajua kila kitu
Eeee bhana eeee !!!
 
Back
Top Bottom