Hivi maisha ya Nigeria yakoje?

Hivi maisha ya Nigeria yakoje?

Isenye

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2024
Posts
486
Reaction score
2,069
Kuna mtu wangu wa karibu anaenda safari Nigeria.
Ningependa kujua maisha ya huko yakoje kuanzia usalama,social life,vyakula na mambo mengine ya msingi.
 
Kama anaenda Abuja mwambie abebe kadi ya bank yenye Visa au Master card kwani lile jiji miamala karibu yote inafanywa kupitia mtandao, pesa zao ni mzigo mkubwa kuubeba kulinganisha na zetu au Dollar.

KAma hana mwenyeji akifika airport aombe ungiwa WiFi kwa mtu kisha atumie App za Bolt kupata usafiri wa kumfikisha hotelini kwani Taxi driver wa pale Nnandi Azikiwe International Airport ni janja janja sana kwa bei za juu.

Mitaa ya Free town kuna hotel nyingi za bei za kawaida <Tsh 60,000/- kwa usiku mmoja na usalama upo vizuri sana.

Vyakula vya Abuja(Nigeria) karibu asilimia 90 viko na pilipili (peppe) hivyo unaweza ulizia kwa kila anachoagiza.

Akifikia Hotel nzuri wako na full WiFi si kama hii yetu ya kidebe atakuwa kama yupo bongo akiwa ndani kasoro normal calls pekee.

Asipende uliza kila mtu kwani watu wa west Africa huwa hawapendi ulizwa sana na mtu wasiye mjua, wapo social sana lakini lazima akujue kwanza kama vile hotel atafikia atapata nafasi ya kuongea nao vizuri sana kadri muda atakuwepo hapo.

Asisahu kujionea mipira (magari) iliyonyooka ya kila aina(left hand) pia madaraja na rami za kiwango cha kimaTaifa.
 
ok abuja ni kwa wayoruba,na mji ambao wayoruba,wa igbo na wahausa hapo ni wengi,sio mjinwenye purukushaninkubwa kama lagos,zingatia yafuatayo:
1.fata kazi iliyokupeleka
2.ukitaka demu tafuta mmoja tu uwe nae,usichanganye wanawake utapotea
3.matapeli ni wengi mno usijihusishe na dili zozote utaangamia
4.ufuska,pombe,klabu za kula raha huko ni kwao ni akili yako tu
5.Mimi nimekaa lagos ma nilichukua mdada wa ki igbo na nikazaa nae,niliidhi nae kwa raha sana
 
Sawa sawa mkuu
 
Kuna mtu wangu wa karibu anaenda safari Nigeria.
Ningependa kujua maisha ya huko yakoje kuanzia usalama,social life,vyakula na mambo mengine ya msingi.
Mji gani anakuja Kaduna, Port Hakot, Onitsha Abuja au Lagos kila mji una tamaduni/character zake
 
Aangalie movie za Aki na Pawpaw yale ndo maisha halisi ya Nigeria , waliona kituo cha polisi cha Oysterbay baada ya msanii wao mmoja kukamatwa Tz ikazua gumzo nchi nzima Nigeria wanashangaa Tz inawezaje kuwa na kituo cha polisi kizuri kama kile ilikua ni maajabu hawajawahi kuona kwao
 
Ni nchi ambayo watu wake kuuza Airport ni jambo la kawaida sana na kuna jamaa alishauza airport huko

PhD holders wanasafisha viatu
Yaani kila mmoja kasoma na ajira hakuna hivyo, kwa hiyo ni wewe na akili yako.

Kama ni kikazi akomae na kazi tu
Yaani awe kazi, nyumbani na asijhusishe nao kabisa iwe socialising au hata imani zozote
Iwe dini au ushirikina
 
Wale jamaa noma kuna aliyempiga hela trump ya maandalizi ya kuapishwa kwake.
Ni nchi ambayo watu wake kuuza Airport ni jambo la kawaida sana na kuna jamaa alishauza airport huko

PhD holders wanasafisha viatu
Yaani kila mmoja kasoma na ajira hakuna hivyo, kwa hiyo ni wewe na akili yako.

Kama ni kikazi akomae na kazi tu
Yaani awe kazi, nyumbani na asijhusishe nao kabisa iwe socialising au hata imani zozote
Iwe dini au ushirikina
 
Kuna mtu wangu wa karibu anaenda safari Nigeria.
Ningependa kujua maisha ya huko yakoje kuanzia usalama,social life,vyakula na mambo mengine ya msingi.
Wanaijeria ni watu wenye ukabira sana nimekaa nao nchi mmoja .pamoja na ukabira wana umoja sana kuliko sisi wanafiki TZ.
Wapo na umoja wa kutoana ila upande mwengine wapo kiroho mbaya kama nchini mwao.
Swala la misosi wale wanajua chakula sio huku ugali mkubwa mboga kisoda.

Kuhusu pisi za kule zinataka mapafu ya mbwa sio uwezo wako wa kizimkazi na CCm kutaka upitishwe.
 
Wa Nigeria sio kwamba wamesoma sana wamefoji sana vyeti pia waliosoma wapo kawaida tu wao kufoji ni sehemu ya maisha yao ni kawaida tu..
Kweli na hilo lipo sana na ni waizi na waongo kupita kiasi

Wamewaliza sana wazee huku Ulaya kwa kuwaomba misaada wakijiganya ni watoto wa vigogo waliofungwa kwenye nchi zenye vita
 
Back
Top Bottom