Hivi mafundi cherehani wana laana gani?

Hivi mafundi cherehani wana laana gani?

Mafundi cherehani walilaaniwa siku nyingi sana, kama maseremala tu,

Mafundi waaminifu ni wangoni tu, na kama wangekuwa ulaya wangoni wangekuwa matajiri sana kwa sababu wangekuwa ma designer wakubwa duniani, tatizo ni ule ugonjwa wao tu....
 
Siku umfumanie kaivaa suti yako uliyomwambia aishone na anaenda Kwenye Party kupartika!
 
Mimi kuna fundi nguo mpaka nimegpmbana nae pale Savei karibia na ukumbini wa Banora maana nguo hashoni ni kunirusha kalenda tu hadi mwaka unayoyoma. Sina hamu nae!
 
mtafute Rashidi Matumla au Francis Cheka uende nae lazima akupe mzigo wako
 
Aisee heri contract,mnasaini kapiga na mwisho ni lini,ikifika siku hajashona unachukua nguo na hela ya usumbufu juu
 
Nimekuwa nikizisikia tu kero za mafundi cherehani lakini na mimi yamenikuta.

Kuna fundi hapa Sinza Madukani nimempa suruali yangu apunguze kiuno, huu mwezi sasa imeshindikana.

Ilikuwa hivi, Nilipa suruali na hela kabisa ya kazi, akaniambia nifuate kesho yake. Ilikuwa Jumamosi, Jumapili sikwenda, nikaenda Jumatatu, akasema bado. Wiki hiyo nikapata safari ya wiki nzima mkoani.

Niliporudi akasema ndio ameanza kushona hivyo nije kesho yake. Bahati mbaya au nzuri nikapata tena safari.

Kurudi baada ya wiki anasema bado hajamaliza.

Jana nimekwenda sikumkuta. Leo nimemkuta eti anasema ile suruali haionekani hivyo nisubiri aitafute leo na kesho.

Hivi nimfanyeje huyu fundi? Halafu ni mtu mzima na heshima zake na ana ofisi kubwa tu!

mgeuzeee kiburudishoo uyoooo
 
Jamani, juzi nimekwenda kwa fundi nimekuta amipata suruari yangu akaanza tena kjnipiga kalenda ya kuishona. Nimeamua kuichukua tu nitaenda kuigawa.
 
Mimi nilishaacha kushonesha nguo kwa uongo wa mafundi hao
 
Nimekuwa nikizisikia tu kero za mafundi cherehani lakini na mimi yamenikuta.

Kuna fundi hapa Sinza Madukani nimempa suruali yangu apunguze kiuno, huu mwezi sasa imeshindikana.

Ilikuwa hivi, Nilipa suruali na hela kabisa ya kazi, akaniambia nifuate kesho yake. Ilikuwa Jumamosi, Jumapili sikwenda, nikaenda Jumatatu, akasema bado. Wiki hiyo nikapata safari ya wiki nzima mkoani.

Niliporudi akasema ndio ameanza kushona hivyo nije kesho yake. Bahati mbaya au nzuri nikapata tena safari.

Kurudi baada ya wiki anasema bado hajamaliza.

Jana nimekwenda sikumkuta. Leo nimemkuta eti anasema ile suruali haionekani hivyo nisubiri aitafute leo na kesho.

Hivi nimfanyeje huyu fundi? Halafu ni mtu mzima na heshima zake na ana ofisi kubwa tu!
mkuu hebu burudika na hiki kibao...
 
Last edited by a moderator:
Mimi Suti yangu hadi dakika hii miezi sita imepita. Tena ilikuwa ya sherehe wamenipiga changa la macho kesho kesho
 
Daahhh...Ktk pita pita zangu nimeikuta hii thread nikaikumbuka TV yangu.......nilimpa fundi aitengeneze before world cup ya 2014, imagine nimepigwa kalenda mpaka leo sijaipata TV yangu....mwisho wa siku ilibidi nisamehe ninunue nyingine tu!!

but kwa usawa ulivyo kipindi hiki cha Commando john itabidi nirudi kwa yule fundi anipe mali yangu nikauze hata scraper...!!
 
Back
Top Bottom