Nimekuwa nikizisikia tu kero za mafundi cherehani lakini na mimi yamenikuta.
Kuna fundi hapa Sinza Madukani nimempa suruari yangu apunguze kiuno, huu mwezi sasa imeshindikana.
Ilikuwa hivi. Nilipa suruali na hela kabisa ya kazi, akaniambia nifuate kesho yake. Ilikuwa jumamosi, jumapili sikwenda, nikaenda juma tatu, akasema bado. Wiki hiyo nikapata safari ya wiki nzima mkoani.
Niliporudi akasema ndio ameanza kushona hivyo nije kesho yake. Bahati mbaya au nzuri nikapata tena safari. Kurudi baada ya wiki anasema bado hajamaliza.
Jana nimekwenda sikumkuta. Leo nimemkuta eti anasema ile suruali haionekani hivyo nisubiri aitafute leo na kesho.
Hivi nimfanyeje huyu fundi? Halafu ni mtu mzima na heshima zake na ana ofisi kubwa tu!