Jana ktk taarifa ya Habari ya saa mbili usiku ITV nilimuona Mh. Lowassa, alihudhuria Jubilee ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, Paul Ruzoka. Nilitegemea kuwa kiongozi wa Serikali ndiye angepewa nafasi ya kuongela LAKINI kwa mastaajabu alipewa Mh. Lowassa!
Kwanza ninajiuliza, wamempa Lowassa hiyo nafasi ya kuongea kwenye hiyo Jubilee kama nani? Lowassa si kiongozi wa Serikali, sio Mbunge wa Tabora, na wala sio Mkatoliki!
Ninachokiona ni kuwa kuna bidii nyingi na nguvu kubwa inatumika kutaka kumpa Lowassa nafasi ya kujionyesha ktk kila tukio kubwa. Kwa upande mwingine kuna nguvu kubwa ya namna hiyohiyo upande wa Chama chake cha CCM kuhakikisha kuwa Lowassa hapati nafasi ya uteuzi wa kugombea kupitia CCM ingawa ni kama wameelemewa na upepo wa mbisho kutoka upande wa Lowassa.
Najiuliza; hivi itakuwaje ikiwa Mh. Lowassa atatoswa na chama chake kuwania huo Urais? Mbona ni kama vile hiyo nafasi anaitafuta kwa udi na uvumba, na kwa kufa na kupona? Najisikia kupatwa na huruma upande mmoja na hofu kwa upande mwingine.
Vv