Hivi Lowassa asipoteuliwa kugombea itakuwaje?

Hivi Lowassa asipoteuliwa kugombea itakuwaje?

Mgombea wa ccm ni Jaji Ramadhani huyo fisadi hatumhitaji

Hii ni hatari sana kwa chama cha mapinduzi na Uhuru wa mahakama....watafanya hivyo kama wakiwaona watanzania ni wapuuzi!!
 
Siku moja arusha katika kumsimika askofu wa kkkt walikuwepo kina sumaye,nyalandu,mkuchika na wengine kibao hadi upinzani...lakini aliongea Lowassa tena alisema "hakuna mtu wala chama chenye hatimiliki ya nchi hii nchi hii ni yetu sote"watu nderemo na vifijo...hiyo ni nyota tu(kismati)😀
 
Hawana mwaka ccm imeshikwa vibaya kama mwaka huu.,ukilea lea lea kitu lazima siku kije kikudhuru,wameacha jamaa kajimbilikizia mali wee mpaka zinakosa pa kwenda.ng'ombe wako mwenyewe unakuchoma pembe,EL kawa maarufu kuzidi chama.
 
ccm hawawezi kumtosa el maana patachimbika,haiwezekani awekeze kwa miaka 10 kwa ajili ya uraisi halfu mumtose.
 
Kwani hana shuhughuli nyingine ya kufanya? Kwani sasa anafanya nini?
 
Jana ktk taarifa ya Habari ya saa mbili usiku ITV nilimuona Mh. Lowassa, alihudhuria Jubilee ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, Paul Ruzoka. Nilitegemea kuwa kiongozi wa Serikali ndiye angepewa nafasi ya kuongela LAKINI kwa mastaajabu alipewa Mh. Lowassa!

Kwanza ninajiuliza, wamempa Lowassa hiyo nafasi ya kuongea kwenye hiyo Jubilee kama nani? Lowassa si kiongozi wa Serikali, sio Mbunge wa Tabora, na wala sio Mkatoliki!

Ninachokiona ni kuwa kuna bidii nyingi na nguvu kubwa inatumika kutaka kumpa Lowassa nafasi ya kujionyesha ktk kila tukio kubwa. Kwa upande mwingine kuna nguvu kubwa ya namna hiyohiyo upande wa Chama chake cha CCM kuhakikisha kuwa Lowassa hapati nafasi ya uteuzi wa kugombea kupitia CCM ingawa ni kama wameelemewa na upepo wa mbisho kutoka upande wa Lowassa.

Najiuliza; hivi itakuwaje ikiwa Mh. Lowassa atatoswa na chama chake kuwania huo Urais? Mbona ni kama vile hiyo nafasi anaitafuta kwa udi na uvumba, na kwa kufa na kupona? Najisikia kupatwa na huruma upande mmoja na hofu kwa upande mwingine.

Vv
La kuuliza? Tanzania itasimama kwa dk kadhaa.
 
Kanisa Katoliki wamempa wasaa Lowassa aongee kwny jubilee? Hii haijawahi kutokea, basi ni kweli kanisa limegawanyika.

Nijuavyo mm msimamo ww kanisa ni kumpinga kwa namna yyt ile Lowassa kugombea Urais ktk kipindi chochote kile!
 
sikiliza Julius Mtatiro (CUF) anavyosema......

Hitimisho

Nguvu ya Lowassa ndani ya CCM haimithiliki na hofu ya chama hicho kuwa kumuacha nje ya ulingo kutakitetemesha haikwepeki. Lakini ukweli ni kuwa ndani ya CCM "kuna minofu mingi" ambayo inawazuia vigogo wakubwa wasiondoke na kuhamia vyama vingine hata kama hawakupitishwa kugombea urais. "There is too much stake to eat in CCM than going out".

Ndiyo maana bado CCM ina nafasi ya kujichagulia mgombea inayemtaka na vigogo wanaotajwa kuitikisa kama Lowassa wakiogopa kuondoka kwa sababu wamekaa serikalini muda mrefu na sasa hawawezi kumalizia maisha bila mfumo huo waliouzoea.

Kwa hiyo, nadhani Lowassa ataendelea kuwa mwanachama mtiifu kwa CCM akiwa Rais au akiwa raia wa kawaida. Kama kuna vyama vya upinzani vilikuwa "vinamtumbulia" macho kama fisi asubirivyo mkono wa binadamu udondoke, ni vyema vikajipanga kupata wagombea wake imara na vijijenge. Pamoja na yote haya namtakia kila la heri Mzee Edward Lowassa katika safari yake ya kisiasa.
 
Kivipi Dada? CCM hawatampitisha au Watanzania hawatampigia kura?

Vv

kwanza CCM hawatampisha, pili akiamua kuhamia chama kingine atagawa kura, kwa hio hatapata urais na iwapo akipitia uwanja wa nyuma basi atapigiwa kura ambazo hazitatosha kabisa
 
Hivi jaman,kuna ukaribu ganimkati yaviongozi wa serikal na maaskof hasa wakatorik + masheik?mi celew mwenzenu
 
Lowassa anasemwa kuwa ana nguvu chamaní. Anasemwa kuwa aweza kuparaganyisha chama endapo atakatwa jina au kutoteuliwa kuwa mgombea wa Urais. Eti,atakiyumbisha chama. Wapi!? Propaganda tu.

Lowassa ni mwanachama wa kawaida sana wa CCM. Hana ukubwa,umaarufu au nguvu zozote zisizo za kawaida chamani. Rupia zake zinamtangaza kama anavyoonekana. Yeye yu kinyume chake. Hakuna aliye juu ya chama. Hakuna maarufu zaidi ya CCM.

Lowassa haufikii mwangwi wa Mrema wa 1995. Mrema alihama chamani na hakuna lolote lililotukia. CCM ikapata na kupeta. Lowassa sasa anafika patamu. Sehemu muhimu. Hatua za hatamu. Ajitangaze,aulizwe na ajiandae.

Rupia hutoa mlio,rupia huchora uongo. Subirini muone filamu ya hamu. Mtaamini!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
hizo hizo rupia ndizo zitafanya wale wanaosema wanamtaka wakagawanyika wampitishe tuu kwani vipi mwenyekiti wa CCM anasaahau wanamtandao wenzake mbona yeye walimkweza au vipi mzee Tupa tupa mbona mpaka sasa hivi munavcheza kwa machale
 
mzee tupa tupa umesahau kwamba mmejiazinshia kautarabu ka kuwaweka watu madarakani kwa vigezo vya nguvu za rupia zao? kwani bila nyerere kuingilia kati 95 si ilikuwa rupia ishike hatamu. msiogope kula matapishi yenu
 
Lowassa anasemwa kuwa ana nguvu chamaní. Anasemwa kuwa aweza kuparaganyisha chama endapo atakatwa jina au kutoteuliwa kuwa mgombea wa Urais. Eti,atakiyumbisha chama. Wapi!? Propaganda tu.

Lowassa ni mwanachama wa kawaida sana wa CCM. Hana ukubwa,umaarufu au nguvu zozote zisizo za kawaida chamani. Rupia zake zinamtangaza kama anavyoonekana. Yeye yu kinyume chake. Hakuna aliye juu ya chama. Hakuna maarufu zaidi ya CCM.

Lowassa haufikii mwangwi wa Mrema wa 1995. Mrema alihama chamani na hakuna lolote lililotukia. CCM ikapata na kupeta. Lowassa sasa anafika patamu. Sehemu muhimu. Hatua za hatamu. Ajitangaze,aulizwe na ajiandae.

Rupia hutoa mlio,rupia huchora uongo. Subirini muone filamu ya hamu. Mtaamini!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Na bado!
Lowassa mnae huyo kama kupe la kwapani!
 
hakuna Mgombea mwingine wa CCM anayeweza kuzungumzwa humu jf isipokuwa Lowassa peke yake? kuna kina Membe, Wasira na wengine, mbona sioni wakuu mkiwajadili?

Au ndio methali ya Mti wenye matunda ndio wenye kupopolewa mawe?
 
Back
Top Bottom