Hivi kweli uchawi upo?

Hivi kweli uchawi upo?

Nikueleze mara ngapi kuwa haiwezekani kuprove negative?

Nimekupa mfano wa watu wawili kwenye chumba kisicho na kitu halafu kati ya hao watu wawili mmoja akadai ndani ya hicho chumba kuna kiti. Mwenzake akakanusha kwa kusema hakuna hicho kiti. Je hapa jukumu la kuthibitisha kuwa kiti kipo ndani ya hicho chumba ni nani?

Wewe inaonyesha huelewi logic ndiyo maana unarudia jambo nalokuambia.

Mimi nitaweza vipi kusema sababu za kutokuwepo uchawi angali nimeshasema haupo?

Hapo kinachotakiwa ni mwenye kudai uchawi upo atoe hoya mimi nikosoe kwa mapungufu nitakayo baini kwenye utetezi huo.

Ni sawa wewe unituhumu nimekuibia pesa yako halafu tena unaniambie niseme kipi kimenifanya nisidhani nimekuibia.

Hapo mantiki ipo wapi?

Ukishindwa kungamua haya nitajua wewe hujaiva kwenye kuchambua mambo critically.

Tatizo mkuu hatuelewani kwa sababu unanipeleka ambapo mie sipo. Haya madai ya kuwepo uchawi tumezaliwa na kuyakuta,sasa wewe pia unadai kuwa hakuna huo uchawi ambao watu wanadai kuwa upo.

Kwahiyo mie nilichotaka kwako ni sababu zilizokufanya kuona hili jambo la kuwepo uchawi si la kweli na ndiyo maana ukasema hakuna uchawi,maana umepinga madai ya kuwepo uchawi hivyo lazima utakuwa na sababu zilizokufanya ukatae hayo madai ya kuwepo uchawi na ndiyo hicho nachotaka.

Hivyo sio kwamba mie nataka ueleze kwanini hakuna uchawi kama ulivyosema.
 
Mkuu, embu nieleweshe,
Hivi? 'kuelezea sababu zinazofanya kwamba jambo la uchawi sio kweli' na 'kuelezea kwanini hakuna uchawi' ni mambo mawili tofauti?

"Kwanini" "kwasababu"
 
kwani wewe unadhani uchawi ni nini... ili tueleweshane
 
Mkuu, embu nieleweshe,
Hivi? 'kuelezea sababu zinazofanya kwamba jambo la uchawi sio kweli' na 'kuelezea kwanini hakuna uchawi' ni mambo mawili tofauti?

"Kwanini" "kwasababu"
Unapaswa ufahamu kuwa anachokifanya yeye hapa ni kupinga madai ya kuwepo uchawi hivyo lazima atakuwa na sababu zilizofanya apinge kuwepo huo uchawi ambao watu wanadai kuwa upo, sasa mie nataka kuzijua hizo sababu zilizofanya apinge kuwepo huo uchawi ambao watu wanadai kuwa upo.

Sasa yeye anaposema kuwa hawezi kueleza sababu za kutokuwepo uchawi inakuwa kama anamaanisha kuwa mie nimeibuka tu na kuanza kumwambia aeleze sababu za kutokuwepo kitu ambachohata hata yeye hakijui,si hivyo bali mie nimemuomba aeleze sababu za kupinga madai kuwa hakuna uchawi.
 
Inawezaka ni story kwako lkn kwa wengine is not a story.
Maswali.
1. Ww ni dini gani?
2. Unahudhuria kwenye nyumba za ibada
3. Una amini Mungu yupo?
4. Una amini shetani yupo?
5. Unaamini Majini yapo?
6. Una amini kuna nguvu za Mungu?
7. Una amini kuna nguvu za giza?
6. Una amini vitabu vya dini?
Tuanzie hapo kwanza. Nahitaji majibu. Ukishajibu nitakupa jibu kuhusu kile unachoamini
Facts

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bufa, sio vitu vya kusadikika, kama haujapatwa tafuta mtu aliyelogwa akueleze. Sasa unapingana na Biblia na Msahafu? Yesu hakuondoa mapepo? Umeshawahi kufanya biashara kwa kuzingatia kanuni zote lakini pesa haionekani? Uchawi upo sema watu wanautumia vibaya badala ya kujilinda. Ukiambiwa utalogwa kimbia haraka kajilinde kulingana na imani yako. Nimeshapatwa hivyo naongea kwa kujiamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda misungwi ukaone fisi wanabatizwa nahisi utapata kwa kuanzia utafiti wako
 
Kuna mtu kasema haamini huu upuuzi! Basi ukiamini Mungu yupo ni upuuzi, haonekani na uchawi hauonekani. Uchawi ni ushetani wa aina yake, kwa kua unaamini Mungu yupo na shetani yupo basi uchawi ni sehemu ya shetani, kwa hiyo uchawi upo. Labda unaekataa ujaribiwe kidogo tu usipotamani ardhi ipasuke uingie humo
 
Back
Top Bottom