Mimi sijasema uchawi upo au haupo ila wewe unasema haupo na ndiyo maana nikashawishika kwa kutaka kujua kutoka kwako kwamba umewezaje kujua kuwa uchawi haupo?
Kwa sababu ukisema tu kuwa haijathibitishwa kuwepo huo uchawi ndiyo sababu iliyokufanya useme hakuna uchawi sidhani kama utakuwa sahihi,chukua mfano leo hii kuna watu wanasema Ben saanane amekufa/ameuliwa. Lakini haijathibitika,je ndiyo unaweza kusema kuwa Ben yupo hai kisa haithibitika kama kafa?
Unaniuliza
"Umejuaje uchawi haupo"
Sentensi yako haina mantiki katika mjadala.
Mwanzo nimekupa angalizo kwamba
You can't prove negative. Haiwezekani kuthibitisha kitu kisichokuwepo.
Kinachowezekana kuthibitishwa ni kilichopo. Sawa?
Naona unanirudisha nilipokujibu
Ni hivi, kwa sheria ya logic haiwezekani kuthibitisha kitu kisichokuwepo.
Nasema logic kwasababu ndiyo itatupa mtiririko mzuri ili wote tuelewane.
Vinginevyo inakuwa mabishano yasiyo na mantiki.
Nirudi kwenye hoja
Hii sentensi "uchawi haupo" ni ukanusho kwahiyo haiwezekani kuithibitisha sentensi hii.
Ni sawa na watu wawili wameingia kwenye chumba kitupu halafu mmoja anadai ndani ya chumba hicho kuna kiti. Mwenzake anamwambia hakuna hicho kiti unachosema kipo. Hapo jukumu la kuthibitisha ni la mwenye madai.
Logic ni ngumu twende polepole.
Kama wewe hujui uchawi upo au haupo maana yake unapaswa upate uthibitisho kwa wanaodai iwepo wake.
Je sababu za kuthibitisha uwepo wa wadai yao unakubaliana nazo?
Kama ndivyo sema ni sababu ipi hiyo? Tutaijadili.